Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,914
- 3,438
- Thread starter
-
- #61
SIKU YA NNE TATHMINI YA USIKU; USHAWISHI WA FIKRA ZAKO.SIKU YA NNE TAFAKARI YA ASUBUHI; NGUVU YA FIKRA.
Unakuwa vile unavyofikiri,
Hapo ulipo sasa ni matokeo ya fikra ambazo umekuwa nazo kipindi cha nyuma.
Kama unapitia magumu sasa ni kwa sababu umekuwa unafikiri kwa magumu.
Fikra zetu ni sumaku, zinavuta kwenye maisha yetu kile tunachokifikiria kwa muda mrefu.
Hivyo hatua ya kwanza ya kuyabadili maisha yako ni kuzibadili fikra zako.
Kagua fikra zote zisizokujenga ambazo umekuwa nazo,
Fikra hasi, kufikiri magumu na kushindwa muda wote.
Kuwa na fikra zinazojenga na kukuwezesha kupiga hatua, fikra chanya na za uwezekano.
Japo kufikiri chanya pekee hakuwezi kuyabadili maisha yako (tutaona mengine muhimu ya kuambatana na fikra), huwezi kuyabadili maisha yako bila kubadili fikra zako.
Kubadili fikra ndiyo hatua ya kwanza na ya muhimu katika kubadili maisha yako.
Na lazima ujue fikra zipi zimekuwa kikwazo kwako mpaka sasa na uachane nazo.
Leo fanya zoezi hili la kuzikagua fikra ambazo zimekuwa zinaitawala akili yako, kujua zipi zinajenga na zipi zinabomoa.
Ondoa zinazobomoa na baki na zinazojenga.
Kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI Ni sehemu sahihi kwako kuanza kujenga fikra mpya na za kiyaboresha maisha yako, kisome sasa hapa; www.bit.ly/somavitabuapp
SIKU YA TANO TATHMINI YA USIKU; MAZOEA YA KUVUNJA.SIKU YA TANO TAFAKARI YA ASUBUHI; MAZOEA.
Sisi binadamu ni viumbe wa tabia, huwa tunazijenga tabia kisha zikishakomaa ndiyo zinaendeshwa maisha yetu.
Huwa ni rahisi kuendelea kufanya kile tulichozoea kufanya kuliko kufanya kipya ambacho hatujazoea.
Mazoea ndiyo yamekuwa kikwazo kwa wengi kufanikiwa kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla.
Hivyo ni muhimu sana kila mmoja wetu kupambana kuyavuka mazoea.
Kwenye kila siku yako jaribu kufanya kitu kipya ambacho kipo nje kabisa ya mazoea yako.
Jaribu kufanya kitu ambacho umekuwa unahofia kukifanya au umekuwa unaona huwezi kukifanya.
Mwanzo itakuwa vigumu, lakini unapodhamiria unaweza kufanya na ukabadili matokeo unayopata.
Ipo kauli kwamba ujinga ni kufanya kitu kile kile, kwa namna ile ile halafu kutegemea upate matokeo tofauti.
Usiwe mjinga, kama unataka kupata matokeo tofauti na unayopata sasa, lazima uachane na mazoea na ufanye kwa utofauti.
Soma kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI ujifunze jinsi ya kuvunja mazoea ambayo ni kikwazo kwako. Kukipata fungua hapa; www.bit.ly/somavitabuapp
Karibu mkuu.Ahsante kwa kutukumbusha
SIKU YA SITA TATHMINI YA USIKU; IMANI ZA KUVUNJA.SIKU YA SITA TAFAKARI YA ASUBUHI; IMANI ULIZOJIJENGEA.
Fikra na mitazamo ambayo umekuwa nayo kwa muda mrefu, hugeuka na kuwa imani.
Imani ulizonazo ndiyo zinaamua aina ya maisha unayokuwa nayo.
Mfano kama tangu ukiwa mtoto umekuwa unaambiwa huna akili au huwezi, unafika mahali na hicho inakuwa ni kitu unachoamini kabisa.
Hivyo kila unapopata fursa mpya, imani yako inapelekea unaiharibu ili tu uthibitishe kwamba huwezi.
Kadhalika kama umekua ukiamini wewe ni masikini na utabaki kwenye umasikini huo, hata ukipata fedha utazitapanya mpaka urudi kwenye hali uliyokuwa nayo kabla ya kuwa na fedha.
