Kite Munganga
Platinum Member
- Nov 19, 2006
- 1,773
- 952
weka ushahidi wa upuuzi uliouandika. Umbea tu mwisho utavalishwa kanga
Mbona wewe wavalishwa shanga sie hatusemi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
weka ushahidi wa upuuzi uliouandika. Umbea tu mwisho utavalishwa kanga
Yericko umejidhalilisha kwa habari ya hovyo kama hii...!
Huyu Yeriko amekua mara nyingi akileta mabandiko ya kipuuzi.unapata raha gani kutunga na mimi nawashangaa waliochafuliwa peleka muhunu huyu mahakamani
Chadema tabia ya kuchafua watu msidhani siku mkipata madaraka mtabaki salama.lengo lako ni nini kama unadiriki hata kutaja vitu bila ushahidi.shame on you
Suala hili limeanigusa kipekee naumia sana nasononeka sana kuona tabia ya kuiba fedha za UMMA uku na viongozi wa upinzani wakitajwa. Hapa "Black Movement Uprising" is inevitable. Ndg, Watanzania hii ni hatari kwa Taifa maskini kama letu watu wanajinufaisha tu wao huku tukiwa bado kwenye umaskini wa kutisha nenda vijijini hakuna maji, umeme, afya boro na uzazi salama kwa mama yangu na mama yako wewe, elimu ni shubili, miundo mbinu ni patashika, wakulima, wafanyakazi, wavuvi na wafugaji ni balaa tupu tumekuwa Taifa la dhuruma kila mpata nafasi ni kuiba, kuaribu na kuvunja hakuna anayejali wote wamepotoka kwa wizi wa mali za UMMA. Mwl Nyerere naamini upo nipe moyo wa ushujaa kuiokoa Afrika na watu Mungu tangulia wote wenye nia ya dhati kulikomboa Taifa langu Tanzania Usawa na Ubinadamu wetu ni muhimu sana. Lot's Of Love To All Reformers.
Familia ya jk ni kubwa sana sijui inawezaje kuhusika yote watanzania wote ni familia ya jk kama hawa.
Tatizo ni kwamba hana watu nyuma yake. Mtu kama Cheyo chochote atakachosema watu watampuuza tu kwa sababu ameshadhihirisha hiyo element ya upinzani hana. Mtu yeyote atakayetaka kucheza mchezo kama huo ni lazima awe na time inayoaminika... kwa mfano, kwa upande wa CCM huwezi kumuhonga mtu ambae unajua A-Z kwamba hata asipopewa chochote lazima ataitetea tu serikali yake lakini utatafuta watu ambao wanaonekana kama rebellious kwa serikali yao wenyewe ambao hata wakipinga kwamba hakuna wizi watu wanaweza kuamini kwavile hapo kabla walishajenga tabia ya "kutoogopa" panapo ukweli! Kwa CCM watu kama akina Kangi Lugola, yule mbunge wa Simanjiro, akina Filikunjombe, Kessy nd the like ndo watu wa kuwaangalia na ukija huku upinzani huna haja ya kupoteza muda kwa mtu kama (nimesahau jina... yule mrs. Nyerere), Cheyo, Mrema ambao unajuwa kila mtu ameshawapuuza! You pay millions only to credible voices but not any voice... hivi assume umempa fungu lake mtu kama Lema, Mbowe Dr. Slaa, (kama angekuwa mbunge), Zitto(ingawaje watu hawamuamini), unafikiri utahitaji back up nyingine zaidi ya hao?Mkuu Cheyo hana impact kweli?
Mwenyekiti wa TCD, au umesahau michango yake bungeni kuhusu kuuponda upinzani?? think broader
Duh! Mkuu, hapo mjepo umemuingiza kimakosaKuna kila dalili kwamba viongozi wakuu wa vyama vya upinzani waliotajwa katika report ya CAG wanatoka CHADEMA.Hii inatokana. na sintofahamu,taharuki na nia ya dhati kupotosha ukweli,dhihaka kwa watetezi na kuwachafua imejionyesha dhahiri chini ya vibaraka wao mjepo Nguruvi3 Yericko Nyerere IKWETE POMPO.
