Familia ya GSM ilivyotembea kwa magoti korido za Ikulu kuomba Hayati Magufuli asiwafunge

Familia ya GSM ilivyotembea kwa magoti korido za Ikulu kuomba Hayati Magufuli asiwafunge

Acha ufala wewe! Nina elimu ya kumzidi huyo CAG wenu huko chooni kwenu Bongo... Na wewe nikuulize unaijua siasa wewe?!

Hiadhi maneno na ripoti zake CAG wa sasa na msikilize tena Rais wenu huyo akishakufa au akistaafu utaelewa.
Unamjua CAG!?..mbona umepanic!!?
 
Uzalendo ni kuiba 1.5 trilioni?

Uzalendo ni kuwabambikia watu kesi, kisha kuwapora pesa zao, na baadaye yeye binafsi kuzipora?

Uzalendo ni kuteka, kuua na kupoteza watu wenye kumkosoa?

Hivi kwa tafsiri yako mtu mzalendo ni mtu mwizi na anayeonea watu?
Can you prove???au ndio zile propagandq za cdm ,muacheni mzee baba apumzike alikuwa mzalendo wa kweli kazi yake imeonekana sio hao walamba asali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamjini wapo kazini cowboys tupo pembeni jamani. Ila lake zone Ni kiboko kwa uongozi. Hawatakigi utani Mana watu wao na wao Ni masikini so wanayo Ile feel yake.
Ila wengine wao Ni kujichotea ama kuiba hela za wananchi masikini kwa manufaa yao binafsi.cheki kwanza kwa taizi la malipo ya Arab contractor kinachoendelea,Mara Kuna 69bn za software ya kufuatilia umeme kukatika tu. Symbion wamefaulu kesi wanalipwa 300bn.
Yaani lake zone Ni Cuba ya Fidel ama Bolivia ya Che guavara, Thomas Sankara,jf Kennedy,Maduro,hugo Chavez ,Gadafi wa Libya,wale viongozi walio tayari kuifia nchi zao. Jamani msinishambulie Ila Kuna ukweli cheki uhalisia.
Nilimsahau comrade wetu mmoja Dr Edward Mondlane Sokoine huyu mziki wake unajulikana na wale waliozaliwa from 1970 backward after 70 Hawa Ni watt. Alikuwa mchunga ng'ombe. Yaani ukichunga ng'ombe sijui inakuwaje Ila unakuwa jasiri Mana inabidi uwatetee wasibiwe na ndio huo upendo unaleta kwa watu wako ikitokea kuwatala
 
Tunaendelea na visa na mikasa ya hayati JPM..

Hakuna siri JPM hakuwa chaguo la wana CCM mwaka 2015, hata mwenyekiti wa chama hakumtaka awe Rais bali alizidiwa na nguvu ya asili.

Mwenyekiti alimkusudia kumrithisha kijiti rafiki yake wa kitambo Bernard Membe,lakini wana CCM walimtaka Edward Lowassa.

Baada ya jina la Magufuli kuibuka kidedea kuna watu hawakulala siku hiyo. Tena sio wapinzani, bali wafanyabiashara na mafisadi ndani ya CCM, walijua kiama chao kimefika.

Mojawapo wa wafanyabiashara hao ni familia ya Bwana Ghalib almaarufu kama GSM.

Tukirudi nyuma kidogo hii familia ina asili ya mkoa wa Tanga na mzee wao marehemu Said Mohamed ambaye alifariki mapema mwaka huu alihamia huko Kusini mwa Tanzania na kujikita na kilimo na biashara ya korosho, alipozeeka akawaachia biashara vijana wake waziendeleze.

Pia hii familia imekuwa na ukaribu na familia ya mstaafu JK kwa miaka mingi.
Tufahamu kuwa JK aliwapenda sana watu wa mkoa wa Tanga kuliko watu wa mkoa wowote uli, labda ni kwa sababu alisoma Tanga School au kwa sababu wilaya anayotokea iko jirani na mkoa wa Tanga sielewi.