Maamuzi mengi unayoyafanya kwenye maisha unayafanya ili kulinda imani ulizojijengea ndani yako.
Hivyo ili kuyabadili maisha yako, kuna imani ulizonazo unapaswa kuzivunja na kujijengea imani nyingine mpya.
Kuna imani zinakuwekea ukomo ambazo kama hutazivunja basi hutaweza kupiga hatua.
Na zipo imani zinazokuweka huru zaidi ambazo unapaswa kujijengea ili kupiga hatua.
Kuna imani 17 unazopaswa kujijengea inapokuja kwenye swala la fedha na utajiri, zijue kwa kusoma kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, fungua; www.bit.ly/somavitabuapp
SIKU YA 7 TATHMINI YA USIKU; NITAFANYA SASA.SIKU YA 7 TAFAKARI YA ASUBUHI; NAMNA YA KUTENDA.
Tumeshaona jinsi fikra, imani na mitazamo tunayokuwa nayo vinavyoathiri matokeo tunayopata.
Lakini hivyo havina nguvu peke yake, bali vinapewa nguvu na hatua ambazo mtu unachukua.
Namna yako ya kutenda, yaani kuchukua hatua kwenye mambo yako mbalimbali unayofanya, inaamua kama utapata matokeo mazuri au mabaya, kama utafanikiwa au utashindwa na kama utapata utajiri au kubaki kwenye umasikini.
Unapaswa kujijengea namna tofauti ya kutenda, namna ambayo unafanya vitu vyako kwa viwango vya juu sana.
Kwa kila unachofanya, lengo lako la kwanza linapaswa kutoa thamani kubwa kwa wengine.
Kabla hujaangalia wewe unapata nini, jiulize kwanza ni mchango gani unaotoa kwa wengine.
Unapotoa thamani kubwa kwa wengine ambayo inayafanya maisha yao kuwa bora, watakuwa tayari kukupa kile unachotaka.
Kitu kingine muhimu sana kwenye utendaji ni kuepuka tabia ya kuahirisha mambo. Hii ni tabia iliyokomaa kwa wengi na kuwa kikwazo kwa mafanikio yao.
Mtu anapanga vizuri nini atafanya, ila wakati wa kufanya unapofika anaahirisha na kusogeza mbele.
Wewe usiwe mtu wa aina hii, panga na fanya kama ulivyopanga. Usiruhusu sababu yoyote ile iwe kikwazo kwako kufanya yale ambayo ni muhimu.
Kuwa na namna bora ya kufanya mambo yako na hiyo itakuwezesha kufanya makubwa.
Soma kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI kujifunza zaidi; fungua, www.bit.ly/somavitabuapp
Ubarikiwe sana mh umeniencourage sanaRafiki yangu mpendwa,
Unaweza kuamini tayari tumefika mwezi wa tano kwenye mwaka huu wa 2021?
Mwaka ambao siku siyo nyingi ulikuwa unauita mwaka mpya na ukajiambia kabisa utakuwa mwaka wa mambo mapya!
Sihitaji kukukumbusha jinsi ambayo mengi uliyojipangia kwa mwaka huu umeshaachana nayo, hivyo ndivyo ilivyo kwa wengi.
Leo nimekuja kwako na pendekezo moja, siyo la kurudi kule ulikopanga na kushindwa, bali pendekezo la kujaribu kitu kipya.
Anza kukijaribu kwa siku 30 tu kisha zinapoisha jifanyie tathmini kuona mabadiliko gani yametokea kwenye maisha yako.
Kama utayapenda mabadiliko hayo endelea na zoezi hilo kwa mwaka mzima, kama hutayapenda achana nalo na rudi kwenye mazoea yako.
Ni siku 30 tu za kufanya jaribio hili na huna cha kupoteza, maana hakuna gharama au kazi ya ziada unayotakiwa kufanya.
JARIBIO LA SIKU 30 LA KUUFANYA MWAKA HUU KUWA WA MAFANIKIO MAKUBWA
Mafanikio yetu yanajengwa au kubomolewa na tabia tunazoziishi kila siku.
Siku zetu zinaendeshwa zaidi na tabia ambazo tayari tumeshajijengea.
Ndiyo maana huwa unasikia huwa tunajenga tabia na kisha tabia zinatujenga.
Kwa siku 30, unakwenda kufanya jaribio la kuziishi tabia 10 ninazokwenda kukushirikisha hapa.
