Familia zetu za Kiafrika zina matatizo gani, kwanini zina ubinafsi sana?

Familia zetu za Kiafrika zina matatizo gani, kwanini zina ubinafsi sana?

Familia zetu, kila mmoja anatakiwa aanzie mwanzo.

Yaani hakuna mwendelezo wa maisha ya uchumi na biashara.

Eti wanakwambia kila mmoja ajipambanie...

Kama kuna mali wazee waliacha basi watu watataka ziuzwe kila mtu afe na chake, ili wajukuu nao wakianza maisha waanze kuteseka upyaaaa[emoji2][emoji2][emoji2] ukoo wote unakuwa ni wa vizazi vya wapambanaji miaka nenda rudi na hawajui wanapambania nini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]

Ndio maana kutoboa inakuwa ni ngumu sana.

Wakisha kusomesha ukapata ka degree basi ukajitegemee.

Unaanza maisha from scratch kabisa bila msaada , ila ukifanikiwa kdg tu ukoo mzima unahamia kwako.

Na hii ndo inasababisha life span ya waafrika kuwa ndogo, ushirikina,chuki, utengano wa familia, yaani full heka heka. Hii kitu imefanya familia nyingi za kiafrika kuendelea kuishi Maisha ya kimaskini.

Vita ya Umaskini inahitaji kurithishwa silaha ulizotumia kupambana hakikisha unakiachia kizazi chako ili kianzie ulipo ishia.

Tujifunze kwa Familia za kiarabu

Hii ni changamoto sana, ndo maana biashara nyingi zilizoanzishwa na wazazi zinakufa hivi hivi in the name of “ usitegemee utarithi hii biashara/duka, kajipambanie”
Mbona hi hali iko kwote kwote kuna exemption kwa familia chache tu, ata India, Arabia Europe hiyo hali ya individual struggle ipo sanaa, tembeeni na uishi hata mwaka moja hi hali utajionea, neenda Europe utasikia wanasema "mind your own bussiness" watoto wengi huachiwa serikali, India 80% katika cast system yao ni masikini sanaa,
 
Angalia wahindi wanavoendeleza Mali za wazazi wao ila bongo ukiendeleza unaambiwa tafuta chako usitegemee cha urisi sasa sijui wanataka majini ndo warisi ndomana majumba meng uswailini ya urisi wanagawana room alafu hawafanyi marekebsho wakizani watachekwa et cha urisi ....... CHA URISI KITAMU ASIKWAMBIE MTU
 
Kuna mzee kafariki kaacha fremu 2 na coaster za daladala 3. Msiba wake ni ngumi mwanzo mwisho. Amezikwa ni ngumi mwanzo mwisho. Vita ipo kati ya watoto wa mke wa kwanza na watoto wa Mke wa pili. Ni vita kweli kweli 🤣🤣

Hapo hakuna muendelezo ni vita tu 🤣
 
Back
Top Bottom