Nikikupa hapa orodha ya watu wa mkoa wa Tanga ambao walibebwa na JK kipindi cha utawala wake utashangaa,wengine hakuna aliyekuwa akiwafahamu wakalama post kubwa za ukuu wa mkoa,wilaya hata uwaziri ,achilia mbali post zingine za juu.

Kipindi hiki cha JK ndipo familia hii ya GSM nayo ikaibuka kama uyoga, kupitia kampuni zao za HSC na Silent Ocean wakaigeuza Kariakoo kuwa Dubai ya Afrika au China ya Afrika, wafanyabiashara toka nchi jirani wakawa hawaendi tena China kufuata mzigo mambo yote yaliiishia kariakoo.

Umafia wa kiwango cha juu uliofanyika bandarini na TRA na kampuni hizi ulivutia wateja wengi, mzigo ulikombolewa bandarini fasta na kwa gharama ndogo.

Kumbe nyuma yake kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za bandari na kodi za TRA, mabilioni ya shilingi yalihujumiwa na hii familia.

Baada ya hii jina la JPM kupenya sasa ikawa patashika nguo kuchanika wakawata na kuwazua wakaamua kuiua kampuno ya HSC wakijua tu ikibaki hewani JPM atowaacha salama.

Kupitia kampuni ya Law Domain Adocate tarehe 19 oct 2015 siku chache kabla ya uchaguzi mkuu,wakafile A notice of resolution to wind up voluntarily. Hii kwa wasiojua sheria, wind up ni kusimamisha shughuli za kampuni kisheria.

Walisahau kitu kimoja ila wakaja kukikumbuka baadae kuwa jinai huwa haifi, pamoja na kuwind up HSC kisheria bado wangekamatwa na kujibu tuhuma hata kama kampuni haipo.

Ile Silent Ocean ilibaki kuoparate kwa sababu inasemekana haikusajiliwa Tanzania japo iliwakenga wafanyabiashara wa Tanzania.

Sasa basi baada ya JPM kuingia madarakani, naweza kusema mwezi mzima alikuwa akishinda kama sio bandarini basi ni TRA, mabosi wa taasisi hizo mbili vitambi viliporomoka.

Vijana wake wakamletea ripoti ya wakwepa kodi maarufu,jina la HSC na Silent Ocean likiwa kidedea pale juu.

Matumbo moto wakajua hapa Segerea inawahusu, kama Manji alilala Segerea who is GSM?

Kwa kutumia ushawishi wa vijana wa mstaafu wakaomba apointment mara kadhaa kuonana na JPM.

Appointment ikawa approved wakaitwa Ikulu, kwa makosa yao walitembea kwa magoti kwenye korido mpaka ofisini kwa JPM. Akiwa na sura iliyokasirika akawaambia sitaki maelezo lipeni hizo arreas au Segerea inawasubiri

Yakalipwa mabilioni kimyakimya GSM dhambi zao zikasamehewa.

Plea bargain kwa wasiojua ilianza na hawa mabwana ila yao ilikuwa ya kimya kimya.

Kuanzia siku hiyo JK na JPM wakawa watu wa kutupiana vijembe hadharani kama utani vile kumbe wanajua kinachoendelea, ukitaka kula lazima uliwe.

Ikulu kutamu jamani
Kuna mengine hujaongea lakin
 
Unamanisha GSM WALILIPA MAHELA KIBAO ILA YALIKWENDA KWENYE MIFUKO YA BISWALO MGANGA NA MZEE KICHWA AU SIO
 
Ndo bas tena....afu Lowassa alishinda daa,CCM bhana,wakiamua kumweka MTU madarakani wanamweka,wakiamua kumtoa wanamtoa...ukigoma kutoka unanyofolewa roho.Hakuna MTU limbukeni kama mwanaadamu.....vyote anaviacha duniani lakini yupo tayari kumtoa roho mwenzie sababu ya Mali...mweee
 
Shukuru Mungu kuwa upepo wake haukukupitia!