Kila siku kamilisha tabia hizo kumi bila kuacha hata siku moja, kisha siku 30 zinapoisha, jifanyie tathmini ya mabadiliko unayoyaona kwenye maisha yako.
TABIA KUMI ZA KUISHI KWA SIKU 30
1. Kila siku amka mapema, saa moja kabla ya muda wako uliozoea kuamka. Ukishaamka usiangalie simu wala usumbufu wowote, bali anza kwa kufanya sala na/au tahajudi (meditation) kisha chukua notebook yako na andika vipaumbele vya siku hiyo, mambo ambayo utakwenda kufanyia kazi (To Do List). Hayo ndiyo mambo utakayoyapa kipaumbele kwenye siku yako, usifanye mengine kabla hayo hayajaisha.
2. Kila siku fanya mazoezi kwa dakika zisizopungua 30, mazoezi mazuri ni ya kukimbia.
3. Kila siku soma kitabu kwa angalau dakika 30, chagua kitabu chochote unachotaka kusoma, iwe ni cha maendeleo binafsi au maendeleo ya kitaaluma kisha soma kwa angalau dakika 30 kila siku.
4. Kila siku pangilia na dhibiti ulaji wako, punguza kabisa vyakula vya wanga na sukari, kula mboga mboga na matunda kwa wingi, kula nyama kwa kiasi na kunywa maji mengi. Pia dhibiti sana vilevi unavyotumia.
5. Kila siku mpigie simu mteja mmoja ambaye amewahi kunufaika na biashara au kazi yako na ongea naye kuhusiana na biashara au kazi yako na changamoto alizonazo unazoweza kumsaidia kutatua. Pia mpigie mteja tarajiwa mmoja, ambaye bado hajanunua ila ana uhitaji ambao unaweza kumsaidia, mwoneshe jinsi unavyoweza kutatua tatizo lake.
6. Kila siku mpigie simu mtu mmoja wa karibu, ndugu jamaa na marafiki na kuwa na maongezi naye ya kuboresha mahusiano yenu.
7. Kila siku jaribu kitu kipya na ambacho umekuwa unahofia kufanya au umekuwa unaona huwezi, hata kama ni kidogo, fanya. Hii inajenga ujasiri wako na kukuwezesha kuvuka hofu.
8. Kila siku kuwa na fikra chanya, fikra za mafanikio na utajiri mkubwa. Pata muda wa kuwa peke yako na jenga taswira ya ndoto kubwa ulizonazo, jione kama tayari umeshazifikia na amini ni kitu ambacho tayari kipo. Jenga taswira hii kwenye fikra zako na pia kuwa na picha ya ndoto ulizonazo unayotembea nayo au iliyo kwenye simu yako na iangalie mara kwa mara.
9. Kwa kila kipato unachoingiza, iwe ni kwa siku, wiki au mwezi, weka pembeni angalau asilimia kumi ya kipato hicho na iweke mahali ambapo huwezi kuitumia. Fedha ya ziada unayoipata ambayo hukuitegemea, yote iweke kwenye fungu hilo.
10. Kila siku unapoimaliza siku yako, jipe muda wa kutafakari jinsi siku hiyo ilivyokwenda. Jua yapi umefanya vizuri, yapi umekosea na wapi unapaswa kuboresha zaidi. Andika kwenye notebook yako yale uliyojifunza kwenye tafakari hiyo ya jioni. Kwa kufanya tafakari hii kila siku, utaendelea kuwa bora zaidi kwa kila siku mpya unayokwenda kuanza.
Rafiki, ni mambo hayo kumi tu ya kufanya kila siku kwa siku 30 bila kuacha hata siku moja, kisha siku 30 zikiisha jifanyie tathmini, kama matokeo ni mazuri fanya hiyo kuwa sehemu ya maisha yako.
NAFASI YA KUSIMAMIWA KWA KARIBU NA KOCHA
Rafiki, unaweza kuhamasika hapa na kuona ni kitu rahisi kufanya, lakini utakapoanza kufanya ndiyo utajua siyo rahisi kama inavyoonekana.
Mazoea ambayo tayari unayo yatakuwa kikwazo kikubwa kwako kufanya jaribio hilo, kila mara utashawishika kuacha na kurudi kwenye mazoea.
Hivyo kama unataka kufanya zoezi hili kwa siku 30 bila kuacha, unahitaji usimamizi wa karibu.
