Familia ya Sauli yaeleza miradi watakavyoisimamia, watoto watakavyoishi

Familia ya Sauli yaeleza miradi watakavyoisimamia, watoto watakavyoishi

Aisee vijana ukiwa unajitafutaa hata kama maisha magumu vip Ebi hakikisha unapata mtoto mapema sanaa yani usivuke 30 huna mtotoo..! Mwana kafariki ila watoto wadogoo mnoo yani yatima 4 sio mchezoo na kumantain maisha aliyowaachia Baba yao ni ndoto kiukweli watoto wanaweza kupitia Msotoo mkali sana..! Apumzike kwa amani sauli.
Mungu hakupi vyote ndugu.....Tajiri na mali Maskini na wana
 
Mtoto alipona duu...
Watoto ni malaika wengi huwa wanapona
Nonsense.Hoja yako ingekuwa na mashiko kama watoto wote wangekuwa hawafi kwenye ajali.Usisahau kuna watu wazima wengi tu wanaopona kwenye ajali mbaya sana kama JAL 123
 
Nonsense.Hoja yako ingekuwa na mashiko kama watoto wote wangekuwa hawafi kwenye ajali.Usisahau kuna watu wazima wengi tu wanaopona kwenye ajali mbaya sana kama JAL 123
Kunywa maji naona umepanick kwa hoja ambayo hukuona generalization...labda ni wapi nimeandika "watoto wote huwa wanapona???
Nonsense......
 
Kunywa maji naona umepanick kwa hoja ambayo hukuona generalization...labda ni wapi nimeandika "watoto wote huwa wanapona???
Nonsense......
Unaona ulivyo KIAZI, umesema watoto ni Malaika ndio maana wengi huwa wanapona kwenye ajali. Nimekwambia hoja yako ni ya KIPUUZI sababu kupona kwenye ajali ni bahati tu haijalishi ni mtoto au mtu mzima.
Watoto sio Malaika,acha UPUMBAVU.
 
Kwa hiki ulichoandika unathibitisha kwamba nilikuwa sahihi kukuita KIAZI na MPUMBAVU.
Come on, I'm just getting started.
Kimekuramba...siku hizi sibishani na wanaume wenye midomo mirefu kama wanakalia moto....napoteza muda tuu
Hapa mm na ww nadhani umeonekana ww ndo juha..mpumbavu kiazi na huna adabu...
Yani umekuta comment ya mtu..hujapendezwa nayo unakuja na kumtukana uko salama kweli?
Hiyo title ya Sir toa hapo ww ni jr...Sir hawezi kuropokwa na matusi juu kisa kaona comment ambayo haijampendeza...
Nimemaliza ukiendelea...basi unakalia moto kweli....
Watoto ni malaika Andamana....
 
Kimekuramba...siku hizi sibishani na wanaume wenye midomo mirefu kama wanakalia moto....napoteza muda tuu
Hapa mm na ww nadhani umeonekana ww ndo juha..mpumbavu kiazi na huna adabu...
Yani umekuta comment ya mtu..hujapendezwa nayo unakuja na kumtukana uko salama kweli?
Hiyo title ya Sir toa hapo ww ni jr...Sir hawezi kuropokwa na matusi juu kisa kaona comment ambayo haijampendeza...
Nimemaliza ukiendelea...basi unakalia moto kweli....
Watoto ni malaika Andamana....
Nafurahi unavyozidi kuthibitisha kuwa wewe ni KIAZI na MPUMBAVU kama nilivyosema hapo awali.
Nipo hapa mpaka ukimbie.
 
aisee, ushauri kwa familia, biashara ya mabus kama hakuna aliyeachiwa njia na namna yakuyaendesha wayauze aisee hela zifanye mambo mengine, hiyo biashara inataka adabu ya Hali ya juu, nazungumzia jambo ninalolifahamu.

