Familia ya Ivan matatani kwa kufukia pesa ya Uganda

Familia ya Ivan matatani kwa kufukia pesa ya Uganda

Nilisema ni kinyume cha sheria zinazolinda pesa.Warejee maoni ya post ya awali.
 
familia ikili kukosa kaburi lifukuliwe mseveni atawasamehe
 
Nilijua ni tanzania tu, kumbe kila sehemu watu wanapenda kiki.

Hao wanasheria wamekosa kazi!
 
Zikuungua mzunguko unakuwepo tena au inakuwaje wao wameunguza pesa zao moto ulipita[emoji24] [emoji33] [emoji40] [emoji72] [emoji87]
 
Ni vyema wakafuatilia suala hili maana hali ya fedha ni ngumu kila pahala, ni afadhali hiyo pesa wangeipeleka kwenye vikundi vya watu wasiojiweza ikawasaidia
 
Itakua serikali imepungukiwa bajeti wanataka waongezee
 
Wanatafuta kiki ,hao ndio wale wana mavyeti mengi hila hana pesa matokeo yake anakuwa na hasira na mafanikio ya watu,kimoyokimoyo anajiona mpumbavu,akitafuta return on investment ratio
Nyamaza wewe haujui lolote
 
Wanasheria nchini Uganda wameamua kuifikisha familia ya Ivan Mahakamani kwa makosa ya kuzika pesa halali za Jamhuri ya Uganda katika kaburi la ndugu yao Ivan. Kwa nchi yoyote kitendo hicho hakikubaliki kwani pesa hizo zingeweza kutumika katika shughuli zingine na kukuza uchumi wa nchi.

Kitendo hicho kinakuja baada ya marafiki wa Ivan kumwaga mamilioni ya pesa ndani ya kaburi la Ivan kama njia ya kumuaga rafiki yao aliyekuwa maarufu kwa matumizi makubwa ya pesa.

Wanasheria wakiongozwa na Tugume Gideon wa Human Rights Defenders Association Uganda wamesema hawakufurahishwa na kitendo cha RICH GANG cha kuzika mamilioni ya pesa ndani ya kaburi, na kwa vile ni kinyume cha sheria,

wameamua kwenda mahakamani kuomba kaburi la Ivan lifukuliwe, pesa zitolewe zikafanye shughuli nyingine na waliohusika washitakiwe kwa kuharibu kwa makusudi alama ya taifa.

View attachment 517701
Pesa madafu bhabha sio issue.....
Zingekua dolar ingekuw baridi tu ila pesa ya Africa kila mtu anatoa macho,....
 
Wako sawa kabisa,,bora wangefukia magari au dhahabu na vyeti au wangemjengea nyumba waiezrke alafu waifukie
 
Back
Top Bottom