Mbona story yako haingii akilini kabisa?House boy au boyfriend kumuua huyo dada kisa mali? labda uniambie kama walijua kuna kiasi cha pesa kiko ndani ya nyumba na walishindwa kukichukua kwani wao walikuwa kikwazo na bado njia hii mbona haiingii akilini kwanini wasingelikodi majambazi wakaiba hiyo pesa kama pesa ilikuwa ndani bila kuacha mianya wao kujulikana walikuwa bedhind.?
Kw mbinu hii ni wazi wahusika sio walio tajwa maana watajwa hawawezi kunufaika na hizo mali ambazo haziamishi na ziko kwenye maandishi ,labda ndugu wa mama au mume na kwenye hili ni ndugu wa mume wanaweza kuwa suspect no 2 kama sio n0 1 maana wao ndio wanaweza kumtuma yeyote kati ya watajwa kutekeleza mauaji maana wao ndio watakuwa wanufaika wa mali baada ya wahusika muhimu kutangulia mbele ya haki..
Hivi mahusiano ya huyu dada na ndugu wa mume na ndugu zake wa tumbo moja yalikuwa ya aina gani? ukitaka kujiuliza zaidi jaribu kufikiri kuhusu mtu kuamua kuishi na watoto wake tuu na mfanyakazi wa kiume na sio wakike..... huyu mtu hakuwa na watu wa karibu au ndugu hata mmoja wa kuishi nae au hata ndugu yake? kuna shida hapa hasa ukifikiria mazingira ya kitanzania.
Hivi vifo vinaweza kuwa na sababu nyingine kabisa kama house boy ni muhusika wa moja kwa moja lakini kama ametumwa basi si muhusika wa moja kwa moja na pesa itakuwa imechangia na wahusika wakuu hawawzi kuwa boyfriend na house boy,