Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,914
- 3,438
- Thread starter
- #41
SIKU YA KWANZA; TATHMINI YA USIKU.SIKU YA KWANZA TAFAKARI YA ASUBUHI.
Hongera kwa wale mliochukua challenge hii ya kuishi tabia hizi kwa siku 30.
Kwenye siku hii ya kwanza tafakari tabia ambazo umekuwa nazo kwenye maisha yako.
Chagua siku moja, labda jumatatu ya wiki iliyopita kisha chukua karatasi na igawe pande mbili;
👉Upande wa kwanza andika malengo yako yote uliyonayo kwenye maisha.
👉Upande wa pili orodhesha yake yote uliyofanya kwenye siku uliyochagua, tangu unaamka mpaka utarudi kulala.
Kisha chora mstari kwenye kila ulilofanya kwenda kwenye lengo ambalo linahusiana na hicho ulichofanya.
Kwa yale ambayo umefanya na hayahusiani na malengo yako, yafute kabisa kwenye maisha yako.
Fanya zoezi hili muhimu leo kujua tabia ambao unazo na hazina mchango kwenye malengo yako kisha ziache mara moja.
Kupata kitabu cha tabia za kitajiri fungua; www.bit.ly/somavitabuapp
Ikamilishe siku yako kwa kujifanyia tathmini ya jinsi ulivyoziishi tabia hizi mpya leo na jinsi siku ilivyoenda kwa ujumla.
Kwenye kitabu cha tabia za kitajiri kuna maelezo mazuri ya jinsi ya kujifanyia vizuri tathmini hii.
Kama bado hujapata kitabu hicho, ingia sasa; www.bit.ly/somavitabuapp