Minabusu, hapa sasa tunazungumzia vitu vingine tofauti, mimi nazungumzia umiliki wa kampuni kwa mtoto ni independent ya mzazi!, wewe sasa unaleta mambo ya eskrow!.
Mambo ya kampuni yanaitwa duniaya ya makampuni, "the corporate word" ambapo kampuni kisheria ni mtu, an entity of its own, independent na wamiliki!, na ikitokea mmiliki ni mtoto wako, wewe kama baba huna any legal resiponsibility kwa mwanao over 18!, akiboronga, ameboronga yeye!.
Kampuni inaweza kushitakiwa mahakamani na ikatozwa fidia ikalipa bila wamiliki kuhusika kwa lolote!, ila inapotokea, kampuni ikafanya kosa la jinai, la kulazimisha mtu kwenda jela!, hapo ndipo mahakama hufanya kitu kinaitwa "un veil the corporate veil" ya wamiliki, ambao sasa ndio watashitakiwa kwa kosa la jinai na watakwenda jela!.
Tukija kwenye issue ya escrow, hii ni account maalum ambayo hufunguliwa kunapotokea ugomvi wowote kati ya wamiliki, mfano Mimi Pasco wa JF na Muna, tumeanzisga kampuni yetu ya PASUMUNA, then tukatofautia kuhusu umiliki, au mgao wa faida, mimi nakushitaki na mahakama inaamua, kufuatia ugomvi wetu, fedha na mali za kampuni, zitakuwa chini ya uongalizi wa BOT hata suluhu itakapo patikana!.
Ndivyo ilivyokuwa IPTIL wabia ni mtu anayeitwa James Rugemalila wa Mabibo wines ameingia ubia na kampuni ya Mechimar ya Malesia kwa makubaliano ya 70/30, wakapata tenda Tanesco, mgao ulipotoka Mlalesia akagoma kumlipa Rugemalila ile 30 % yake kwa hoja ni kubwa mno huku Ruge amechangia mchango sifuri!, ndipo Ruge akaenda mahakamani kumshitaki partner wake!. Sasa hapa ndipo escrow account ikafunguliwa hadi mgogoro uishe!.
Singa Singa wa PAP akala dili kujifanya ameinunua IPTL 100% percent, na kuwasilisha vithibitisho vya ununuzi, Ruge akafuta kesi, hivyo kukawa hakuna tena kesi, kufuatia taarifa ya kufutwa kesi BOT ikaifunga hiyo escrow na kumpa Singasinga fedha zote!.Kama BOT ilifungua escrow kufuatia mgogoro, sasa mgogoro umeisha, kwa nini asirelease hizo funds!.
Uchunguzi ukithibitisha Singa Singa ni tapeli, hakununua, hapo ndipo kutakuwa na ngoma!. Na kama parners wa Singa Singa ni kijana na binti mfame, mfalme hahusiki!, ni vijana wake wakubwa!.
Nawaomba tusishabikie sana suala la nani ni mmiliki, hivi mnajua kuwa Richmond ndio Dowans ndio Simbion, mashine ni zile zile, gharama ni zile zile, na wamiliki ni wale wale, ila tuu, majina ndio wamebadili!, kuna anyone anaye bother mmiliki wa Simbion ni nani?!.
Pasco.