Familia inateseka sana. Nisaidieni natafuta Kazi, Kibarua

Familia inateseka sana. Nisaidieni natafuta Kazi, Kibarua

Hayo matatizo yatapita tu mkuu...usichoke kupambania familia.
 
Habari wana JF,

Mie kijana wa kiume, naishi Dodoma! Nina mke na mtoto mchanga wa miezi 4. Kitaalum ni muhitimu wa Bachelor ya Computer Science, na nilikuwa nimeajiriwa sehem lkn tulipunguzwa kipindi kile janga la corona limepamba moto.

Sina kazi maalum kwa muda sasa, naunga unga tu kiukweli, nikibahatisha kupata kazi ya mtu binafsi mfano kutengeneza website au la kidogo imekuwa ikinibeba hasa kulipia kodi, lkn sijapata hizo kazi kitambo sasa! nimejaribu sana na bado naendelea kutuma maombi lkn sijafanikiwa, hali imekuwa ngumu kweli kweli kwetu! Nafanya vibarua sometimes hadi vya kubeba zege japo tu familia ipate mlo hasa mke anaenyonyesha!

Lakini saa nane kasoro hii usiku naandika hapa, tumelala njaa, leo nimejaribu vibarua bila mafanikio, hatuna hata sh. mia hapa ndani, imeniuma sana ndio maana nimekuja kwenu kuomba kazi, kibarua chochote halali hata cha kipato kidogo tu!

Mtoto wa miezi minne imebidi tu aanze kunywa uji maana mlo wetu mmoja kwa siku mama anakosa maziwa ya kutosha!

Mwenye chumba kanivumilia hadi kachoka kaniambia nikabidhi tu chumba, japo hii laptop naitumia kwa kazi zangu, lakn kama kuna mteja wana JF naiuza laki3, au kama kuna mtu anakopesha niiweke bond, atunusuru tafadhalini tunatolewa kwenye hii nyumba!

Nipo tayari kuja popote kufanya kazi/kibarua chochote halali! Naombeni sapoti nateseka sana, hasa huyu mzazi kulala njaa hivi inanipa stress sana!

Kwa mawasiliano, namba zangu 0767 960 255 au 0629 531 358.

Natanguliza Shukrani na Mungu atubariki!
Pole mkuu me nilikua najua majanga matatizo ni mimi tu,ebu jaribu njia nyingine ya utafutaji maana mjini chakula kodi
 
Nenda hapo mjini ulizia zinapo patikana ofisi za kampuni ya ulinzi inaitwa GARDAWORLD SECURITY nenda pale hautakosa kazi mshahara wao ni 300,000 kwa mwezi ila utachukua 280,000 baada ya makato.

Nenda wale jamaa kila siku wanaajiri tena kama unaweza nenda Arusha kwenye ofisi zao hutochukua muda utakuwa umesha anza kazi.

Uza hiyo laptop muachie mke hela wewe kapambanie hiyo kazi
Mkuu umenena kiume mengi tunapitia Mali si kitu
 
Wengi vimo vinatuangusha mkuu, mi nimejaribu kwenda pale Mikocheni kila kitu kikawa sawa. But tatizo kimo tu, japo kuna wengine niliwaona nawazidi urefu ila wako pale wanafanya kazi. Nikasema haya bn, kisicho ridhiki hakiliki!
Ni kweli ndugu, ila yote ni mapenzi yake Mungu
 
ulikuwa wa 50K,nilianza na lita 20.....1500/lita, ilobaki kwenye hyo 50 nikanunua vidumu na mkaa,mie nilikuwa nayachemsha kabisa
Hili ndo jambo la msingi, kiume akitwambia mtaji alikuwa nao Kuna bnadam tunaweza kumpush...
 
Ukipata 50k utaanza biashara ya maziwa?

Mzunguko wake wa soko ukoje?
 
Kama huna uhakika wa milo 3 kwa siku na kibaruaau kazi ya uhakika please USIOE

Unatesa watu bure

Msikimbilie kuoa wakati wewe mwe mwenyewe maisha una unga unga .

Pole mleta mada utapata kazi
 
Ukipata 50k utaanza biashara ya maziwa?

Mzunguko wake wa soko ukoje?
Ndio naweza anza mara moja maana wateja tayari ninao,na tuna genge pia ambalo kwa sasa tumelifunga nafikiria wife akae hapo na maziwa yaliyochemshwa na bites coz anatengeneza bites yeye,wakati mimi nazungusha mtaani!Mzunguko wake sio mbaya,lita 20 namaliza ndani ya siku2,japo natamani ziishe kwa siku1,nafikiria kutengeneza vipeperushi nizunguke migahawani,japo niliwahi zunguka huko
 
Kama huna uhakika wa milo 3 kwa siku na kibaruaau kazi ya uhakika please USIOE

Unatesa watu bure

Msikimbilie kuoa wakati wewe mwe mwenyewe maisha una unga unga .

Pole mleta mada utapata kazi
Asante kwa ushauri,binafsi nilikuwa na kazi before! hata tulipopunguzwa kazini nilikuwa nafanya biashara ya maziwa,mambo yalizid kuwa magumu zaid baada ya wife kufikia muda wa kujifungua,akapitiliza,ikahitajika Operation,na ina gharama kiasi,akiba yote ikaishia huko,hadi mtaji pia!sikuwa na sapoti na kuanzia hapo hali ikawa mbaya sana kwetu
 
Pole sana kaka .... Mungu ni mwema na nina iman atatenda miujiza ktk hili, kikubwa tuzid kueka imani kwake ... pole ndugu
 
Ndio naweza anza mara moja maana wateja tayari ninao,na tuna genge pia ambalo kwa sasa tumelifunga nafikiria wife akae hapo na maziwa yaliyochemshwa na bites coz anatengeneza bites yeye,wakati mimi nazungusha mtaani!Mzunguko wake sio mbaya,lita 20 namaliza ndani ya siku2,japo natamani ziishe kwa siku1,nafikiria kutengeneza vipeperushi nizunguke migahawani,japo niliwahi zunguka huko
Big up ... komaa tu ndugu na kwa style iyo milango mingine ambayo hata haukuitaraji lazima itafunguka na kuna siku uliyoyapitia utakujaga kuyasahau na kujishangaa utakapofikia ... amini hili
 
Asante kwa ushauri,binafsi nilikuwa na kazi before! hata tulipopunguzwa kazini nilikuwa nafanya biashara ya maziwa,mambo yalizid kuwa magumu zaid baada ya wife kufikia muda wa kujifungua,akapitiliza,ikahitajika Operation,na ina gharama kiasi,akiba yote ikaishia huko,hadi mtaji pia!sikuwa na sapoti na kuanzia hapo hali ikawa mbaya sana kwetu
...dahh pole mwana
 
Big up ... komaa tu ndugu na kwa style iyo milango mingine ambayo hata haukuitaraji lazima itafunguka na kuna siku uliyoyapitia utakujaga kuyasahau na kujishangaa utakapofikia ... amini hili
Asante ndugu,naamini hivo pia!AMEN
 
Back
Top Bottom