Familia ya Hans Poppe kutinga kwa Rais Samia kudai mabilioni ya baba yao yaliyoporwa na Hayati Magufuli kwenye ‘plea bargain’

Familia ya Hans Poppe kutinga kwa Rais Samia kudai mabilioni ya baba yao yaliyoporwa na Hayati Magufuli kwenye ‘plea bargain’

Kuna Dereva wake ( wa Familia ya Marehemu Hanspoppe ) Mmoja 'Mpenda Mbunye' Kawe aliniambia kuwa Boss wake Hanspoppe ameacha Pesa za Kula Wake zake Lukuki, Watoto na Wajukuu zake kwa miaka 100 ijayo.
BOSS BOSS alikuwa ameajiriwa kama MKURUGENZI WA KAMPUNI, lakini wamiliki wa hiyo KAMPUNI ni wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA VYA MWANZA [NCU], SHINYANGA [SHIRECU] na TABORA [WETCU].
 
Kama tunavyofahamu vigogo watatu wa SSC,Evans Aveva,Hans Poppe na Geofrey Nyange Kaburu walikuwa na kesi inayowakabili mahakamani.

Wakati Aveva na kaburu wanakamatwa Hans Poppe alishatoroka nchi kimafia.

RIP Hans Poppe,tangu umetutoka mwezi Sept, 2021 timu yako ya Simba inapata taabu sana
Ni Zakaria Hans Poppe.
Hans Poppe alikuwa baba yake. Naye ana historia yake kubwa katika Vita vya Uganda.
 
Kila shetani na mbuyu wake .
Pope kwa hapo alionewa ila naye ana madhambi yake mengi .

Tujikumbushe mtafaruku wake na boss wa keko juu ya kuficha sukari na mwisho mzee wa watu akaishia kupigwa risasi .

Dunia ya wananzengo wa keko ikasimama Pope akahudumia msiba mwanzo mwisho kwa vyakula na safari mpaka Moshi kumuhifadhi mtesi wake .

Waswahili na wahuni wa keko wakanywea naye akapita kimya kimya kama hakuna lililotokea .

Dereva wa boss wa Keko akaeleza A--Z uvamizi mpaka risasi kupigwa kwa boss wake na wahusika akawataja kuwa aliwaona na Pope akiwepo .

Dereva yule mhaya wa watu akachimbwa mkwara mnene akaona cha kufia nini ?

Akaondoka zake Dar es salaam sasa ni dereva Halmashauri moja huko Lindi anausukuma uzee kwa sasa .

Keep in resting easy Pope the real hustler japo ulipita kushoto sana japo sio kote ila baadhi ya sehemu [emoji24]
Weka yote mkuu. Boss wa Keko alikuwa nani? Keko gerazani au?
 
Kuna Dereva wake ( wa Familia ya Marehemu Hanspoppe ) Mmoja 'Mpenda Mbunye' Kawe aliniambia kuwa Boss wake Hanspoppe ameacha Pesa za Kula Wake zake Lukuki, Watoto na Wajukuu zake kwa miaka 100 ijayo.

Hivyo nimeshangaa leo kusikia kuwa Familia yake inapanga Kudai tena Pesa Serikalini wakati alishasamehewa na Hayati Dk. Magufuli ( kwakuwa tu alikuwa ni Mwana Simba SC Mwenzake ) Kesi yake Kubwa ya Uhujumu Uchumi kwa Kuingiza nchini Meli yenye Shehena ya Sukari Mbovu ( Feki )
Magufuli ili akusamehe ni lazima mpunga ukutoke tu ,iwe waziwazi au kimya kimya.
Ilikuwakama kituo cha polisi,kuingia bure kutoka na hela
 
Kama tunavyofahamu vigogo watatu wa SSC,Evans Aveva,Hans Poppe na Geofrey Nyange Kaburu walikuwa na kesi inayowakabili mahakamani.

Kesi yenyewe ni kutoa taharifa za uongokuhusiana na malipo ya kodi kifungu 106(1) AC(1) cha income tax sura 332 REF 2008

Wakati Aveva na kaburu wanakamatwa Hans Poppe alishatoroka nchi kimafia.
Ishu yake inafanana na mmiliki wa TP mazembe bwana Katumbi alivyowahi kutoroka nchi yake DRC miaka michache iliyopota kabla ya kurejea.
Kuna viongozi wakishika nchi kama una ugomvi nae lazima ukimbie.

Baada ya Hans Poppe kukimbia nchi akapokea ujumbe toka kwa Hayati kuwa arudi nchini hatofanywa kitu ila kwa sharti moja tu,alipe hizo hela dola zaidi ya 300,000.

Hicho ji kiasi kidogo sana kwa Poppe alikubali kurejea nchini Oct 16,2018 akapelekwa kwa DPP jambo la ajabu ikawa sio dola 300,000 tena bali akatakiwa kulipa mabilioni ya shilingi.

Kwa shingo upande akayalipa . kesho yake akapelekwa kisutu na kufutiwa mashitaka,hakuwahi kulala Segerea hata usiku mmoja tofauti na Aveva na Kaburu masikini jeuri ambao walisota sana Segerea.

Sasa familia inataka hizo fedha kupitia mwanasheria wao ,mapesa yenyewe tunaambiwa yalitoroshwa ughaibuni.

RIP Hans Poppe,tangu umetutoka mwezi Sept, 2021 timu yako ya Simba inapata taabu sana
Huu ulikuwa utawala wa shetani kabisa
 
Back
Top Bottom