Ufisadi wa dola 250m (zaidi ya 400bn) umetikisa nchi kwa kuikosesha takribani miradi ya sh 3trilion imefahamika. Kampuni ya PAP ilipewa dola 122m (200bn), na kusaini makubaliano kikao cha kunduchi beach hotel oct8.2013 kuwa kiasi kilichobaki (128m au zaidi ya 200bn), PAP watalipwa kila mwezi 8bn mpaka deni kwisha.
Kampuni hii ya PAP iliyopewa tuzo hiyo ya 400bn kwa kuwekeza 6mTsh tu ni ya nan? Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, 50% inililiwa na Singh Sethi(singasinga) na mwanae na asilimia 50% zinamilikiwa na kampuni ya Simba Trust ya Australia.
Simba trust ni nan.? Uchunguzi umeonesha kuwa Simba trust ya Australia inamilikiwa na watu wawili ambao ni salima Kikwete na Miraji Kikwete.
Uwepo wa majina haya mawili kama wamiliki wa PAP inatafsiriwa kuwa ndio sababu kuu ya JK kuvuta miguu huku nchi ikiumia.
Kwa mkataba huu wa IPTL wa 100MW wa miaka 20 (1995_2015), umeongezwa miaka mingine 20 (2013_2033)kwa kuzalisha 500MW.
Kwa mujibu wa mkataba huu, kampuni ya PAP italipwa 400m kila siku kama capacity charges . Maana yake singasinga mwenye 50% atapata 200m kila siku. Na watoto wawili wa JK watapata kila mmoja 100m kila siku hadi 2033.
Uwepo wa familia ya JK kwenye ufisadi huu inadaiwa ndio Kinga ya wahusika ; Muhongo, werema, maswi, mramba, likwilile na hata waziri mkuu kutetea
Ushahidi unakwenda kuonesha kuwa hata uamuzi wa Gavana kuruhusu fedha hiyo itoke kimakosa ni baada ya kupata MEMO kutoka Katibu wa rais Bw Mbena ikisema Rais kaelekeza.
Na ni sababu hiyo pia baada ya Dr Hosea kuwasilisha report kwa rais, JK alisoma na kumjibu achana nayo na ndio maana mpaka sasa report hiyo haijapelekwa kwa DPP ili.wahusika wafikishwe mahakamani
KAMA SEHEMU YA MWANGAZA.
Napenda kuwakumbusha Watanzania, Mataifa ya Ulaya na Marekani huwa hayakurupuki kutoa shutuma, ukiona wanatoa tamko ujue wana uhakika. Walieleza juu ya meli za Iran kutumia bendera ya Tanzania, Membe alikurupuka kukanusha kama kawaida yake, baadaye ikadhihirika ni kweli.
Mataifa ya Ulaya yalitishia kusimamisha misaada kutokana na ufisadi wa Richmond, kwanza serikali ilikanusha baadaye ilidhirika kuwa ni kweli kulikuwa na wizi.
Mataifa ya Ulaya yaliwahi kuelezea ufisadi katika manunuzi ya radar, serikali ikatoa maelezo marefu kuonesha hakuna ufisadi, baadaye ikadhihirika ni kweli.
Sasa wametoa tamko kuwa hakuna msaada kutolewa kwa Tanzania mpaka waone taarifa ya CAG kuhusu ufisadi katika akaunti ya Escrow, serikali imekanusha hakuna ufisadi.
Vyombo vya habari vya Ulaya vimeeleza kuhusu kuhusika kwa serikali ya Tanzania, CCM na China katika biashara haramu ya pembe za ndovu, Membe kama kawaida yake amekurupuka kukanusha lakini mambo hayo yote yatakuja kudhihirika kuwa ni kweli kwa 100%.
Taarifa ya Escrow ipo tayari lakini yaliyomo ndani ni balaa maana ni zaidi hata ya wananchi walivyokuwa wakiitegemea.
Hii iliyopo chini ni kama tetesi lakini ni tetesi yenye uhalisia. Endeleeni kufuatilia kashfa hii kubwa inayogusa ofisi kubwa zote za nchi.
______________________________ ______________________________ ____________
Ikiwa ni siku chache tangu Baraza la Usalama la Taifa kukutana na kupitia ripoti ya uchunguzi ya PCCB kuhusu ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni 200 kwenye akaunti ya Tegeta escrow Benki Kuu, Taarifa za uchunguzi zinaeleza kuwa mkurugenzi wa PCCB Dr. Edward Hosea atamkabidhi Mh. Rais Jakaya Kikwete ripoti hiyo Jumatano ijayo kama ilivyoelekezwa na Baraza la Usalama wa Taifa.
