Fanya Jaribio Hili La Siku 30 Litakaloubadili Mwaka 2021 Uwe Wa Mafanikio Makubwa Kwako

SIKU YA KWANZA; TATHMINI YA USIKU.
Ikamilishe siku yako kwa kujifanyia tathmini ya jinsi ulivyoziishi tabia hizi mpya leo na jinsi siku ilivyoenda kwa ujumla.
Kwenye kitabu cha tabia za kitajiri kuna maelezo mazuri ya jinsi ya kujifanyia vizuri tathmini hii.
Kama bado hujapata kitabu hicho, ingia sasa; www.bit.ly/somavitabuapp
 
SIKU YA PILI; TAFAKARI YA ASUBUHI.
Watu wanaokuzunguka na unaotumia nao muda wako mwingi wana ushawishi mkubwa sana kwako.
Jinsi ulivyo sasa ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka na unaotumia nao muda wako mwingi.
Hivyo hatua muhimu kwenye kubadili maisha yako ni kubadili watu unaotumia nao muda wako mwingi.
Kagua watu wote unaowapa muda wako, jua ni wapi wanakusukuma kupiga hatua na wapi wanakurudisha nyuma.
Achana na wanaokurudisha nyuma na endelea na wanaokusukuma kupiga hatua.
Soma zaidi kwenye kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, fungua; www.bit.ly/somavitabuapp
 
Kwani sisi wa miaka 50 tuna lipi la kufanya hapo?
 
Ahsante sana kwa uzi mzuri na Mungu akubariki sana.
 
 
Kwani sisi wa miaka 50 tuna lipi la kufanya hapo?
Unafanya yote,
Miaka 50 bado ni midogo sana kwenye safari ya mapambano ya maisha.
Sayansi inakua kwa kasi na umri wa watu kuishi unaongezeka sana, hasa mtu ukiwa na nidhamu na fedha pia.
Hivyo miaka 50 ya zama hizi ni sawa na miaka 30 ya zama zilizopita.
Fanyia kazi yote ili umri unavyokwenda usiwe mtu wa lawama kwa wengine.
 
SIKU YA PILI; TATHMINI YA USIKU.
Tafakari ya asubuhi ya leo ilihusu kukagua mahusiano yetu na kuona yapi yasiyofaa na kuachana nayo.
Kuna watu wanaitwa 'watu sumu' (toxic people), watu hawa huona ubaya, ugumu na kushindwa kwenye kila jambo.
Ni watu waliokata tamaa na walio vizuri kwenye kuhakikisha wengine pia wanakata tamaa.
Hawa ni watu wa kuwafuta kwenye maisha yako bila kuchelewa au kubembeleza maana watakuvuta na kukurudisha nyuma.
Huhitaju kugombana nao, wala huhitaji kuwaambia chochote.
Ukishajua mtu ni sumu, usimpe muda kwenye maisha yako, kuwa bize na yale muhimu kwako kiasi kwamba hupati muda wa kupoteza kwa watu wa aina hiyo.
Dunia ina watu wengi sahihi kwako, acha kung'ang'ana na wanaokurudisha nyuma.
Soma kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI kujifunza zaidi, fungua; www.bit.ly/somavitabuapp
 
SIKU YA 3 TAFAKARI YA ASUBUHI; CHAKULA CHA AKILI.
Kila siku unaulisha mwili wako chakula,
Kila siku unauvalisha mwili wako mavazi,
Unatumia gharama kubwa kwenye kulisha na kuvisha mwili wako.
Lakini je ni juhudi kiasi gani unaweka kwenye kulisha na kuvisha akili yako?
Chakula cha akili ni maarifa mazuri.
Mavazi ya akili ni maarifa mazuri.
Hakikisha unailisha na kuivisha vizuri akili yako.
Kama unavyougharamia mwili, ndivyo pia unapaswa kuigharamia akili yako.
Usilishe mwili ukaacha akili ikiwa na utapiamlo.
Usivishe mwili ukaacha akili ikiwa uchi.
Ubora wa maisha yako unategemea sana uwekezaji uliofanya kwenye akili yako.
Weka kipaumbele sasa kwenye uwekezaji wa akili yako kwa kupata maarifa yaliyo sahihi.
Soma zaidi kwenye kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, kukipata fungua; www.bit.ly/somavitabuapp
 
Kwani sisi wa miaka 50 tuna lipi la kufanya hapo?
Sawa sawa mkuu nimekuona vizuri! Hongera kwa kujitolea kuwajenga vijana!
 
sis tunaoishi kwa kubet huu Uzi tunaupita tu
 
Tatizo kubwa la Watoa Ushauri ( Mawazo ) mazuri, ya Kuelimisha na kutia moyo kama haya Wao wenyewe ukibahatika Kuwakuta wala hawaishi kama hivi walivyoandika. Anyways thanks for these Vital Tips na Ubarikiwe pia.
Lengo ni biashara ya Kitabu chake. Hata hivyo fuata ushauri usifuate matendo.
 
As a spiritpreneur, I'm saying this; do what makes you happy always, all great things have small beginnings, there is no overnight success.
 
SIKU YA TATU TATHMINI YA USIKU; USAFI WA AKILI...
Akili yako imejaa kila aina ya uchafu ulioingia kutokana na maarifa hasi ambayo umekuwa unakutana nayo kila siku.
Pamoja na kuchagua kulisha akili yako maarifa chanya, unahitaji pia kufanya usafi wa akili yako, kwa kuondoa fikra na mitazamo yote hasi uliyojijengea mpaka sasa.
Zoezi la kusafisha akili yako unalifanya kwa kutahajudi (meditation) na kuwa na kauli chanya unazojiambia (affirmation) mara kwa mara.
Kila fikra hasi inayoingia kwenye akili yako, usiipe muda na nafasi ya kukua, bali iondoe haraka kwa kutumia kauli chanya ulizojitengenezea.
Kama unavyosafisha mwili wako kila siku ili uwe safi, ndivyo pia unavyopaswa kusafisha akili yako ili ifikiri kwa usahihi na kukuwezesha kufanya makubwa.
Kama bado hujasoma kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI unakosa maarifa mazuri kwako ya kuboresha maisha yako, fungua sasa; www.bit.ly/somavitabuapp
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…