Bei ya umeme uniti 1= tsh.306.56/-
posho za ewura 1% = tsh. 3.07-
mchango REA 3% = tsh. 9.20/-
VAT 18% maVX = tsh. 55.18/-
tozo kila mwezi = tsh. 5,520/- (unalipa kila mwezi hata kama hujatumia)
JUmla LUKU Bei ya uniti 1 = tsh. 680/-
Kadirio la chini kabisa kwa nyumba ya familia ya watu watano walau wanahitaji uniti 1.5 kwa siku, gharama yake ni tsh.1020/- kwa siku.
Sababu ya gharama za uzalishaji umeme kuwa kubwa;
1.kila kukicha wakurugenzi wa TANESCO wanapiga dili, mfano Mhando.
2.kulipia tsh.5,520/- kila mwezi kwa ajili ya kukamilisha mikataba kama IPTL, Songas, RICHMOND, PAP, Dowans, Symbion
WANANCHI TUTAUTUA MZIGO HUU SIKU TUTAKAPOAMINI BILA CCM INAWEZEKANA, kama tutaendelea na CCM tutapigwa danadana na habari zisizo rasmi TANESCO wanaandaa DODOSO LA KUPANDISHA BEI UMEME. wakipandisha tu posho ya ewura, REA, VAT zote zitapanda kwa sababu upatikana kupitia bei itakayopandishwa na TANESCO. mfano bei ikipanda hadi kufikia 450/- mtumiaji wa umeme utalipia uniti moja kwa tsh. 927 tena hapo tsh.5,520/- ambayo unalipia kila mwezi ibaki kama ilivyo.
bila vurugu za ufisadi bei ya umeme ni tsh. 373/- kwa unit ka elfu kumi kako ungepata uniti 26.8
TUCHAGUE CCM lakini TUTAMBUE NA CHANGAMOTO ZAKE.
Ikumbukwe kwamba uhamishaji wa asilimia 70 ya hisa
za IPTL kwenda PAP umeambatana na nyaraka za
kughushi kutokana na kutokuwepo kabisa kwa
uthibitisho wa cheti halisi cha hisa (share certificate)
kutoka kampuni ya Mechmar kwenda kampuni ya
Piperlink. Nyaraka za TRA zinaonyesha kwamba hisa
hizo (70%) ziliuzwa kwa Shilingi za Kitanzania milioni
sita (6) tu. Na bado hakuna ushahidi kuonyesha
kwamba uhamishaji huo wa hisa ulipata baraka za
mamlaka husika kama inavyotakiwa na sheria za nchi.
Wakati huyo anayejiita mmiliki mpya wa IPTL aliposaini
mkataba wa kuchukua fedha kutoka akaunti ya Escrow
zilizokuwapo BoT, hakuwa mmiliki halali kisheria kwani
kodi ililipwa siku moja baada ya wao kupokea fedha
kutoka BoT. Sheria inataka kutolewa kwa cheti na
Kamishna wa TRA kama uthibitisho kwamba kodi yote
imelipwa ipasavyo (Sheria ya Fedha ya 2012 kifungu
cha 29).
Ni nani wamiliki wengine wa kampuni ya PAP?
Uchunguzi ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa
wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara
ya Nishati na Madini.
Inapaswa tutafakari kuona kwamba Harbinder Singh
aliyechukua fedha za Escrow, anamiliki vitalu vya
mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo HydroTanz
ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na
anwani sawa na ya kampuni ya Simba Trust. Kitalu
hicho cha mafuta kinaitwa Mnazi Bay North, jirani
kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani
Mtwara.