Fanya hivi ukikutana na wanyama hawa porini

Fanya hivi ukikutana na wanyama hawa porini

Kwenye tembo tembea na filimbi hawapendi kelele so ukipiga filimbi anakimbia na wewe kabisa ila kuna tembo wakorofi sana hawa ni wale walio tengwa na familia zao

Nyati akiwa mmoja huna ujanja sanasana hapo ukikimbia lala chini uwe una kroo au kuloli kwa walio pitia jeshi wanaelewa ila wakiwa wengi huwa wao ndio wanakimbia
Umenipa maarifa mapya
 
Kama unapita kwenye mapori au msitu wenye simba cha kufanya we beba Mua tu. Hakuna simba atakayekusogelea.

Unataka kujua sababu? Nitakuambia post inayofuata.
 
ukikutana na Faru kimbia alafu uwe unavua nguo moja baada ya nyingine, yeye atabaki kulirarua shat ulilovua, muda huo wewe umeshafika mbali
Hata kwa cobra au koboko,kimbia achilia nguo juu ya kitawi chochote,atakipiga meno haswa

Faru yeye ukiwasha moto,atataka auzime kwanza.
 
Ikitokea umebananishwa na umekutana na mojawapo wa wanyama hawa wakali Fanya haya kujiokoa

1 Simba
Huyu ni mnyama mkali sana
Ukikutana na Simba porini panda mti, au jiamini mtizame na uanze kumfukuza
Simba anaogopa ujasiri wa kiumbe yeyote atakimbia

2. Chui
Chui huishi mafichoni, chui hukaa peke yake
Ukikutana na chui, jifanye hujamwona.
Chui ni dhaifu, usimchokoze maana anaweza kukubadilikia

3. Tembo
Huyu ni mpole, ila ukikuta amevurugwa labda amepoteza ndama ujue safari yako imeishia hapo atakuua akukanyage uwe kama chapati
Ukikutana nae kamba Kuna mlima kimbia kama unateremka, au ingia shimoni au ndani kama Kuna nyumba

Usije ukapanda mti ukimwona tembo

4.Nyati/ Faru
Ukikutana na wanyama hawa una asilimia 80 za kuwa marehemu,
Hawa Bora ukitane na Simba
Vyote omba ila usikutane na hawa viumbe porinii dadeki

5 Chatu
Kama unaenda porini na unahisi Kuna Chatu penda kutembea na mbwa, Atamkamata mbwa we ukimbie, maana na Chatu na mbwa wana uadui wao

6 Fisi
Hawa huvizia usiku na huogopa mwanga, we tembea na tochi
Au akikuvuzia kamata mkia

6. Nyoka
Hawa wapo wa aina tofauti na kila nyoka ana tabia zake
Kuna wanaovizia, wanaoshambuliwa, wanaosubiri uwakanyage n. K
Kikubwa ukipata ajali ya nyoka kunywa mkojo wako

7 Mamba
Hawa hukaa ukingoni mwa moto au ziwa
Ukienda maeneo hayo ukakuta utulivu usio wa kawaida usijaribu kuingia majini
Kujiokoa mdomoni mwa mamba ni ngumu
Ila jaribu tu kumbinya tumbo

8 Mbwa mwitu
Hawa hutembea kundi kubwa unakuta wapo zaidi ya 50
Hawa ukiwaona panda mti
Somo zuri, Thanks.

>>Kama ni hivyo bora niwe naenda kwenye zoo tu. Mawe😜

Hata hivyo ndio utagundua mababu zetu walivyokuwa majasiri. Karibia wanyama wote hao walikuwa kitoweo.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ikitokea umebananishwa na umekutana na mojawapo wa wanyama hawa wakali Fanya haya kujiokoa

1 Simba
Huyu ni mnyama mkali sana
Ukikutana na Simba porini panda mti, au jiamini mtizame na uanze kumfukuza
Simba anaogopa ujasiri wa kiumbe yeyote atakimbia

2. Chui
Chui huishi mafichoni, chui hukaa peke yake
Ukikutana na chui, jifanye hujamwona.
Chui ni dhaifu, usimchokoze maana anaweza kukubadilikia

