Fanya hivi ukikutana na wanyama hawa porini

Fanya hivi ukikutana na wanyama hawa porini

Ni kweli kuna maelekezo mengi yameshatolewa juu ya Mtu ufanye nini unapokutana na Mnyama fulani ila bado kuna changamoto ya kupata matokeo chanya (positive) wakati wote. Kwa mfano hapo kwenye Simba haipishani sana na maelekezo utakayopewa kuhusu nini ufanye unapokutana na Mbwa mkali.Ila my friend sio wakati wote utafanikiwa maana itategemea naye amekutana na nini muda mchache kabla hamjakutana.Hawa jamii ya Paka hawatabiriki kirahisi,ni kweli Wana uwezekano mkubwa wa kupuuzia ili mradi tu nawe usihangaike naye.Na zipo shuhuda hizo,ila nasisitiza haitotokea mara zote. Kuhusu Chui nadhani neno sahihi ni "shy" Wana aibu ila sio dhaifu.Kwa kupenda kwao utulivu anaweza akakuacha tu upite zako ali mradi nawe usiwe na habari naye.Ila kama kwa Simba inaweza Isiwe hivyo mara zote. Hapo kwa Nyoka hawa nao ni viumbe wanaotajwa kama wenye aibu "shy" na mara nyingi huchagua kukimbia kama atafanikiwa yeye kukuona mapema, ila ndio hivyo wakati mwingine bila ya kujua unaweza kujikuta umemuweka yeye hatarini bila kukusudia naye atakugonga tu.Ila hapo kwenye ushauri wa nini Mtu afanye akigongwa naona umepotosha.Tahadhari ni kukwepa kupita kwenye majani marefu au basi uwe umevaa buti na suruali n.k.
Hapo kwenye suruali ni kwamba atang'ata suruali na si ngozi au maana ya kuvaa suruali ni nini
 
Hapo kwenye nyati na faru umekosa kabisa Cha kushauri zaidi ya kusubiri kifo
 
Ikitokea umebananishwa na umekutana na mojawapo wa wanyama hawa wakali Fanya haya kujiokoa

1 Simba
Huyu ni mnyama mkali sana
Ukikutana na Simba porini panda mti, au jiamini mtizame na uanze kumfukuza
Simba anaogopa ujasiri wa kiumbe yeyote atakimbia

2. Chui
Chui huishi mafichoni, chui hukaa peke yake
Ukikutana na chui, jifanye hujamwona.
Chui ni dhaifu, usimchokoze maana anaweza kukubadilikia

3. Tembo
Huyu ni mpole, ila ukikuta amevurugwa labda amepoteza ndama ujue safari yako imeishia hapo atakuua akukanyage uwe kama chapati
Ukikutana nae kamba Kuna mlima kimbia kama unateremka, au ingia shimoni au ndani kama Kuna nyumba

Usije ukapanda mti ukimwona tembo

4.Nyati/ Faru
Ukikutana na wanyama hawa una asilimia 80 za kuwa marehemu,
Hawa Bora ukitane na Simba
Vyote omba ila usikutane na hawa viumbe porinii dadeki

5 Chatu
Kama unaenda porini na unahisi Kuna Chatu penda kutembea na mbwa, Atamkamata mbwa we ukimbie, maana na Chatu na mbwa wana uadui wao

6 Fisi
Hawa huvizia usiku na huogopa mwanga, we tembea na tochi
Au akikuvuzia kamata mkia

6. Nyoka
Hawa wapo wa aina tofauti na kila nyoka ana tabia zake
Kuna wanaovizia, wanaoshambuliwa, wanaosubiri uwakanyage n. K
Kikubwa ukipata ajali ya nyoka kunywa mkojo wako

7 Mamba
Hawa hukaa ukingoni mwa moto au ziwa
Ukienda maeneo hayo ukakuta utulivu usio wa kawaida usijaribu kuingia majini
Kujiokoa mdomoni mwa mamba ni ngumu
Ila jaribu tu kumbinya tumbo

8 Mbwa mwitu
Hawa hutembea kundi kubwa unakuta wapo zaidi ya 50
Hawa ukiwaona panda mti
Wewe hizo mbinu umezitoa wapiii???
Kama ni akili Yako
BIG NO
 
Mbinu nyingine tunadanganyana. Wanasema ukikutana na nyoka mkague muundo wa macho yake kumjua kama ana sumu au hana. Yakiwa na shepu kama kisu basi huyo ana sumu, na yakiwa yana shepu kama duara huyo hana sumu.

Yaani niache kutimua mbio, eti nimsomgolee nimtazame machoni
Msogeleee uuponze
 
Hapa inabidi zile za kuambiwa uchukue kiduchu na za kwako ziwe nyingiiii walau ukizichanga utapata suluhu........ Ila si haba umetukumbusha uhatari wa haya madubwana.
 
Ukikutana na simba vua nguo zote halafu mbong'olee yaani geuka nyuma inama kisha aone matako yako, simba ataogopa kwa maana hayo matako atahisi kama ni vichwa viwili hivyo atasitaajabu na kukimbia kwakuwa hajawahi kuona.mnyama mwenye vichwa viwili.
Ulisha jaribu na ikafanya kazi au unataka kutuponza
 
Back
Top Bottom