Fanya hivi ukikutana na wanyama hawa porini

Fanya hivi ukikutana na wanyama hawa porini

Inategemeana na nyumba utakayokimbilia,ila kwa mazingira ya kijijini nyumba nyingi ni tope na zimeezekwa kwa nyasi hapo nakushauri usikimbilie humo. mwaka 2016 nilikuwa na kiredio changu uck nilikuwa nakiwasha non stop,kumbe bhana tembo wanapita nje,mmoja mkubwa wao akajaribu kutikisa kiberiti nikakizima kiredio nikaingia uvunguni na mkojo ukifuatia. kijiji chetu kwa miaka mingi kimekuwa kilikumbana na masahibu ya tembo kila mwaka wanavamia na kula mazao ya wakulima mana kijiji chetu kina poli la akiba. ila tunashukru serikali kwa kuingia ubia na kampuni ya allience one kufanya project ya upandaji wa miti, sasa hali ni shwari.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hahaha hatari mkuu, hata kijijini ziliwahi kupita zikabomoa nyumba bahati nzuri hakuwemo mtu, kuingia ndani ya nyumba inabidi usome uelekeo wa tembo na mood yake kama ana hasira au anapita tu
 
kwa hiyo kwa faru au nyati nianze kuswali swala yamwisho? kwamba wao hawana mbinu? sasa umewaweka iweje kwenye list? nawaza nakutana na simba face toface lazima aniue mana sjajua kama ntageuka usain bolt au nife kwa kihoro
Faru na Nyati ukiwaona, uamuzi wa haraka nikuondoka chap na mazingira kama yanafaa kimbia...
Ukikimbia kwenda mbali na wao mara nyingi hawakukimbizi
Kukwea mti pia kwaweza kuwa kwa msaada japo mara nyingi hawa hukaa kwenye vichaka na majani marefu (bila kuwepo miti mikubwa).

Muhimu; mara zote ukitembea maeneo ya wanyama kama Mamba & chatu usisau kubeka kisu kidogo.
Mamba: ukimchoma kichwani kwa kisu anakuachia na hasa ukiweza kulenga macho anakuachia mara moja; Lakini pia akikushika akawa anajizungusha, zunguka naye, ukijizuia utavunjika na ndivyo anataka.

Chatu; ukiweza kumkata kata na ukibahatisha mdomo wake ukaukata/chana anakuachia. Kumbuka Chatu hana meno hivyo nguvu yake ipo kwenye kukuvinga hivyo jitahidi kumtoa asikuviringe
Mara nyingi chatu hupendelea watoto; Mtu mzima aliyesimama huonekana mkubwa sana kwake....
 
Faru na Nyati ukiwaona, uamuzi wa haraka nikuondoka chap na mazingira kama yanafaa kimbia...
Ukikimbia kwenda mbali na wao mara nyingi hawakukimbizi
Kukwea mti pia kwaweza kuwa kwa msaada japo mara nyingi hawa hukaa kwenye vichaka na majani marefu (bila kuwepo miti mikubwa).

Muhimu; mara zote ukitembea maeneo ya wanyama kama Mamba & chatu usisau kubeka kisu kidogo.
Mamba: ukimchoma kichwani kwa kisu anakuachia na hasa ukiweza kulenga macho anakuachia mara moja; Lakini pia akikushika akawa anajizungusha, zunguka naye, ukijizuia utavunjika na ndivyo anataka.

Chatu; ukiweza kumkata kata na ukibahatisha mdomo wake ukaukata/chana anakuachia. Kumbuka Chatu hana meno.
this only applicable in movies, kiuhalisia kitendo cha kudakwa na chatu au mamba mimi ni mfu tayar hao faru itategemea na distance tutakayokutana nna uhakika miguu yangu haitonikwamisha
 
Ikitokea umebananishwa na umekutana na mojawapo wa wanyama hawa wakali Fanya haya kujiokoa

1 Simba
Huyu ni mnyama mkali sana
Ukikutana na Simba porini panda mti, au jiamini mtizame na uanze kumfukuza
Simba anaogopa ujasiri wa kiumbe yeyote atakimbia

2. Chui
Chui huishi mafichoni, chui hukaa peke yake
Ukikutana na chui, jifanye hujamwona.
Chui ni dhaifu, usimchokoze maana anaweza kukubadilikia

3. Tembo
Huyu ni mpole, ila ukikuta amevurugwa labda amepoteza ndama ujue safari yako imeishia hapo atakuua akukanyage uwe kama chapati
Ukikutana nae kamba Kuna mlima kimbia kama unateremka, au ingia shimoni au ndani kama Kuna nyumba

Usije ukapanda mti ukimwona tembo

4.Nyati/ Faru
Ukikutana na wanyama hawa una asilimia 80 za kuwa marehemu,
Hawa Bora ukitane na Simba
Vyote omba ila usikutane na hawa viumbe porinii dadeki

5 Chatu
Kama unaenda porini na unahisi Kuna Chatu penda kutembea na mbwa, Atamkamata mbwa we ukimbie, maana na Chatu na mbwa wana uadui wao

6 Fisi
Hawa huvizia usiku na huogopa mwanga, we tembea na tochi
Au akikuvuzia kamata mkia

6. Nyoka
Hawa wapo wa aina tofauti na kila nyoka ana tabia zake
Kuna wanaovizia, wanaoshambuliwa, wanaosubiri uwakanyage n. K
Kikubwa ukipata ajali ya nyoka kunywa mkojo wako

