Familia ya marehemu Joe Mutaboyerwa yavamiwa. Mama na watoto wawili wauawa

Familia ya marehemu Joe Mutaboyerwa yavamiwa. Mama na watoto wawili wauawa

updates
Dar Es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Shadrack Kapanga (34) kwa tuhuma za mauaji ya mama na watoto wake wawili eneo la Masaki mtaa wa Maryknol.

Kapanga ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani alikamatwa jana Ijumaa Juni 11, 2021 eneo la Magomeni akiwa kwenye harakati za kutoroka baada ya kuwaua Emilly Mutaboyerwa ambaye ni mama na Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Juni 12, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba baada ya kufanya tukio hilo.

“Vitu alivyokutwa navyo wakati akitoroka ni simu za marehemu, televisheni, king’amuzi cha DSTV na rimoti,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Muliro ameeleza kuwa upelelezi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la mauaji Juni 9, 2021 baada ya kuwapiga kila mmoja kwa wakati tofauti kwa kitu kizito na kuwasababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

“ Baada ya kuwaua aliwafungia ndani na kutoroka. Upelelezi wa shauri hili unaendelea ili kujua sababu za msingi za mauaji hayo na mara utakapokamilika mhusika/wahusika watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,” inaeleza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia ya leo mambo yalivyo unatakiwa uwe makini na kuto amini Binaadamu yoyote yule, Na ni muhimu sn kujiwekea HIDDEN CAMERA ndani kwako au hata CCTV CAMERA ndani kwako kwani husaidia kujua mambo mengi sn katika nyakati tofauti.
 
Wanawake bhana!! Mume kafariki juzi tu keshapata HAWARA hadi anajua nyumbani kwake na hela zilipo!!!! Huyo hawara anayepajua home mume kafa juzi tu lazima alikuwepo kabla. Mjane anaishi mwenyeweee na wanawe tu very selfish utakuta hapo wakwe, mawifi na mashemeji aliwakatia laini wasiguse urithi alioachiwa akaamini mlinzi na kibenten.. Matokeo yake watoto malaika wanauwawa very sad!!!
Mwanamke mshenzi sana lazima huyo jamaa alikuwa anamla hata kabla ya jamaa kufariki sababu amemuamini vipi mpaka kujua deal za mwanamke na kujua kwamba ana hela nyingi? Women bana tinahangaikaga sana kuwatafutia hela Ila hawana maana kabisa
 
Ulitaka Mshana Jr. aende amuulize umri wako, shughuli zako ni zipi, una miliki mali gani!!!!!!

Watu wengine bana, sijui!

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma na usome tena nilichoandika
Huwenda ukaelewa nilichomaanisha

Watu wanamlaumu marehemu kwa kutembea na kidogodogo ilihali habari haijataja hata umri wa huyo boyfriend

Sijamtaka mshana kutaja umri wa mtu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
mahusiano ya kimapenzi yasiyo rasmi ni kukaribisha mauaji.
zama hizi watu wanatamaa na fedha hatari, hata ndugu yako usimuamini. mbaya zaidi kwenye mapenzi ndio hatari zaidi.
tulio baki hai tujifunze ili tuepuke kupoteza uhai kizembe.
 
Wajameni, this is very sad!. Emmy Kaungamno, alikuwa jirani yetu next Door, enzi za udogoni pale Drive in Flats, "mafletini". Last Sunday nimesali Msasani Lutheran, nikasalimiana nae, na kujoke, how come, she looks so cute as if she is early twenties, na kusema lazima kuna watu wanatunza!, akasema thanks, hakuna mtu ni Almight God only!. Its as if alikuwa anatuaga!. So sad!.
Paskali
Paskali una undugu na pisikali ?
 
Back
Top Bottom