Familia nyingine ni za ajabu sana

Bi mkubwa miaka 60+ nimchukue nije niishi nae dsm uswaz kwenye nyumba za kupanga mi mwenyewe sijaowa halafu nakaa chumba kimoja
Dah...pagumu sana hapo...ila komaa TU ndugu yangu...wasaidie ndugu zako... Hamna namna nyingine Mungu ndio ameshakupa mtihani huo...amini nakwambia familia zote zipo hivyo...tena familia nyingine zina vichaa Zaidi ya hao ndugu zako. Kikubwa usichoke kupambana,

jitahidi uzidi kunisaidia mama Yako kwani kama wewe TU unatumia kitendo Cha hao ndugu zako kuwa awana maisha ya kueleweka jua. Hata mama pia roho Ina muuma pia sema ndio hivyo kama mzazi Hana jinsi. Wazazi wanajivuniq sana kutuona tumefanikiwa...!​
 
Sorry madam point yako ni nini haswa kwenye hili ?maana unasema suala la uchungu wa mtoto as if ni la mama tu? Hata huyu mtoa mada anapitia uchungu kwa matendo ya kaka zake. Tusijifiche kwenye uchungu tukaacha kutafuta alternative solutions. Sio kila Mizigo ni ya kasafiri nayo mingine ni ya kuacha stend kama haina faida.
 
Shida huyu ana asili ya uchoyo ukimpa mtu oitu uwezi kumkata asitumie na mtu nisawa kumpa mtu gari afu umkataze asipakie rafiki zake
Pia na wewe unasili ya kulea ujinga hata wahisani wana masharti yao ukiona magumu acha kuomba. Faraja ya msaada ni kumsaidia mtu anayepambana kujikwamua sio sababu ni ndugu yako nikomae kusaidia majitu mazima hayana ulemavu wala magonjwa yanayotatiza uwezo wao wa kufanya kazi kisa sifa za kijinga eti sio mchoyo. BIG NO
 
Ndiomana wanawasumbua pole sana bro
Hapo wa kuokoa jahazi ni mama yako
Na mama ndio umwambii kitu kuhusu hao jamaa yani ukianza tu kuwaongelea bi mkubwa anaishiwa raha na ushirikiano kwenye maongez akupi ila umwambie tu kwamba kuna mtaji unataka kuwapa hao jamaa yani atafurahi kishenz
 
Kijana jitahidi hata kwahicho kidogo ulichonacho kugawana na ndugu zako, kwa life la kijijini hata ukiwa unawatumia just 10K kwa week watakuombea na kukushukuru.
Na sisi hatupo kijijini ni mkoani ndio ila tupo town kabisa tena kwenye wilaya inayobeba hadhi ya mkoa mzima
 
Shukran mkuu
 
Sawa mkuu
 
Kabisa mzee huku ni kutiana umaskini tu
 
Mi ningewachinjia NUNGWI kitambo sana.

Ningemchukua bimkubwa hao jamaa watajijua wenyewe.

Siwezi Lea mtu mzima tena mwanaume aheri angekuwa mwanamke au mwenye ulemavu.

Jitu unalipa Hela linakunywa pombe na wanawake tupa kule.

Kuna wakati lazima uwe ROHO MBAYA kweli Ili mambo yaende la sivyo utabaki pale pale hupigu hatua
 
Sanaa mi nimeamuaga tu kukaa kimya niliongea nikachoka,
nikawapa mitaji waliyotaka ili wajitegemee wakatafuna wakarudi palepale.
Mama yao nae ndo kiongozi kuwatetea
Na hao ni over 42

[emoji23][emoji23] ila kuna muda wazazi nao wanakosea ila ukisema uwaambie ukweli unaanza kupewa laana[emoji23][emoji23][emoji119]
 
Mimi siamini kwenye LAANA bwana wazazi wazamani walikuwa wachawi wachawi...ukiwazingua wanakuloga harafu wanajidai wanakulaani...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ila wazazii hapana
 
Haya mambo yapo sana,kuna familia moja bibi wa miaka 80 anawatunza wanae 60yrs mkubwa na 55yrs mdogo. Wote ni wanaume na hamna mwenye mke maana wake zao wote waliondoka wakawaachia watoto ambao ni wajukuu wa bibi sasa. Nao wajukuu wanamtegemea bibi kwa kila kitu. Ulevi ndo alama ya familia hii. Ukichunguza vizuri kuna laana au maagano yamo ndani ya familia hizi na zisipovunjwa huenda zikaendelea kuzitesa familia hizi. Ombea kizazi chako.
 
Mimi siamini kwenye LAANA bwana wazazi wazamani walikuwa wachawi wachawi...ukiwazingua wanakuloga harafu wanajidai wanakulaani...🤣🤣🤣🤣
Mi nilipigwa mkwara wa laana pale airport na maza nikamwambia kiungwana tu.
Umemaliza?
"Umeongea sana utakua na kiu wewe,twende ukapate soda"
Akasmile, nikampa soda yake.
Na mwenzake na visnack snack pale BP.
Nilivyoondoka hatukuonana wala kuongea miaka 10
Mpk alipoomba sana.
Msamaha
 
Pole sana mkuu. Namna rahisi ya kumuua kupe ni kumnyima damu. Kwa kuwa mama yupo peke yake kijijini (pamoja na hawo walevi). Nakushauri kama itawezekana kaka yako wa mjini amchukue bi mkubwa au umlete aishi kwako halafu tuone hawo walevi na malaya zao watakula nini. Simple like that!
 
Hao ndio ndugu sahihi wa kuwatoa kafara unateseka wakati mali zipo jiongeze
 
Kama kuna uwezekano, mchukueni bi Mkubwa muishi nae alaf nyumba pangisheni. Haya majamaa yaachieni chumba kimoja.

Hakikisheni hati na documents muhimu za nyumba mnazitoa hapo home. Baada ya hapo, hakuna tena sababu ya kuwatumia hela ya matumizi
Mkuu umemaliza kila kitu. Hakuna haja ya kuendelea kuwalea hawo jamaa kwa sababu ya uzembe wao wa ulevi. Wangekuwa walemavu hata mimi ningewaonea huruma na kuwatunza. Lakini kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi na wakipata pesa wanaenda kunywea na kut0mbEa, siwezi ku entertain ujinga huo. Ningekuwa mimi ningewatia adabu wasingekuja kunisahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…