DOKEZO Familia ya Rais Kikwete yahusika ufisadi wa ESCROW

DOKEZO Familia ya Rais Kikwete yahusika ufisadi wa ESCROW

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ufisadi wa dola 250m (zaidi ya 400bn) umetikisa nchi kwa kuikosesha takribani miradi ya sh 3trilion imefahamika. Kampuni ya PAP ilipewa dola 122m (200bn), na kusaini makubaliano kikao cha kunduchi beach hotel oct8.2013 kuwa kiasi kilichobaki (128m au zaidi ya 200bn), PAP watalipwa kila mwezi 8bn mpaka deni kwisha.

Kampuni hii ya PAP iliyopewa tuzo hiyo ya 400bn kwa kuwekeza 6mTsh tu ni ya nan? Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, 50% inililiwa na Singh Sethi(singasinga) na mwanae na asilimia 50% zinamilikiwa na kampuni ya Simba Trust ya Australia.

Simba trust ni nan.? Uchunguzi umeonesha kuwa Simba trust ya Australia inamilikiwa na watu wawili ambao ni salima Kikwete na Miraji Kikwete.

Uwepo wa majina haya mawili kama wamiliki wa PAP inatafsiriwa kuwa ndio sababu kuu ya JK kuvuta miguu huku nchi ikiumia.

Kwa mkataba huu wa IPTL wa 100MW wa miaka 20 (1995_2015), umeongezwa miaka mingine 20 (2013_2033)kwa kuzalisha 500MW.

Kwa mujibu wa mkataba huu, kampuni ya PAP italipwa 400m kila siku kama capacity charges . Maana yake singasinga mwenye 50% atapata 200m kila siku. Na watoto wawili wa JK watapata kila mmoja 100m kila siku hadi 2033.

Uwepo wa familia ya JK kwenye ufisadi huu inadaiwa ndio Kinga ya wahusika ; Muhongo, werema, maswi, mramba, likwilile na hata waziri mkuu kutetea

Ushahidi unakwenda kuonesha kuwa hata uamuzi wa Gavana kuruhusu fedha hiyo itoke kimakosa ni baada ya kupata MEMO kutoka Katibu wa rais Bw Mbena ikisema Rais kaelekeza.

Na ni sababu hiyo pia baada ya Dr Hosea kuwasilisha report kwa rais, JK alisoma na kumjibu achana nayo na ndio maana mpaka sasa report hiyo haijapelekwa kwa DPP ili.wahusika wafikishwe mahakamani


KAMA SEHEMU YA MWANGAZA.

Napenda kuwakumbusha Watanzania, Mataifa ya Ulaya na Marekani huwa hayakurupuki kutoa shutuma, ukiona wanatoa tamko ujue wana uhakika. Walieleza juu ya meli za Iran kutumia bendera ya Tanzania, Membe alikurupuka kukanusha kama kawaida yake, baadaye ikadhihirika ni kweli.
Mataifa ya Ulaya yalitishia kusimamisha misaada kutokana na ufisadi wa Richmond, kwanza serikali ilikanusha baadaye ilidhirika kuwa ni kweli kulikuwa na wizi.

Mataifa ya Ulaya yaliwahi kuelezea ufisadi katika manunuzi ya radar, serikali ikatoa maelezo marefu kuonesha hakuna ufisadi, baadaye ikadhihirika ni kweli.

Sasa wametoa tamko kuwa hakuna msaada kutolewa kwa Tanzania mpaka waone taarifa ya CAG kuhusu ufisadi katika akaunti ya Escrow, serikali imekanusha hakuna ufisadi.

Vyombo vya habari vya Ulaya vimeeleza kuhusu kuhusika kwa serikali ya Tanzania, CCM na China katika biashara haramu ya pembe za ndovu, Membe kama kawaida yake amekurupuka kukanusha lakini mambo hayo yote yatakuja kudhihirika kuwa ni kweli kwa 100%.

Taarifa ya Escrow ipo tayari lakini yaliyomo ndani ni balaa maana ni zaidi hata ya wananchi walivyokuwa wakiitegemea.

