Consultant
JF-Expert Member
- Jun 15, 2008
- 11,503
- 20,892
duh! Naona ndo umeamka baada ya kukesha kubadili wanaume Jolie Club. Haya sasa hoja hii ina uhusiano gani na escrow?
Waombe tu apone ili waendelee kuikalia hiyo ripoti.
Hii nayo ni list of shame namba 2 Kwenye list of shame namba 1 mkuu wa familia ya rais yumo, hii namba mbili watoto wake wamo. Inatisha. Kweli ikulu ilishabadilishwa kutoka mahali patakatifu mpaka pango la wanyang'anyi. Mimi naona wakati wa utawala wa Ben ndipo maasi makubwa yalifanyika pale ikulu ikuiwa ni pamoja na EPA, uporaji wa nyumba za serikali, mgodi wa Kiwira nk. Nyerere alikaa pale zaidi ya miaka 24 pakiwa hapana fensi lakini paliheshimiwa sana. Walipoingia wezi wakaanza kwanza kuweka fensi ili waweze kufanya maasi yao kadiri watakavyo ili tusiwaone. Ama kweli heshima ya Tanzania ilikwenda na Nyerere. Nyerere alishawahi kusema mke wa kaisari hafai hata kutuhumiwa lakini sasa kaisari mkuu na watoto wake wanatuhumiwa lakini bado wanaongoza nchi. Ajabu ya Firauni!Ufisadi wa dola 250m (zaidi ya 400bn) umetikisa nchi kwa kuikosesha takribani miradi ya sh 3trilion imefahamika. Kampuni ya PAP ilipewa dola 122m (200bn), na kusaini makubaliano kikao cha kunduchi beach hotel oct8.2013 kuwa kiasi kilichobaki (128m au zaidi ya 200bn), PAP watalipwa kila mwezi 8bn mpaka deni kwisha.
Kampuni hii ya PAP iliyopewa tuzo hiyo ya 400bn kwa kuwekeza 6mTsh tu ni ya nan? Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, 50% inililiwa na Singh Sethi(singasinga) na mwanae na asilimia 50% zinamilikiwa na kampuni ya Simba Trust ya Australia.
Simba trust ni nan.? Uchunguzi umeonesha kuwa Simba trust ya Australia inamilikiwa na watu wawili ambao ni salima Kikwete na Miraji Kikwete.
Uwepo wa majina haya mawili kama wamiliki wa PAP inatafsiriwa kuwa ndio sababu kuu ya JK kuvuta miguu huku nchi ikiumia.
Kwa mkataba huu wa IPTL wa 100MW wa miaka 20 (1995_2015), umeongezwa miaka mingine 20 (2013_2033)kwa kuzalisha 500MW.
Kwa mujibu wa mkataba huu, kampuni ya PAP italipwa 400m kila siku kama capacity charges . Maana yake singasinga mwenye 50% atapata 200m kila siku. Na watoto wawili wa JK watapata kila mmoja 100m kila siku hadi 2033.
Uwepo wa familia ya JK kwenye ufisadi huu inadaiwa ndio Kinga ya wahusika ; Muhongo, werema, maswi, mramba, likwilile na hata waziri mkuu kutetea
Ushahidi unakwenda kuonesha kuwa hata uamuzi wa Gavana kuruhusu fedha hiyo itoke kimakosa ni baada ya kupata MEMO kutoka Katibu wa rais Bw Mbena ikisema Rais kaelekeza.
Na ni sababu hiyo pia baada ya Dr Hosea kuwasilisha report kwa rais, JK alisoma na kumjibu achana nayo na ndio maana mpaka sasa report hiyo haijapelekwa kwa DPP ili.wahusika wafikishwe mahakamani
KAMA SEHEMU YA MWANGAZA.
Napenda kuwakumbusha Watanzania, Mataifa ya Ulaya na Marekani huwa hayakurupuki kutoa shutuma, ukiona wanatoa tamko ujue wana uhakika. Walieleza juu ya meli za Iran kutumia bendera ya Tanzania, Membe alikurupuka kukanusha kama kawaida yake, baadaye ikadhihirika ni kweli.
Mataifa ya Ulaya yalitishia kusimamisha misaada kutokana na ufisadi wa Richmond, kwanza serikali ilikanusha baadaye ilidhirika kuwa ni kweli kulikuwa na wizi.
Mataifa ya Ulaya yaliwahi kuelezea ufisadi katika manunuzi ya radar, serikali ikatoa maelezo marefu kuonesha hakuna ufisadi, baadaye ikadhihirika ni kweli.
