utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,813
Lakini kitu cha muhimu ni amani na mshikamano na ufanisi katika kazi. hata kama nchi itaongozwa na waislamu tu au wakristo tu na wana uwezo na wanahakikisha nchi inakuwa salama na inasonga mbele, hapo tatizo la udini au mfumo fulani kukandamiza serikali halipo. shida inapokuwa pale viongozi wa dini fulani wanapochafua viongozi wa serikali kwa vile tu ni wa dini nyingine. hapo ndiyo shida huja.
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anatakiwa awe anastaafu leo kwa mujibu wa sheria. Ametumikia chini ya Kikwete tangu miezi michache tu baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Chini ya uongozi wake wa idara hii nyeti kabisa nchini ambayo haiko chini ya Katibu Mkuu Kiongozi mengi yametokea na kwa kiasi kikubwa mengi ya kufanya watu wakumbuke idara wakiwa na maswali mengi kichwani.
Tunaweza kuanza kuorodhesa mambo ambayo yameonesa ulegevu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika ulinzi wa taifa chini ya uongozi wa Rashid Othman na Zoka (ambaye naye legally amestaafu lakini "bado yupo"). Kuna viongozi kadhaa wa Idara wanaotakiwa kustaafu hivi sasa lakini wote bado "wapo" na kuna dalili kuwa RO anataka Rais amuongezee muda ili wamalize wote 2015.
mkuu acha utani, inamana haya hili hujui?????????? ngoja kigwangalla aje hapa atakwambia anavom attend mgonjwa wake lissu
No, I beg to differ sipo huko mkuu, ila kiukweli taratibu au sheria ziliwekwa ili zifuatwe so kama tunaona hazifai, basi bunge liongeze muda wa kustaafu, meanwhile if you go to equity you must do equity, Jaji mkuu mstaafu samatta alitoa maoni tume ya katba umri wa majaji kustaafu uongezwe, so to say watoe tu pendekezo umri wao wa kustaafu uongeze lakini siyo kuvunja sheria zilizopo kwa kigezo cha uwezo wa kuongoza, hata mbuyu ulianza kama mchicha mkuu
tujenge hoja zinazojenga sio kwa sababu mtu una komputa chumbani kwako basi unaandika tu kile kinachokujia kichwani. nchi inakabiliwa na mambo mengi makubwa yanayopaswa kujadiliwa kwa kina, leo tunaletewa mjadala wa kujadili maisha ya mtu na familia yake....huku ni kutumia vibaya akili na maarifa uliyopewa bure na mungu
Hongera kwasababu unaonyesha your ignorance, ina maana umri wa kustafu uliwekwa ili uwe trampled upon? mtu akisema ukweli siyo lazima awe wa kijiweni mkuu, so take care not to judge a book by its cover, tusifanye vitu kwa kubebana na usiwadharau walopata zero maana mfumo unaoutetea ndo umewapa matokeo hayo tumekengeuka maadili ya kitaifa na tumebaki kushabikia trivial party politics, udhaifu mfumo wa elimu aliuzungumzia Mh. Mbatia wabunge wa magamba walichomfanyia unakielewa, Mungu si Athuman matokeo yamewaumbua sasa wanaleta tume, shame.
Hizi propaganda za wanasiasa hazitatufika mbali, ndiyo yale yale wanafunzi wanafeli halafu wanasiasa wanawafuata na kuwapa pesa ili waandamane, hivi vyombo vya ulinzi tunavyovisakama ni sawa na kuupiga mawe mti wenye matunda. Hawa jamaa wanafanyakazi sana, tazama kila siku tunasikia majambazi wameuawa, majangili wamekamatwa, n,k hayo yote hatuyaoni na kuishia kushabikia wanasiasa ambao malengo yao ni kushika madaraka.
