Farewell RO....

Farewell RO....

Status
Not open for further replies.
tujenge hoja zinazojenga sio kwa sababu mtu una komputa chumbani kwako basi unaandika tu kile kinachokujia kichwani. nchi inakabiliwa na mambo mengi makubwa yanayopaswa kujadiliwa kwa kina, leo tunaletewa mjadala wa kujadili maisha ya mtu na familia yake....huku ni kutumia vibaya akili na maarifa uliyopewa bure na mungu
 
Lakini kitu cha muhimu ni amani na mshikamano na ufanisi katika kazi. hata kama nchi itaongozwa na waislamu tu au wakristo tu na wana uwezo na wanahakikisha nchi inakuwa salama na inasonga mbele, hapo tatizo la udini au mfumo fulani kukandamiza serikali halipo. shida inapokuwa pale viongozi wa dini fulani wanapochafua viongozi wa serikali kwa vile tu ni wa dini nyingine. hapo ndiyo shida huja.

Hivi kweli tukianza kutafuta idara zote za serikali mbali na hiyo idara ya usalama wa Taifa hatuwzi kupata watumishi wa serikali waliostaafu na bado wanafanyakazi kwa mkataba? Hivi wanasiasa watakaa wapi wajisafishe kuwa vyama vyao havina udini? iweje kila hoja inayoletwa humu JF lazima iongelee kwa sababu mtu fulani ni dini fulani? siyo udini huu kweli. Nimeona post moja inasema,eti jina lenyewe RASHID, jamani tunakwenda wapi?
 
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anatakiwa awe anastaafu leo kwa mujibu wa sheria. Ametumikia chini ya Kikwete tangu miezi michache tu baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Chini ya uongozi wake wa idara hii nyeti kabisa nchini ambayo haiko chini ya Katibu Mkuu Kiongozi mengi yametokea na kwa kiasi kikubwa mengi ya kufanya watu wakumbuke idara wakiwa na maswali mengi kichwani.

Tunaweza kuanza kuorodhesa mambo ambayo yameonesa ulegevu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika ulinzi wa taifa chini ya uongozi wa Rashid Othman na Zoka (ambaye naye legally amestaafu lakini "bado yupo"). Kuna viongozi kadhaa wa Idara wanaotakiwa kustaafu hivi sasa lakini wote bado "wapo" na kuna dalili kuwa RO anataka Rais amuongezee muda ili wamalize wote 2015.

hata kama wakiamua kustaafu leo, hiki chombo kipo imara na kitazidi kuwa imara, wenye wivu wajinyonge.
 
mkuu acha utani, inamana haya hili hujui?????????? ngoja kigwangalla aje hapa atakwambia anavom attend mgonjwa wake lissu

Maradhi gani yanamsumbua jamaa yetu, inamaana mjengoni safari hii kutakuwa kustaarabu?
 
No, I beg to differ sipo huko mkuu, ila kiukweli taratibu au sheria ziliwekwa ili zifuatwe so kama tunaona hazifai, basi bunge liongeze muda wa kustaafu, meanwhile if you go to equity you must do equity, Jaji mkuu mstaafu samatta alitoa maoni tume ya katba umri wa majaji kustaafu uongezwe, so to say watoe tu pendekezo umri wao wa kustaafu uongeze lakini siyo kuvunja sheria zilizopo kwa kigezo cha uwezo wa kuongoza, hata mbuyu ulianza kama mchicha mkuu

mkuu nadhani umeenda chaka hapo. mie nasema kuwa suala la ufanisi wa mtu halitokani na rika lake. kama mtu ana uwezo haijalishi ni mzee au kijana. tunachotaka ni kuzuia makosa katika kufanya maamuzi. halafu kumbuka uwepo wa hao watu unaowaita wazee haimaanishi kazi haziendi mkuu. hao unaowaita wazee wanafanya kazi kwa ushauri wa vijana ambao wamewazunguka kila kona. kumbuka penye wazee hapahalibiki neno. hata kule kijijini maamuzi mazito na jukumu la kuangalia jamii wamepewa wazee kwa kuamini kuwa kuishi kwao miaka mingi, wamevumilia mengi na wana busara ya kutosha. cha muhimu ni namna gani ninyi vijana mtatumia busara za wazee kufanya maamuzi sahihi

kuhusu hilo la kuvunjwa kwa sheria hapo dnugu umepotea. pitia sheria namba 2 ya 2002 ya utumishi wa umma pamoja na miongozo yake. utajua kuwa kumbe kuna ajira za kudumu na ajira za mkataba. kama mtumishi amestaafu na mwajiri bado anamhitaji, kinachofanyika ni kuwa anastaafu kwa mujibu wa sheria na mwajiri anampa mkataba kwa kadri inavyofaa. kumbuka anayetoa mkataba ni mwajiri. hivyo huwezi kuanza kulialia eti Othman na Zoka wanazuia nafasi za wengine. hayo ni majembe. hata kule kijijini, mara nyingi jembe zuri halitupwi labda unabadilishwa mpini tu. lakini jembe baya hata kama umelinunua leo unaweza kulitupa darini kwa vile halikusaidii.
 