Kumbuka: Wengine upepo uliwapitia kihalali (walikuwa waovu na mafisadi) na kuna wengine upepo uliwapitia kwa uonevu.
Kumpa mtu sifa zake hakuhusiani na upepo kupitiwa au kutopitiwa huwezi vunja Sheria za nchi au kwenda kinyume usiadhibiwe na ukiadhibiwa basi huyo mtu mbaya NO tatizo wabongo mshazoea uchafu na mnauona ni usafi, KAZI bila dili na rushwa huwezi fanya na mambo mengine ya kupindishapindisha ndio mnapenda
 
Wamjini wapo kazini cowboys tupo pembeni jamani. Ila lake zone Ni kiboko kwa uongozi. Hawatakigi utani Mana watu wao na wao Ni masikini so wanayo Ile feel yake.
Ila wengine wao Ni kujichotea ama kuiba hela za wananchi masikini kwa manufaa yao binafsi.cheki kwanza kwa taizi la malipo ya Arab contractor kinachoendelea,Mara Kuna 69bn za software ya kufuatilia umeme kukatika tu. Symbion wamefaulu kesi wanalipwa 300bn.
Yaani lake zone Ni Cuba ya Fidel ama Bolivia ya Che guavara, Thomas Sankara,jf Kennedy,Maduro,hugo Chavez ,Gadafi wa Libya,wale viongozi walio tayari kuifia nchi zao. Jamani msinishambulie Ila Kuna ukweli cheki uhalisia.
Kipindi cha Magufuli ndio Mnyeti na Makonda walikuwa watu wa kawaida sana ila baada ya kuteuliwa wakawa mabilionea
 
Wamjini wapo kazini cowboys tupo pembeni jamani. Ila lake zone Ni kiboko kwa uongozi. Hawatakigi utani Mana watu wao na wao Ni masikini so wanayo Ile feel yake.
Ila wengine wao Ni kujichotea ama kuiba hela za wananchi masikini kwa manufaa yao binafsi.cheki kwanza kwa taizi la malipo ya Arab contractor kinachoendelea,Mara Kuna 69bn za software ya kufuatilia umeme kukatika tu. Symbion wamefaulu kesi wanalipwa 300bn.
Yaani lake zone Ni Cuba ya Fidel ama Bolivia ya Che guavara, Thomas Sankara,jf Kennedy,Maduro,hugo Chavez ,Gadafi wa Libya,wale viongozi walio tayari kuifia nchi zao. Jamani msinishambulie Ila Kuna ukweli cheki uhalisia.
Kama makonda si ndio?
 
Nawashangaaga sana wale jamaa wanaojipendekezaga na hao kina Salaah, sijui GSM sijui nani... hao jamaa ni washenzi tu! Ndo mana wenzetu watasha wanafanikiwa sana! Ufanikiwe nchini kwao na kodi usilipe halafu na humohumo nchini kwao unapata wafuasi wanajitia marafiki zako wa karibu huku unawanyonya tu 😂

Dahh! Afrikaaaa ni nani alikuroga wewe na watu wako?!
Unapenda tuwe na watu kama makonda na sabaya? Au yule anayesema mukichagua upinzani sahauni mimi kuwaletea maendeleo jimboni kwenu? Au yule aliekabomoa nyumba dar ila kule mwanza akadai wasibomolewe kisa walimpigia kura?
 
Takwimu za ukuaji uchumi zikoje kabla na wakati wa utawala wake?..ili tuone huo uchumi uliivyokua unakua
Sina muda wa kuanza kukuandikia takwimu, we kama huyajui mambo hayo tulia tu....tangu huyu maza aanze kuwa kiongozi wa nchi akisaidiana na mafisadi uchumi unashuka tu daily, hadi aje kumaliza muda wake nchi itakuwa hoi. Tuombe Mungu rais ajaye asiwe pandikizi la hawa mafisadi nje na hapo tusahau maendeleo hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom