Huu mfano wako hauendani kabisa na hoja yako unayo jaribu kuitetea hapa,nikukumbushe tu pengine,hoja yako ni kuwa “badilisha Dada/Kaka wa kazi nyumbani hata kama anafanya kazi vizuri na hana tatizo kisa amekaa muda mrefu na kazoea “
Narudi kwenye uhalisia sasa,unajua madhara ya mathalani kukaa unabadilisha Dada wa kazi ndani katika malezi ya watoto wako wadogo? Yani kila baada ya mwaka mmoja unaondoa Dada waliyemzoea tena anatimiza wajibu wake vizuri na pengine watoto wanampenda sana kisa tu kazoea unaleta tena Dada wa kazi mwingine. Yani watoto kila baada ya muda wanakuwa ni wa kuji adjust kulingana na Dada wa kazi aliyepo? Kwa Mzazi yoyote mwenye kujali malezi ya watoto wake wadogo hawezi ondoa Msaidizi wa ndani bila sababu maalumu.