SIKU YA 10 TAFAKARI YA ASUBUHI; UNALIPWA KWA THAMANI.
Kiwango cha fedha unacholipwa ni sawasawa na thamani unayozalisha.
Kama unafanya kazi na mshahara unaolipwa ni mdogo, maana yake thamani unayozalisha ni ndogo.
Kama unafanya biashara na faida unayopata ni ndogo maana yake thamani unayoitoa ni ndogo pia.
Hatua ya kwanza kwenye kuongeza kipato chako ni kuanza kuongeza thamani unayoitoa.
Kama umeajiriwa, toa thamani kubwa kwa mwajiri wako kiasi kwamba hatakuwa tayari kukupoteza na hapo atakuwa tayari kukulipa zaidi.
Kama unafanya biashara, jitofautishe kwa kutoa thamani kubwa ambayo wateja wako hawawezi kuipata sehemu nyingine. Hapo utakuwa na wateja wengi na ambao watakuwa tayari kulipa zaidi.
Na muhimu zaidi, usipende kulipwa kwa muda unaofanya kitu, bali penda kulipwa kwa thamani unayozalisha.
Maana muda una ukomo, ila thamani haina ukomo. Zalisha thamani kubwa na utalipwa kiasi kikubwa.
Jifunze zaidi kwenye kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI hapa;
www.bit.ly/somavitabuapp