7 Mamba
Hawa hukaa ukingoni mwa moto au ziwa
Ukienda maeneo hayo ukakuta utulivu usio wa kawaida usijaribu kuingia majini
Kujiokoa mdomoni mwa mamba ni ngumu
Ila jaribu tu kumbinya tumbo

8 Mbwa mwitu
Hawa hutembea kundi kubwa unakuta wapo zaidi ya 50
Hawa ukiwaona panda mti
Haya kuyasema ni rahisi lkn kwa ground ni ngumu mno, si rahisi ukawa na ujasiri wa kumtazama simba,na kuna baadhi ya miti simba anapanda

Labda atleast tembo kwa kukimbia mlimani,lkn mambo mengine yote hayatekelezeki
 
Hao Namba nane nilikutana nao week 2 zilizopita nilijidai kama siwaon vile nao wakakaa kimya. Walikuwa zaidi ya watano
 
Faida kama
(a) Chakula
(b) Nyoka ni kivutio cha utalii, hivyo hulipatia taifa fedha za kigeni
(c) Nyoka hutumika kama mlizi shambani zidi ya wadudu wanaokula mazao,
Mfano: panya hushambulia sana mashamba ya karanga, ikitokea shamba lako limevamiwa na panya, mwaga nyoka mkuu shamba nzima mkuu na (d) dawa ya mtu aliegongwa na nyoka anayo nyoka mwenyewe, na ndiomaana ukigongwa na nyoka ukaenda hospital, swali la kwanza la Dr. anataka kujua ni Haina gani ya nyoka aliekugonga.

Hizo ni chache tu kati nyingi.
 
Mbinu nyingine ni vichekesho. Nimeona humu mtu anasema "ukikutana na Simba mkimbilie, ataogopa na yeye atakimbia".
 
𝚆𝚎 𝚓𝚊𝚖𝚊𝚊 𝚑𝚞𝚞 𝚗𝚒 𝚞𝚣𝚒 𝚝𝚞 𝚞𝚖𝚎𝚕𝚎𝚝𝚊 𝚠𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚊𝚌𝚑𝚊𝚗𝚐𝚒𝚎 𝚒𝚕𝚊 𝚔𝚒𝚞𝚑𝚊𝚕𝚒𝚜𝚒𝚊 𝚞𝚔𝚒𝚔𝚞𝚝𝚊𝚗𝚊 𝚗𝚊 𝚒𝚣𝚘 𝚖𝚋𝚊𝚗𝚐𝚊 𝚖𝚑𝚑𝚑 𝚑𝚊𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚔𝚒𝚝𝚞 𝚌𝚑𝚊 𝚣𝚒𝚊𝚍𝚊 𝚣𝚊𝚒𝚍𝚒 𝚢𝚊 𝚞𝚋𝚘𝚗𝚐𝚘 𝚞𝚝𝚊𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚒𝚊, 𝚖𝚣𝚎𝚎 𝚝𝚘𝚔𝚊 𝚗𝚍𝚞𝚔𝚒 𝚜𝚑𝚠𝚊𝚊𝚊𝚊𝚊𝚊 𝚝𝚊𝚏𝚞𝚝𝚊 𝚏𝚒𝚌𝚑𝚘 𝚌𝚑𝚊𝚙
 
𝚆𝚎 𝚓𝚊𝚖𝚊𝚊 𝚑𝚞𝚞 𝚗𝚒 𝚞𝚣𝚒 𝚝𝚞 𝚞𝚖𝚎𝚕𝚎𝚝𝚊 𝚠𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚊𝚌𝚑𝚊𝚗𝚐𝚒𝚎 𝚒𝚕𝚊 𝚔𝚒𝚞𝚑𝚊𝚕𝚒𝚜𝚒𝚊 𝚞𝚔𝚒𝚔𝚞𝚝𝚊𝚗𝚊 𝚗𝚊 𝚒𝚣𝚘 𝚖𝚋𝚊𝚗𝚐𝚊 𝚖𝚑𝚑𝚑 𝚑𝚊𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚔𝚒𝚝𝚞 𝚌𝚑𝚊 𝚣𝚒𝚊𝚍𝚊 𝚣𝚊𝚒𝚍𝚒 𝚢𝚊 𝚞𝚋𝚘𝚗𝚐𝚘 𝚞𝚝𝚊𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚒𝚊, 𝚖𝚣𝚎𝚎 𝚝𝚘𝚔𝚊 𝚗𝚍𝚞𝚔𝚒 𝚜𝚑𝚠𝚊𝚊𝚊𝚊𝚊𝚊 𝚝𝚊𝚏𝚞𝚝𝚊 𝚏𝚒𝚌𝚑𝚘 𝚌𝚑𝚊𝚙
Utamzidi kazi nyati, Simba, chui
 
Ukikutana na simba vua nguo zote halafu mbong'olee yaani geuka nyuma inama kisha aone matako yako, simba ataogopa kwa maana hayo matako atahisi kama ni vichwa viwili hivyo atasitaajabu na kukimbia kwakuwa hajawahi kuona.mnyama mwenye vichwa viwili.
Kwa Stahili hiyo utapigwa miti mzee yaani unamuelekezea kunduchi bila aibu asee
 
Back
Top Bottom