hapa tatizo kuna wachumia tumbo wasiokua na akili ndio wanatuvuruga ila niwaambie hizi mali za wananchi mnazokula ipo siku mwisho wenu utafika.walikuwepo watu wezi kuliko nyinyi lakini wamepita na nyie panya na ukoo wenu tuueni tuu wananchi kwa kutunyonya pesa zetu lakini na nyie mtakufa.sina cha kusema ila kwa mwananchi masikini kama mm nimekasirika zaidi kuona wananchi wenzangu wakimtetea huyu rais ambae hajawahi kumchukulia mtu hatua kila wizi na yeye anahusika.
Mkuu Legendari, hili la kufa ndio njia yetu sote, matajiri, watakufa na sisi masikini, tutakufa!, tofauti yetu ni kuwa kwa vile sisi masikini tunafukiwa ndani ya mwandani, miili yetu itaoza na kuliwa na udongo, matajiri wao wanazikiwa masandukuni, kwenye majeneza ya gharama, na makaburi yaliyojengewa kwa marumaru, hivyo wao hawaozi, mule miili yao, inaishi milele!.
Aliyekupa wewe kumbi, ndie aliyewapa wao kiti!, anayefanikisha wengine wapate humu Duniani ni Mungu, tena formular yake iko very open, "mwenye nacho, ataongezewa, asiye nacho, atanyang'anywa hata kile kidogo, alichonacho!", Ugumu zaidi ni mbinguni kwa Mungu BABA, matajiri wana sehemu yao, inayofanania utajiri wao, na sisi masikini tuna yetu, sana utakachoweza kufanya baada ya sote kufa, ni wewe kuwaona tuu na kuwapungia!, fulani yule!, ukiondoka masikini, hata kule utaendelea na umasikini wako, usije kufikiri, wakifa, kule mbinguni utajiri wao, ndio utapewa wewe!.
Pole!.
Pasco.