Familia nzima yateketea kwa moto uliosababishwa na gesi

Familia nzima yateketea kwa moto uliosababishwa na gesi

King Kong III

Platinum Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
64,227
Reaction score
98,761
Umuofia Kwenu wana JF,

Bonne Annee and X-mas!!

Ndugu Sigfrid Sisti Kimbi na familia yake yote yateketea kwa moto uliotokana na gesi! Mke na watoto mapacha wawili ndio walianza kufa na mme amefariki akiwa njiani anakimbizwa hospital KCMC kwa matibabu.

=======

Ndugu zangu sisi familia ya Kimbi tumepata janga kubwa na msiba mzito ambao bila maombi hatuwezi kuukabili.
Ndugu yetu Sigifrid Sist Kimbi aliunguliwa na nyumba tarehe 25 kuamkia tarehe 26 na familia nzima wakiwa ndani wamelala. Bahati mbaya kabisa mkewe na watoto wetu wawili walifariki dunia siku hiyo hiyo kwa kuungua vibaya sana na moto huo.

Ndugu yetu alikimbizwa hospital na kuanza kupatiwa matibabu. Jana tuliendelea kuandaa mazishi ya mkewe na watoto ili tuwazike leo. Wakati tukijipanga jana jioni ndugu Sigifrid nae akafariki dunia. Kwa hiyo leo tunawahifadhi kaburini familia nzima ya Sigi Kimbi.

Kwa niaba ya familia tunawashukuru wote mnaoendelea kutushika mkono kwa chochote Mungu alichowajaalia katika kuhakikisha tunafanikisha mazishi haya. Tunaomba msichoke kutuombea maana jambo hili hi gumu mno ktk mioyo yetu. Peke yetu bila sala hatuwezi. Tunaendelea kuwashukuru sana.

Mazishi yatafanyika leo Uru Kisomboko karibu na Uru seminary. Mungu awalaze roho za marehemu pema peponi amina.

28/12/2020

Jamaa alirudi home amelewa
Akataka kupasha msosi ale, akawasha gesi hakuona kiberiti. Akatafuta kiberiti wee akaja kukipata late, kuwasha kumbe gesi ilikuwa ishasambaa sana.


TRG.jpg

TRG0.jpg

TRG1.jpg

TRG2.jpg
 
Back
Top Bottom