Hahaha nchi ya wezi hii, alipokuwepo Magufuli alianza kujaribu kuwaweka hadharani. Watu tulipinga utaratibu alioutumia, tukamuita katiri, roho mbaya na kila kitu.
Leo Rais SSH kawaacha wezi wale kwa urefu wa kamba zao, tuna lalamika. Shamba la bibi, kila kitu Zanzibar, kila mtu anakula atakavyo, upigaji wa kufa mtu, na kila kelele tunazozisikia.
Hii yote ni kwasababu watu wana jaribu kulinganisha njia za mwenda zake na huyu wa Kizimkazi.
Leo watu wanatafuta kufukia legacy ya mwendazake kwa kumuhusisha na mauaji ya watu tusio fahamu wamefariki au la.
Wanataka watu waone kukemea uovu ni dhambi, na majbazi yanataka yaendelee kuiba.
Sisi tunaoibiwa tunashangilia mipango ya waovu, na kadri tunavyoendelea hivi naamini hawataki tupate kiongozi mwenye uchungu na nchi na mali za nchi kwa manufaa ya wengi.
Akipatikana wanaanza kumtisha, walikuwepo kina Magufuli, wako wapi.
Jamani haya maneno tukizushiwa sisi hatupendi, kwanini tunawazushia wengine?
Tuletewe ushahidi tuache hizi story za kusadikika.
Tusiwe wepesi kudanganywa na kudanganyika.
Sio kila kibaya kinachosemwa kuhusu tusio wapenda ni kweli.