Kwenye migodi nako ni yaleyale tu, unahitaji descipline kuendesha mashimo hasa kama bado njia haijafikiwa, ila kama wapo kwenye mwamba mali inatoka wawe na adabu pia ya matumizi maana njia chini huwa zinakata pia, wanaweza kuleta kizaazaa kwenye familia, nazungumzia jambo ninalolifahamu pia.

All in all, nawatakia kheri familia kwenye uendeshaji na usimamizi wa mali mwamba, zinufaishe familia, ndugu na jamaa kama ambavyo mwenyewe alivyokuwa hai.
Apumzike Kwa amani bwana Sauli na tunamuombea kwa mwenyezi Mungu amfanyie wepesi kwenye safari yake ya mpya ya maisha.
 
Familia ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomon Mwalabhila imesema kumpoteza mpendwa wao huenda baadhi ya miradi ikayumba hususan ya mabasi huku ikisisitiza imejipanga kusimamia vyema migodi ya dhahabu ili kuwasaidia watoto wake.

Mwalabhila maarufu kwa jina la Sauli, alifariki dunia Agosti 4, 2024 kwa ajali ya gari maeneo ya Mlandizi Mkoa wa Pwani na mwili wake ulisafirishwa jana Jumanne kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) hadi Songwe, Mkoa wa Mbeya.

Baada ya kuwasili, mwili huo ulisafirishwa kwenda wilayani Chunya mkoani humo kwa mazishi yanayotarajia kufanyika leo Jumatano,Agosti 7, 2024 nyumbani kwao Kijiji cha Godima huku msiba ukiwa nyumbani kwake Kibaoni.

Asubuhi ya leo Jumatano, Mwananchi imezungumza na Osward Mwasenge ambaye ni binamu wa marehemu anayesimamia machimbo ya madini, akisema yapo maeneo walimtegemea zaidi Sauli, hivyo ipo hofu ya baadhi ya miradi kuyumba.

Amesema sehemu ya mabasi walimtegemea yeye, lakini upande wa migodi watatumia njia alizokuwa akipita kuweza kuziendeleza kwa manufaa ya watoto wake takribani 10.

"Watoto wake bado wanahitaji msaada kwakuwa wakubwa wawili Octavian na Gravian Sauli ndio wamemaliza kidato cha nne na wengine bado wadogo, ni pigo kubwa kwa kuwa kuna miradi alitegemewa yeye hasa upande wa magari," amesema Mwasenge.

"Kwa upande wa migodi ninaposimamia mimi kwa miaka 10 sasa, sitarajii itetereke kwa kuwa alishatupa njia na tutatumia uzoefu kuweza kulinda rasilimali hii na kila kitu kitakuwa wazi kwa ustawi wa familia."

Mwasenge amesema: “Mabasi ya biashara yalikuwa manne japokuwa yalisimama kutoa huduma hivi karibuni ila alikuwa akishughulikia yarejee, mengine manne yalikuwa ya kutembelea ila moja ndilo limeharibika baada ya ajali, hivyo jumla yanabaki saba," amesema Mwasenge.

Binamu huyo ameongeza enzi za uhai wa Sauli, alipenda na kuwaamini sana ndugu zake ndio maana miradi yote aliikabidhi katika ukoo, hivyo kifo chake kimekuwa pigo na simanzi kubwa.

"Alikuwa mpenzi sana na watoto wake, ndio maana hata kwenye ajali alikuwa na mwanaye mdogo ambaye alijeruhiwa kidogo, tutakaa kikao kuamua nani aweze kuwa msimamizi mkuu wa familia na mali kwa jumla," amesema Mwasenge.

Chanzo: Mwananchi

Pia Soma
- TANZIA - Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomoni Mwalabhila afariki dunia
Hakuna.kitu.
 
AAcha ujinga watu wenye vipato kama sauli huku kusini ni wengi , shida ni kuwa hawafanyi biashara ya gari za abiria hiv kiwafahamh ngumu
Acha ujinga huwa anasemwa mtu anayejulikana kama hujulikani hata mtaani wewe maskini, utajiri ni umaarufu.
 
Back
Top Bottom