Hapa natoa nafasi kwa watu wachache wanaotaka kusimamiwa kwenye hili niwasimamie.
Kupata nafasi hiyo ya kusimamiwa pata kwanza zawadi ya kitabu kipya cha TABIA ZA KITAJIRI, kitabu kinapatikana hapa; Soma Vitabu - Apps on Google Play
Ukishapata kitabu hicho tuma ujumbe kwenda wasap namba 0717396253 wenye maneno USIMAMIZI WA TABIA ZA KITAJIRI na utapata maelekezo zaidi.
Kwa maulizo yoyote kuhusiana na zoezi hili la siku 30, tuma ujumbe kwenda wasap namba 0717396253.
Kama kwa kusoma hapa nafsi yako imekuambia hiki ni kitu unachohitaji, basi isikilize, achana na kauli nyingine utakazokuwa unajiambia kwamba huwezi au mambo haya siyo muhimu.
Nafsi yako inakujua vizuri wewe, isikilize na shiriki zoezi hili la siku 30 na utaona mwenyewe jinsi mwaka 2021 unavyoweza kubadilika kwako. Chukua hatua sasa kwa kufuata maelekezo hayo hapo juu.
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
NB; Zoezi hili unaweza kulifanya wakati wowote unapokuwa tayari, unapohitaji msaada wa kusimamiwa katika kulifanya wasiliana nami kwa wasap namba 0717396253. Karibu.
ThanksRafiki yangu mpendwa,

Karibu sana mkuu.Ubarikiwe sana mh umeniencourage sana
Ndiyo mkuu, nauza kitabu pia na ni kizuri, kina maarifa yanayoweza kumpa mtu ukombozi mkubwa wa kifikra na akapiga hatua kwenye maisha.Kwahio kumbe unauza kitabu! Mi nafikiri haya mambo yanawezekana Ulaya tu. Kuishi kwa ratiba ni ngumu sana bongo
SIKU YA 8 TATHMINI YA JIONI; MALALAMIKO YAMEKUPA NINI?SIKU YA 8 TAFAKARI YA ASUBUHI; MAISHA YAKO WAJIBU WAKO.
Kama unataka kufanikiwa kwenye maisha, basi hatua ya kwanza na muhimu kuchukua ni kubeba jukumu la maisha yako.
Jua kwamba maisha yako ni wajibu wako binafsi.
Usimlaumu wala kumlalamikia yeyote yule kama maisha yako hayapo unavyotaka wewe.
Kama unaweza kusoma hapa, basi jua huna wa kumlalamikia wala kumlaumu.
Hupaswi kuwalalamikia wazazi kwa chochote walichofanya au kutokufanya, walijitahidi kadiri ya uelewa na uwezo wao.
Hupaswi kuilalamikia serikali, yenyewe inategemea ikutoze wewe kodi ndiyo ijiendeshe.
Hupaswi kulalamikia mazingira au hali ya uchumi, kwani katika hayo hayo kuna ambao wanafanya vizuri.
Beba jukumu la maisha yako, fikiri kwa usahihi, chukua hatua sahihi na badili maisha yako.
Chochote unachotaka na hujawa nacho bado, kinachokuzuia ni namna unavyofikiri na namna unavyotenda. Badili hayo na utapata chochote unachokitaka kwenye maisha yako.
Kujifunza zaidi kuhusu kubeba jukumu la maisha yako, fungua hapa; www.bit.ly/somavitabuapp
SIKU YA 9 TATHMINI YA USIKU; WATU AMBAO UMEKUWA UNAWALIPA.SIKU YA 9 TAFAKARI YA ASUBUHI; SIYO KIPATO BALI MATUMIZI.
Kuna wanaingiza kipato kikubwa lakini bado wamekwama kwenye umasikini.
Na kuna wanaoingiza kipato kidogo lakini wameweza kupiga hatua.
Kinachowatofautisha watu kwenye utajiri na umasikini siyo kipato wanachoingiza, bali jinsi wanavyokitumia kipato hicho.
Kama matumizi yanalingana au kuzidi kipato, lazima utabaki kwenye umasikini.
Kama matumizi yako chini ya kipato, una fursa ya kuondoka kwenye umasikini.
Hivyo pamoja na kupambana kuongeza kipato, pambana pia kudhibiti matumizi yake.
Soma zaidi hapa; www.bit.ly/somavitabuapp