Fanya Jaribio Hili La Siku 30 Litakaloubadili Mwaka 2021 Uwe Wa Mafanikio Makubwa Kwako



Hii ifanyiwe Maboresho. Ni bora kuwa na written goals (short, medium, long term)

Then kila siku mtu anaandika “to do list” za kueleweka towards achieving those goals
 
Hii ifanyiwe Maboresho. Ni bora kuwa na written goals (short, medium, long term)

Then kila siku mtu anaandika “to do list” za kueleweka towards achieving those goals
Asante sana mkuu kwa nyongeza hii.
Hii ipo kwenye kitabu ambacho ni mwongozo wa zoezi hili la siku 30

 
Reactions: Pep
Mada hii inamlenga mtu yeyote anayetaka kupiga hatua kwenye maisha yake,bila ya kujali anaanzia wapi.
Nawe pia unaweza kuwa mmoja wao, karibu sana.
Kitabu kitakuwa kinawalenga wafanyabiashara zaidi,
 
Tatizo kubwa la Watoa Ushauri ( Mawazo ) mazuri, ya Kuelimisha na kutia moyo kama haya Wao wenyewe ukibahatika Kuwakuta wala hawaishi kama hivi walivyoandika. Anyways thanks for these Vital Tips na Ubarikiwe pia.
 
Kitabu kitakuwa kinawalenga wafanyabiashara zaidi,
Siyo kweli mkuu,
Kitabu kinamlenga yeyote anayetaka kupiga hatua zaidi kwenye maisha hake,
Iwe hana kazi, ameajiriwa au anafanya biashara.
Kina mbinu za kumwezesha mtu kuanzia pale alipo sasa na kupiga hatua zaidi.
Karibu sana ukisome.
 
Tatizo kubwa la Watoa Ushauri ( Mawazo ) mazuri, ya Kuelimisha na kutia moyo kama haya Wao wenyewe ukibahatika Kuwakuta wala hawaishi kama hivi walivyoandika. Anyways thanks for these Vital Tips na Ubarikiwe pia.
Usemalo ni kweli mkuu,
Huwa kuna kauli kwamba wasioweza kufanya hufundisha na ndivyo ilivyo kwenye kila eneo.
Hata walimu wa vyuo vikuu, huwa wanafundisha lakini ni nadra sana wao kufanya yale wanayofundisha.
Mfano mwalimu wa masomo ya biashara hana hata biashara.
Kuna mengi ya kuchimba hapo ila tusiende mbali sana.

Sasa tukirudi kwangu, nilianza kuandika rasmi mwaka 2013 na nilijiwekea msimamo huu, najifunza vitu kupitia usomaji wa vitabu, navitumia kwenye maisha yangu na kisha nawashirikisha wengine.
Na hivyo ndiyo nimekuwa nafanya, kila ninaloshirikisha nimefanya kwenye maisha yangu.
Nikukaribishe sana kama utapenda kunifuatilia kwa karibu,
Maana hiki siyo kitu nafanya leo na kesho, ni kitu nilichoamua nitakifanya maisha yangu yote pale nitakapokuwa hai.
Karibu sana.
 
Naona nayaweza tisa la kumi lanitesa kutokana na maisha yangu kipato sio cha kuukimbia wanga kabisa
 
Reactions: Pep
Tatizo lenu motivesheni spikazi huwa mnapenda sana kuandika au kuongea kwa kujumuisha watu wote kana kwamba wanaishi maisha yanayofanana. Mfano hapo kwenye ulaji wa vyakula, kuna watu mfano mimi, siwezi kula chakula kingi cha protein, lazima nile wanga wa kutosha protein kias ili niweze kumudu kazi yangu.

Ungetofautisha hapo kwa namna maisha yetu yalivyo. Wewe mkaa kwenye kipupwe full time, na mimi mhenyekaji wa kazi nzito hatuwezi kuwa sawa. Swala la ngono usilihesabie kabisa, kama unafanya ngono na huli vizuri hilo ni tatizo, ila kama unakula vizuri na unakula mbususu vyedi hata akili inafanya kazi vyema. Hayo mengine wenzangu watachangia
 
Karibu mkuu,
Ushauri au mafunzo yoyote unayopata kwenye maisha huwa ni mwongozo tu, wa mambo muhimu kuzingatia.
Lakini lazima uuchakate na kuona unautumiaje kulingana na hali yako binafsi.
Itakuwa ni hatari sana kama utakopi na kupesti kila unachoshauriwa au kuambiwa na wengine.
Maisha yangekuwa rahisi hivyo kila mtu angekuwa amefanikiwa sana, maana ushauri wa mafanikio ni mwingi kila kona.
Tunapokwama siyo kwa kukosa ushauri au mafunzo mazuri, hivyo ni vingi mno kwa sasa.
Tunapokwama ni kushindwa kuvichakata kwa namna vinaendana na sisi ili tuvitumie kwa ubora.
Tumezoea sana kutafuniwa kila kitu sisi tuweze tu.
Sasa kwenye mafanikio hakuna anayeweza kukutafunia, maana hakuna anayejua unataka nini hasa isipokuwa wewe mwenyewe.
Hivyo chukua hizi kama guidelines, lakini ziprocess kisha integrate kwenye maisha yako kwa namna inayokufaa wewe.
Kila la kheri.
 
SIKU YA KWANZA TAFAKARI YA ASUBUHI.
Hongera kwa wale mliochukua challenge hii ya kuishi tabia hizi kwa siku 30.
Kwenye siku hii ya kwanza tafakari tabia ambazo umekuwa nazo kwenye maisha yako.
Chagua siku moja, labda jumatatu ya wiki iliyopita kisha chukua karatasi na igawe pande mbili;
👉Upande wa kwanza andika malengo yako yote uliyonayo kwenye maisha.
👉Upande wa pili orodhesha yake yote uliyofanya kwenye siku uliyochagua, tangu unaamka mpaka utarudi kulala.
Kisha chora mstari kwenye kila ulilofanya kwenda kwenye lengo ambalo linahusiana na hicho ulichofanya.
Kwa yale ambayo umefanya na hayahusiani na malengo yako, yafute kabisa kwenye maisha yako.
Fanya zoezi hili muhimu leo kujua tabia ambao unazo na hazina mchango kwenye malengo yako kisha ziache mara moja.
Kupata kitabu cha tabia za kitajiri fungua; www.bit.ly/somavitabuapp
 
Pamoja sana mkuu
 
Kocha Dr. Makirita Amani

Kuna sheria ya 21/90.
Siku 21 mwanadamu anao uwezo wa kujijengea tabia mpya.

Siku 90 mwanadamu anaweza kujijengea aina na mtindo wake mpya wa mfumo wa maisha.

Katika usomaji wangu wa vitabu nimeona kuna siri kubwa sana ya kuamka saa 11 Alfajir.Kitu cha kwanza ni kuanza kushukuru lkn kama pia kutaendana na nakushukuru na nakufanya tafakuri ya maneno ya kiroho.

Kwamba kwa yale unayoyatarajiwa kuwa unayejenga katika fikra yaweze kuwa katika uhalisia inakuwa ni kama maandalizi ya kuyaandaa.
 
Reactions: Pep
Asante mkuu kwa nyongeza hii.
Ni kweli kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…