Awali ripoti hiyo ilikuwa akabidhiwe Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lakini taarifa za ndani zinabainisha kuwa uzito wa ripoti hiyo unastahili Mkuu wa nchi mwenyewe kwani kuna maeneo ambayo Waziri Mkuu atastahili kuwajibika.
Ofisi nyingine zilizohusika kwenye ufisadi huu kwa mamlaka yao ni Wizara ya Fedha, Benki Kuu, TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, TRA, na baadhi ya vigogo Ikulu.
RIpoti hiyo imekwenda mbali zaidi kuonesha baadhi ya majina ya watu maarufu waliojipatia fedha hizo kwa namna mbalimbali. Kwa mfano, akaunti ya kampuni ya VIP Engineering katika Benki ya Mkombozi iliyopokea hela za escrow imekutwa hela nyingi zimetoka kwenda kwa Wabunge,Mawaziri Majaji, na baadhi ya watu maarufu (hii ni kwa mujibu wa benki statement ya akaunti hiyo yenye kurasa 27 kuanzia tarehe 20 Januari mpaka tarehe 14 Agosti 2014).
Baadhi ya majina ndani ya benki statement hiyo yalitumiwa pesa kupitia akaunti hiyo ni pamoja na Waziri Anna Tibaijuka, Waziri wa zamani William Ngeleja, Mwanasheria Mkuu wa zamani Andrew Chenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na mmoja wa Majaji wa mahakama kuu ya Tanzania Mujulizi. Katika orodha hiyo kuna Wabunge, wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini, wote isipokuwa mmoja tu ambaye ni mtumishi mwandamizi wa zamani wa Serikali. Viongozi wawili wakuu wa vyama vya siasa vya upinzani nchini wameonekana katika orodha hiyo pia.
Juhudi kubwa zinafanywa hivi sasa kuzuia taarifa ya CAG na PCCB isikabidhiwe Bungeni kwani kama itakuwa wazi inaweza kusababisha kuibuka kwa mtikisiko mkubwa.
Kwani unadhani Rais anaweza kuondolewa kwa uzushi wa wapuuzi kama akina Yeriko?Hivi kuna namna ya kumshtaki na kumuondoa Rais kabla ya 2015? This is too serious to have this nuts in the highest office of the country!!
Suala hili limeanigusa kipekee naumia sana nasononeka sana kuona tabia ya kuiba fedha za UMMA uku na viongozi wa upinzani wakitajwa. Hapa "Black Movement Uprising" is inevitable. Ndg, Watanzania hii ni hatari kwa Taifa maskini kama letu watu wanajinufaisha tu wao huku tukiwa bado kwenye umaskini wa kutisha nenda vijijini hakuna maji, umeme, afya boro na uzazi salama kwa mama yangu na mama yako wewe, elimu ni shubili, miundo mbinu ni patashika, wakulima, wafanyakazi, wavuvi na wafugaji ni balaa tupu tumekuwa Taifa la dhuruma kila mpata nafasi ni kuiba, kuaribu na kuvunja hakuna anayejali wote wamepotoka kwa wizi wa mali za UMMA. Mwl Nyerere naamini upo nipe moyo wa ushujaa kuiokoa Afrika na watu Mungu tangulia wote wenye nia ya dhati kulikomboa Taifa langu Tanzania Usawa na Ubinadamu wetu ni muhimu sana. Lot's Of Love To All Reformers.
......maneno mengi ya nini?..tushikeni mashine...yote yatajipa.
kwani unadhani rais anaweza kuondolewa kwa uzushi wa wapuuzi kama akina yeriko?
Halafu kinachokera zaidi ni hii michango ya ujenzi wa maabara, wazazi wetu masikini wanakimbia familia zao sababu ya huu upuuzi kumbe mshiko mnene unanufaisha familia zisizozidi 10.Nadhani upinzani wajipange wachukue dola kidemokrasia rather than mapinduzi au kuingia barabarani, haitaleta afya kwa watanzania.ukawa wajipange vizuri maana karata wanazo za kutosha kwa sasa
Leteni hiyo ripoti sasa!! mbona mnaficha>??? Help us catch the rat!!!Kwani unadhani Rais anaweza kuondolewa kwa uzushi wa wapuuzi kama akina Yeriko?