Sasa wametoa tamko kuwa hakuna msaada kutolewa kwa Tanzania mpaka waone taarifa ya CAG kuhusu ufisadi katika akaunti ya Escrow, serikali imekanusha hakuna ufisadi.
Vyombo vya habari vya Ulaya vimeeleza kuhusu kuhusika kwa serikali ya Tanzania, CCM na China katika biashara haramu ya pembe za ndovu, Membe kama kawaida yake amekurupuka kukanusha lakini mambo hayo yote yatakuja kudhihirika kuwa ni kweli kwa 100%.
Taarifa ya Escrow ipo tayari lakini yaliyomo ndani ni balaa maana ni zaidi hata ya wananchi walivyokuwa wakiitegemea.
Hii iliyopo chini ni kama tetesi lakini ni tetesi yenye uhalisia. Endeleeni kufuatilia kashfa hii kubwa inayogusa ofisi kubwa zote za nchi.
______________________________ ______________________________ ____________
Ikiwa ni siku chache tangu Baraza la Usalama la Taifa kukutana na kupitia ripoti ya uchunguzi ya PCCB kuhusu ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni 200 kwenye akaunti ya Tegeta escrow Benki Kuu, Taarifa za uchunguzi zinaeleza kuwa mkurugenzi wa PCCB Dr. Edward Hosea atamkabidhi Mh. Rais Jakaya Kikwete ripoti hiyo Jumatano ijayo kama ilivyoelekezwa na Baraza la Usalama wa Taifa.
Awali ripoti hiyo ilikuwa akabidhiwe Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lakini taarifa za ndani zinabainisha kuwa uzito wa ripoti hiyo unastahili Mkuu wa nchi mwenyewe kwani kuna maeneo ambayo Waziri Mkuu atastahili kuwajibika.
Ofisi nyingine zilizohusika kwenye ufisadi huu kwa mamlaka yao ni Wizara ya Fedha, Benki Kuu, TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, TRA, na baadhi ya vigogo Ikulu.
RIpoti hiyo imekwenda mbali zaidi kuonesha baadhi ya majina ya watu maarufu waliojipatia fedha hizo kwa namna mbalimbali. Kwa mfano, akaunti ya kampuni ya VIP Engineering katika Benki ya Mkombozi iliyopokea hela za escrow imekutwa hela nyingi zimetoka kwenda kwa Wabunge,Mawaziri Majaji, na baadhi ya watu maarufu (hii ni kwa mujibu wa benki statement ya akaunti hiyo yenye kurasa 27 kuanzia tarehe 20 Januari mpaka tarehe 14 Agosti 2014).
Baadhi ya majina ndani ya benki statement hiyo yalitumiwa pesa kupitia akaunti hiyo ni pamoja na Waziri Anna Tibaijuka, Waziri wa zamani William Ngeleja, Mwanasheria Mkuu wa zamani Andrew Chenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na mmoja wa Majaji wa mahakama kuu ya Tanzania Mujulizi. Katika orodha hiyo kuna Wabunge, wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini, wote isipokuwa mmoja tu ambaye ni mtumishi mwandamizi wa zamani wa Serikali. Viongozi wawili wakuu wa vyama vya siasa vya upinzani nchini wameonekana katika orodha hiyo pia.
Juhudi kubwa zinafanywa hivi sasa kuzuia taarifa ya CAG na PCCB isikabidhiwe Bungeni kwani kama itakuwa wazi inaweza kusababisha kuibuka kwa mtikisiko mkubwa.
Weka ushahidi wa nyaraka, haya maneno matupu hata mie ningeweza kuyatunga na kuyaandika humu JF
Mkuu Mmbabe, nawapenda sana watu wakweli toka ndani ya nafsi zao, na wewe uu mmoja waoi!.Pasco, mbona hili suala liko straightforward kabisa??
sijataja ya Richmond kwa vile kuna mtu aliamua kubeba masalaba kwa niaba ya "chief culprit" (ndiyo maana mimi nadiriki kusema kwa ujasiri kabisa kuwa asipoteuliwa Dr Slaa na chama chake kuwa candidate wa kuingia Magogoni 2015, mr grey head is my alternative default option).