3. Tembo
Huyu ni mpole, ila ukikuta amevurugwa labda amepoteza ndama ujue safari yako imeishia hapo atakuua akukanyage uwe kama chapati
Ukikutana nae kamba Kuna mlima kimbia kama unateremka, au ingia shimoni au ndani kama Kuna nyumba

Usije ukapanda mti ukimwona tembo

4.Nyati/ Faru
Ukikutana na wanyama hawa una asilimia 80 za kuwa marehemu,
Hawa Bora ukitane na Simba
Vyote omba ila usikutane na hawa viumbe porinii dadeki

5 Chatu
Kama unaenda porini na unahisi Kuna Chatu penda kutembea na mbwa, Atamkamata mbwa we ukimbie, maana na Chatu na mbwa wana uadui wao

6 Fisi
Hawa huvizia usiku na huogopa mwanga, we tembea na tochi
Au akikuvuzia kamata mkia

6. Nyoka
Hawa wapo wa aina tofauti na kila nyoka ana tabia zake
Kuna wanaovizia, wanaoshambuliwa, wanaosubiri uwakanyage n. K
Kikubwa ukipata ajali ya nyoka kunywa mkojo wako

7 Mamba
Hawa hukaa ukingoni mwa moto au ziwa
Ukienda maeneo hayo ukakuta utulivu usio wa kawaida usijaribu kuingia majini
Kujiokoa mdomoni mwa mamba ni ngumu
Ila jaribu tu kumbinya tumbo

8 Mbwa mwitu
Hawa hutembea kundi kubwa unakuta wapo zaidi ya 50
Hawa ukiwaona panda mti
Simba na chui wa siku hizi huishi juu ya miti na ndiyo dipufriza zao za kutunzia nyama, kwahiyo utajitanguliza mwenyewe.
Tembo, nyumba za vijijini huziondoa paa kutafuta mahindi,bhatakuelewa akikuona humo, ukiingia shimoni atakandamiza ulipoingilia mpaka ukose hewa, tembo ni watu wanene waliofariki zamani.
Mamba binya kwa vidole macho yake kwani tumbo lake hautaweza kulifikia kwani hujiviringisha akishika kitu.
Muhimu acha kutembea porini kama siyo jangiri au jifanye mmaasai.
 
Nishasikia Hawa Mbwa mwitu Wana ka mchezo ka kumtanguliza mmoja kama chambo na wanaselect yule dhaifu ili umnyanyase, sasa jichanganye .
Huu mtego umewaponza sana baadhi ya wanyama hatari mwituni kwa kujidai wao ndio mabingwa yakawatokea puani.
 
Hiyo ndiye njia pekee ya kujikomboa kwa mnyama.simba, tena kwa mwanamke ni added advantage ukiwa uchi wa mnyama ukabinuka hivyo plus hayo maziwa kifuani simba atachanganya mbio balaa
Huu utafiti na majaribio ulifanya wapi,lini na ushahidi uko wapi?
 
Tembo uingie ndani ya nyumba!!! Umeisha
Inategemeana na nyumba utakayokimbilia,ila kwa mazingira ya kijijini nyumba nyingi ni tope na zimeezekwa kwa nyasi hapo nakushauri usikimbilie humo. mwaka 2016 nilikuwa na kiredio changu uck nilikuwa nakiwasha non stop,kumbe bhana tembo wanapita nje,mmoja mkubwa wao akajaribu kutikisa kiberiti nikakizima kiredio nikaingia uvunguni na mkojo ukifuatia. kijiji chetu kwa miaka mingi kimekuwa kilikumbana na masahibu ya tembo kila mwaka wanavamia na kula mazao ya wakulima mana kijiji chetu kina poli la akiba. ila tunashukru serikali kwa kuingia ubia na kampuni ya allience one kufanya project ya upandaji wa miti, sasa hali ni shwari.
 
Je ukikutana na Lisu na Chadema yake unatakiwa ufanye nini??
 
Back
Top Bottom