mkuu nadhani umeenda chaka hapo. mie nasema kuwa suala la ufanisi wa mtu halitokani na rika lake. kama mtu ana uwezo haijalishi ni mzee au kijana. tunachotaka ni kuzuia makosa katika kufanya maamuzi. halafu kumbuka uwepo wa hao watu unaowaita wazee haimaanishi kazi haziendi mkuu. hao unaowaita wazee wanafanya kazi kwa ushauri wa vijana ambao wamewazunguka kila kona. kumbuka penye wazee hapahalibiki neno. hata kule kijijini maamuzi mazito na jukumu la kuangalia jamii wamepewa wazee kwa kuamini kuwa kuishi kwao miaka mingi, wamevumilia mengi na wana busara ya kutosha. cha muhimu ni namna gani ninyi vijana mtatumia busara za wazee kufanya maamuzi sahihi
kuhusu hilo la kuvunjwa kwa sheria hapo dnugu umepotea. pitia sheria namba 2 ya 2002 ya utumishi wa umma pamoja na miongozo yake. utajua kuwa kumbe kuna ajira za kudumu na ajira za mkataba. kama mtumishi amestaafu na mwajiri bado anamhitaji, kinachofanyika ni kuwa anastaafu kwa mujibu wa sheria na mwajiri anampa mkataba kwa kadri inavyofaa. kumbuka anayetoa mkataba ni mwajiri. hivyo huwezi kuanza kulialia eti Othman na Zoka wanazuia nafasi za wengine. hayo ni majembe. hata kule kijijini, mara nyingi jembe zuri halitupwi labda unabadilishwa mpini tu. lakini jembe baya hata kama umelinunua leo unaweza kulitupa darini kwa vile halikusaidii.
Unaongea nini wewe?wezi wa EPA,Kagoda,Richmond,Twiga,Pembe za Ndovu,Mwakyembe,Dr nani sijui na uozo mwingine mwingi uko wapi,unakuja kutuletea eti wanakamata majambazi wakati wanakamata vibaka tu.
Think twice mkuu kabla hujatetea hicho chama chako hapa.
UDINI udini utatumaliza sana tu watanzania, kumbe tatizo hapa ni jina na siyo umri tena? kazi ipo! Basi RASHID aondoke aingie PETER SLAA au vipi. Nimesha kuwa bored, hivi tutafika wapi na udini udini huu.
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anatakiwa awe anastaafu leo kwa mujibu wa sheria. Ametumikia chini ya Kikwete tangu miezi michache tu baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Chini ya uongozi wake wa idara hii nyeti kabisa nchini ambayo haiko chini ya Katibu Mkuu Kiongozi mengi yametokea na kwa kiasi kikubwa mengi ya kufanya watu wakumbuke idara wakiwa na maswali mengi kichwani.
Tunaweza kuanza kuorodhesa mambo ambayo yameonesa ulegevu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika ulinzi wa taifa chini ya uongozi wa Rashid Othman na Zoka (ambaye naye legally amestaafu lakini "bado yupo"). Kuna viongozi kadhaa wa Idara wanaotakiwa kustaafu hivi sasa lakini wote bado "wapo" na kuna dalili kuwa RO anataka Rais amuongezee muda ili wamalize wote 2015.
kuwepo kwa hao watu uliowataja haimaanishi hakuna mfumo kristo. hebu ngoja nikuulize na naomba ujibu inavyotakiwa. kama wewe ni mpenzi au mchezaji wa mpira wa miguu, bila shaka unajua kuwa timu yenye wachezaji 11 hucheza kwa mujibu wa formation inayoandaliwa na kocha ambaye ni mmoja tu. je kwa wachezaji wanapokuwa uwanjani wanafuata matakwa yao au maelekezo ya kocha. hata kama watafuata matakwa yao kuna mtu yuko pembeni (kocha) anawaangalia na wakienda kinyume anawarekebisha. ndo maana ya mfumo (formation) kristo. ingawa mmeshikilia nyinyi hizo nafasi lakini mnaongozwa na mamlaka nyingine. fanya utafiti kwa kila idara ya serikali ili kujua idadi ya waislamu na wakristo. matokeo utakayoyafanya ndiyo yatakayokubainisha kuwa kweli kuna kitu kiitwacho MK
umesema kweli mkuu, maandamano yaanzie ofisi za chadema makao makuu tumtoe slaa kwani amezeeka sana lakini bado wamo tu, kisha tumtoe na mbowe maana amekaakwenye uenyekiti yapata miongo kadhaa sasa......tukimaliza hapo tunaingia mawizarani sasa, mbona patamu apoooooooooooooo
wanaolalamika ni wale ambao watoto wao, ndugu zao na jamaa zao wamefanya vibaya katika matokeo hayo[/COLOR], wale ambao watoto wao wamefanya vizuri wamefurahi sana na kuipongeza serikali tena tunao mitaani wanasema wazi kuwa watoto wa jirani zao walikuwa wavuta bangi, watumia simu za mikononi hovyo na vitu kama hivyo. Hivi mtaala hata ukiwa mzuri vipi utamzuia mtoto kuvuta bangi?