Hii iliyopo chini ni kama tetesi lakini ni tetesi yenye uhalisia. Endeleeni kufuatilia kashfa hii kubwa inayogusa ofisi kubwa zote za nchi.
______________________________ ______________________________ ____________

Ikiwa ni siku chache tangu Baraza la Usalama la Taifa kukutana na kupitia ripoti ya uchunguzi ya PCCB kuhusu ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni 200 kwenye akaunti ya Tegeta escrow Benki Kuu, Taarifa za uchunguzi zinaeleza kuwa mkurugenzi wa PCCB Dr. Edward Hosea atamkabidhi Mh. Rais Jakaya Kikwete ripoti hiyo Jumatano ijayo kama ilivyoelekezwa na Baraza la Usalama wa Taifa.

Awali ripoti hiyo ilikuwa akabidhiwe Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lakini taarifa za ndani zinabainisha kuwa uzito wa ripoti hiyo unastahili Mkuu wa nchi mwenyewe kwani kuna maeneo ambayo Waziri Mkuu atastahili kuwajibika.

Ofisi nyingine zilizohusika kwenye ufisadi huu kwa mamlaka yao ni Wizara ya Fedha, Benki Kuu, TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, TRA, na baadhi ya vigogo Ikulu.

RIpoti hiyo imekwenda mbali zaidi kuonesha baadhi ya majina ya watu maarufu waliojipatia fedha hizo kwa namna mbalimbali. Kwa mfano, akaunti ya kampuni ya VIP Engineering katika Benki ya Mkombozi iliyopokea hela za escrow imekutwa hela nyingi zimetoka kwenda kwa Wabunge,Mawaziri Majaji, na baadhi ya watu maarufu (hii ni kwa mujibu wa benki statement ya akaunti hiyo yenye kurasa 27 kuanzia tarehe 20 Januari mpaka tarehe 14 Agosti 2014).

Baadhi ya majina ndani ya benki statement hiyo yalitumiwa pesa kupitia akaunti hiyo ni pamoja na Waziri Anna Tibaijuka, Waziri wa zamani William Ngeleja, Mwanasheria Mkuu wa zamani Andrew Chenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na mmoja wa Majaji wa mahakama kuu ya Tanzania Mujulizi. Katika orodha hiyo kuna Wabunge, wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini, wote isipokuwa mmoja tu ambaye ni mtumishi mwandamizi wa zamani wa Serikali. Viongozi wawili wakuu wa vyama vya siasa vya upinzani nchini wameonekana katika orodha hiyo pia.
Juhudi kubwa zinafanywa hivi sasa kuzuia taarifa ya CAG na PCCB isikabidhiwe Bungeni kwani kama itakuwa wazi inaweza kusababisha kuibuka kwa mtikisiko mkubwa.

Mmmh! Hii kashfa ni kubwa,kweli Tembo wakubwa lazma wadondoke!
 
ahsante Mkuu Pasco. Nina hakika Yeriko hataingia tena kwenye uzi huu japo anachungulia kwa mbali kusoma comments za watu. Nipo naye karibu na namuona anavyohangaika

Unafki tu huna lolote
 
Nakwambia kwa namna walivyomtenda Lowassa,hapa hatapaachia,lazima afe na wabaya wake.
 
Hii nchi ni ya kishkaj.. leo mtu anapata skendo na kesho anakuwa mtu muhimu kwetu..hizi kesi wanaziweza China na Uarabuni maana hatoki mtu huko ila hapa mwakani washukiwa wote watapeta tu.
 
hahahahahahahaaaaaa! Mwambie Dr Slaa aache uzinifu na badala yake aoe ili aishi maisha ya Ndoa. Kama dini ni kikwazo, anaweza kubadili ili apate haki yake ya kuishi maisha halali ya ndoa. Ndoa tamu jamani. Uzinifu haufai. Ni laana kwa Mungu na huondoa baraka ya maisha. Mambo mengine Dr Slaa anajitakia mwenyewe, pengine angeoa mpaka sasa angekuwa Presidaa wetu

Ys a shame chama unachoshabikia kinaongoza serikali but hujui kwamba kuishi ka kwanamke miezi sita tu kiserikali inatambulika kama ndoa halali sijui unahitaj nn cha zaid kwa slaa
 
Ikiwa habari hii ni ya kweli basi tunapaswa kuamini hata hapo kwenye red. Kutokana na hilo ndio maana wenye akili zao na wasiopenda kubeba mikoba ya wanasiasa wanaamini kwamba CCM, CHADEMA, CUF, NCCR n.k wote ni wezi tu na mafisadi wakubwa.