Hii nayo ni list of shame namba 2 Kwenye list of shame namba 1 mkuu wa familia ya rais yumo, hii namba mbili watoto wake wamo. Inatisha. Kweli ikulu ilishabadilishwa kutoka mahali patakatifu mpaka pango la wanyang'anyi. Mimi naona wakati wa utawala wa Ben ndipo maasi makubwa yalifanyika pale ikulu ikuiwa ni pamoja na EPA, uporaji wa nyumba za serikali, mgodi wa Kiwira nk. Nyerere alikaa pale zaidi ya miaka 24 pakiwa hapana fensi lakini paliheshimiwa sana. Walipoingia wezi wakaanza kwanza kuweka fensi ili waweze kufanya maasi yao kadiri watakavyo ili tusiwaone. Ama kweli heshima ya Tanzania ilikwenda na Nyerere. Nyerere alishawahi kusema mke wa kaisari hafai hata kutuhumiwa lakini sasa kaisari mkuu na watoto wake wanatuhumiwa lakini bado wanaongoza nchi. Ajabu ya Firauni!
Ile ya madawa ya kulevya mbona hawajasema kuhusu mashataka waliyoyafungua..??Unapata faida gani kutungia watu uongo? Miraji na Salama fungua mashtaka haraka iwe fundisho kwa watu wa aina hiii
Kuna kila dalili kwamba viongozi wakuu wa vyama vya upinzani waliotajwa katika report ya CAG wanatoka CHADEMA.Hii inatokana. na sintofahamu,taharuki na nia ya dhati kupotosha ukweli,dhihaka kwa watetezi na kuwachafua imejionyesha dhahiri chini ya vibaraka wao mjepo Nguruvi3 Yericko Nyerere IKWETE POMPO.
Bei ya umeme uniti 1= tsh.306.56/-
posho za ewura 1% = tsh. 3.07-
mchango REA 3% = tsh. 9.20/-
VAT 18% maVX = tsh. 55.18/-
tozo kila mwezi = tsh. 5,520/- (unalipa kila mwezi hata kama hujatumia)
JUmla LUKU Bei ya uniti 1 = tsh. 680/-
Kadirio la chini kabisa kwa nyumba ya familia ya watu watano walau wanahitaji uniti 1.5 kwa siku, gharama yake ni tsh.1020/- kwa siku.
Sababu ya gharama za uzalishaji umeme kuwa kubwa;
1.kila kukicha wakurugenzi wa TANESCO wanapiga dili, mfano Mhando.
2.kulipia tsh.5,520/- kila mwezi kwa ajili ya kukamilisha mikataba kama IPTL, Songas, RICHMOND, PAP, Dowans, Symbion
WANANCHI TUTAUTUA MZIGO HUU SIKU TUTAKAPOAMINI BILA CCM INAWEZEKANA, kama tutaendelea na CCM tutapigwa danadana na habari zisizo rasmi TANESCO wanaandaa DODOSO LA KUPANDISHA BEI UMEME. wakipandisha tu posho ya ewura, REA, VAT zote zitapanda kwa sababu upatikana kupitia bei itakayopandishwa na TANESCO. mfano bei ikipanda hadi kufikia 450/- mtumiaji wa umeme utalipia uniti moja kwa tsh. 927 tena hapo tsh.5,520/- ambayo unalipia kila mwezi ibaki kama ilivyo.
bila vurugu za ufisadi bei ya umeme ni tsh. 373/- kwa unit ka elfu kumi kako ungepata uniti 26.8
TUCHAGUE CCM lakini TUTAMBUE NA CHANGAMOTO ZAKE.
Dongo, hoja hapa ni Yeriko kuitaja familia ya JK kuhusika na Escrow. Tumemtaka athibitishe ila mpaka sasa kakimbia mjadala
Pasco, mbona hili suala liko straightforward kabisa??
kwenye level ya executive suala la conflict of interest lipo dhahiri. rais au wanafamilia hawapaswi kufanya biashara ambayo serikali ni mdau au ina maslahi ya moja kwa moja. mtu huhitajiki kuwa gwiji wa sheria kutambua hili.
but nnachojua mimi ni kuwa hili litapita tu kama ilivyopita issue ya Mkapa. kama lilivopita suala la EPA. kama ilivyopita issue ya Mwangosi (mwandishi). kama ya yule dk aliyeng'olewa meno. ne mengine mengi tu. why? kwa vile sisi Watz nikiwemo na mimi na wewe Pasco are simply f....ed!!
sijataja ya Richmond kwa vile kuna mtu aliamua kubeba masalaba kwa niaba ya "chief culprit" (ndiyo maana mimi nadiriki kusema kwa ujasiri kabisa kuwa asipoteuliwa Dr Slaa na chama chake kuwa candidate wa kuingia Magogoni 2015, mr grey head is my alternative default option).
Mkuu Mmbabe, nawapenda sana watu wakweli toka ndani ya nafsi zao, na wewe uu mmoja waoi!.
Pamoja sana!.
Pasco.