Familia nyingine ni za ajabu sana

Walikuwa wanatuLoga harafu wanasingizia LAANA... Harafu utasikia nenda kamuombe msamaha mzazi wako...🤣🤣🤣
 
Kashasema bro wake amepata majanga hayuko vizuri.
Dogo nae ndo kwaanza ameanza anza life kapata kiajira.
So hapo utaona ugumu uko wapi.
Lazima dogo aanze kujiweka sawa baada ya kukesha sana sebuleni kwa kakaake.
Sasa kapata kiajira hao kupé kupitia mama yao ndo km vile wao wamepata ajira.
Kila mwisho wa mwezi/wiki wanadai chao.
Mama nae bila kufikiri huyo kumsumbua dogo "kuna shida lete hela."
Kumbe kuna hiyo mikunguni haina hela ya kulewea.
Conclusion
Ampige maza dozi ndefu ya sina hela.
Aongee na mangi jirani aweke bili na limit.
Maza atumiwe senti 2-3 za umeme kwa mwezi.
Shughuli iishie hapo.
 
hapo umenena mkuu
 
Yatakayotokea:

1. Nyumba wahuni watauza tu.
2. Wasipouza, Mama akifariki.
3. Watauwana kwa ugomvi, Jela.
4. Au wataingia kwenye kesi za miaka.

Nyumba haina maana yeyote au faida kwenye familia isiyokuwa na maelewano.

Yani hao wakaka wanasubiri urithi hapo ndio maana hawachezi mbali
Aisee kazi sio kuzaa,kulea ndio kazi
Mtoto hadi ajisimamie mwenyewe na kuwa wa kueleweka ni neema tu,kuna wazazi wana majeraha sana mioyoni mwao
Kamwe hakuna mtoto anaempenda mzazi kama mzazi anavyo mpenda mtoto
Ukiacha wazazi wachache wa hovyo
 
Mungu akutie nguvu uweze kufanya haya.
1. Nunua mashamba/ walime chakula chao
2. Nunua ng'ombe/ mbuzi,kondoo,kuku kienyeji.
Utapunguza tatizo hili.
Wataviuza washazoea kuiba na kutumbua hela
 
Ni nani aliyekuwa akimfungulia mlango huyo mpuuzi aliye fumwa koridoni?

Ujinga wa hao kaka zako nyuma yao kuna mama yenu ndiye aliye lifanikisha hilo akidhani ana waonesha upendo na kumbe alikuwa akimhujumu mmewe na uchumi wa familia kwa ujumla.
We jamaa ni genius dahhh umejuaje
 
Wakimchukua ni mkubwa,hao kenge hawachelewi kumlilia hi mkubwa,naye ni mkubwa Kwa huruma anaweza lialia wayasaidie tena

Kikubwa tia sumu ya panya kupunguza jam
Ndiyo maana ukawa mwalimu hapa Tanzania kwa roho yako mbaya[emoji1]
 
Mchukue bi Mkubwa uishi naye huko uliko then wale kaka zao mizigo acha wapambane na hali zao kule waliko.
 
Unadhani Mungu ni cheap kiasi hicho wa kumfuata simply tu muda unaotaka? Unadhani Mungu anamsikiliza kila anayemuomba na kumjibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…