John Cheyo,A.Mrema na Dovutwa nao niwapinzani?
 
Ukisikia mtoto wa raisi ni tajiri ni kawa hivi! Japo wao watasema wana mashamba ya matikiti msoga..tehe tehe wenye akili wanajua.
 
hahahahahahahaaaaaa! Mwambie Dr Slaa aache uzinifu na badala yake aoe ili aishi maisha ya Ndoa. Kama dini ni kikwazo, anaweza kubadili ili apate haki yake ya kuishi maisha halali ya ndoa. Ndoa tamu jamani. Uzinifu haufai. Ni laana kwa Mungu na huondoa baraka ya maisha. Mambo mengine Dr Slaa anajitakia mwenyewe, pengine angeoa mpaka sasa angekuwa Presidaa wetu

Dr slaa akioa au asipooa inatusaidia nn kama taifa?
 
dada yangu, haya umeandika ukiwa umelalia kifuani mwa mwanaume? Lo! Hadi unatia huruma dada. Kazi zingine waachie wanaume. Wewe huziwezi

Sa gender discrimination za nn sasa si ujibu hoja no mata amelala kwa mwanaume au kwa mwanamke mwenzie
By the way t shows how much una boga kichwani kama mzee wa msoga tu
 
we unajua hata unachozungumzia?? this contradiction proves that "its a made up story"

Kwa nini unauliza swali ambalo ndo msingi wa thread yako?? Sipendi uongozi wa JK, lakini sipendi zaidi wazushi kama wewe sababu mnatumika ku divert attention ya watu kutoka katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo kwa kutaka kuwaaminisha majibu yasiyo na msingi.

Ungetusaidia zaidi kama ungeweka walau nyaraka yeyote katika hili, lakini kwa porojo hii unayotumia inaonyesha hujui kitu na umeweka bandiko hili kutumia hayo majina ili wanaojua waje wakupe taarifa ya nani muhusika wa hizo 50%
Ungeweza tu kuuliza moja kwa moja na ungepata majibu, kuliko kuja na majina alafu baadaye unasahau kuwa ushaweka majina na unauliza tena eti majina ya wamiliki ni kina nani?? Ridiculous , poor Yericko Nyerere

Mkuu mbona umepanic Sana??? Vipi na wewe ni familia ile ile nini?
 
Last edited by a moderator:
mkuu tusipoamua kufanya maamuzi wenyewe tutaendelea kumsubiri sana huyo mungu kiziwi, kwanza kwanini atuletee Rais kiazi namna hii?

Mkuu chunga ulimi wako, unamkufuru Mungu.
Wakati mwingine Mungu huwa anaruhusu mabaya yatupate kwa ajili ya kutupatia Neema zake huko mbeleni. Unakumbuka wana wa Israel utumwani Misri, jangwani hadi walipofikia nchi ya ahadi Canaan ya maziwa na asali walipitia magumu gani? Only if you ara a Christian.
 
Aiseee kumbe wanaofanyaga mapinduzi huwa wanakuwa wameteswa na wameumia sana yaani yamewafika hadi wanaamua kumpiga Risasi Rais wao huwa wamechoshwa. Yaani sisi bado hatujachoka kabisa tena wanaiba pesa ndogo sana hizo bado hatujachoka ila utakuja kufika wakati sijui ni hiki kizazi au baadaye kitakapo choka watu watatoka hata kwa mtutu
 
Ukiona mtu anaanzisha mada, then anapoulizwa maswali anashindwa kujitokeza na anaedit mara kwa mara taarifa yake na anaongeza maneno kwa kadri mjadala unavyoenda basi ujue hana hakika na alichokiandika. yeriko Nyerere unatia aibu. Kajipange upya
 
Back
Top Bottom