tujenge hoja zinazojenga sio kwa sababu mtu una komputa chumbani kwako basi unaandika tu kile kinachokujia kichwani. nchi inakabiliwa na mambo mengi makubwa yanayopaswa kujadiliwa kwa kina, leo tunaletewa mjadala wa kujadili maisha ya mtu na familia yake....huku ni kutumia vibaya akili na maarifa uliyopewa bure na mungu

Mkuu, umesema vyema, lakini humu JF hairuhusiwi kujadili maisha binafsi ya mtu mmoja tu naye ni Mzee wetu WILBROAD PETER SLAA, huyu ukimgusa tu burn.
 
Mwanakijiji hoja yako nimeipenda. Baadh ya wachangiaji wanashindwa kutofautisha mwanasiasa na mtumishi wa umma. Mimi napendekeza sasa ni wakati muhimu mwanakijiji na raia wema kutengeneza dossier inayoonyesha wafanyakazi wote ambao muda wa kustaafu umefika,wamepewa mikataba au wameforge umri ili washugulikiwe na wananchi, human right activist na asasi mbalimbali. Inabid maandamano yafanyike kwenda kila wizara wanayojua hawa watu wameshikilia nafasi nyeti na hawatak kuachia.kuhusu RO, yeye kama kweli muda umeisha apishe. Kipind cha nyerere na mwinyi kila mwananchi,alipenda ajiite mlinzi wa nchi yake.kwa sasa ikionekana umepeleka taarifa muhim kwa tiss,pccb,uamiaji,polisi. Wewe ndiye unakuwa adui. Maadili katika idara hizi hakuna. Mwakyembe anasema madin ya rwanda yalibadilishwa bandalin dar huku polisi,tiss wakiwa wausika wakuu. Idara hizi zote zina kuzi-reassemble na waliotimiza muda wakustaafu wapishe
 
Hongera kwasababu unaonyesha your ignorance, ina maana umri wa kustafu uliwekwa ili uwe trampled upon? mtu akisema ukweli siyo lazima awe wa kijiweni mkuu, so take care not to judge a book by its cover, tusifanye vitu kwa kubebana na usiwadharau walopata zero maana mfumo unaoutetea ndo umewapa matokeo hayo tumekengeuka maadili ya kitaifa na tumebaki kushabikia trivial party politics, udhaifu mfumo wa elimu aliuzungumzia Mh. Mbatia wabunge wa magamba walichomfanyia unakielewa, Mungu si Athuman matokeo yamewaumbua sasa wanaleta tume, shame.

sijamdharau mtu hata mmoja mana hata mimi nina wadogo zangu wamefeli, lakini sababu za msingi zinajulikana, mojawapo ni watoto kutumia mitandao ya kijamii hususan FACEBOOK kutafuta wapenzi na wachumba, kuangalia picha za ngono na lmambo yanayofanana na hayo.......... sheria zinafuatwa ndio mana hao unaotaka wastaafu waliingia kwa sheria na wataondoka kwa sheria....................asante kwa kutambua ignorance yangu kwani ndio sifa ya kibinadam, ila wewe usitumike, ni hatari kwa afya yako na famili na taifa kwa ujumla. be free in ur thinking
 
Hizi propaganda za wanasiasa hazitatufika mbali, ndiyo yale yale wanafunzi wanafeli halafu wanasiasa wanawafuata na kuwapa pesa ili waandamane, hivi vyombo vya ulinzi tunavyovisakama ni sawa na kuupiga mawe mti wenye matunda. Hawa jamaa wanafanyakazi sana, tazama kila siku tunasikia majambazi wameuawa, majangili wamekamatwa, n,k hayo yote hatuyaoni na kuishia kushabikia wanasiasa ambao malengo yao ni kushika madaraka.

Unaongea nini wewe?wezi wa EPA,Kagoda,Richmond,Twiga,Pembe za Ndovu,Mwakyembe,Dr nani sijui na uozo mwingine mwingi uko wapi,unakuja kutuletea eti wanakamata majambazi wakati wanakamata vibaka tu.
Think twice mkuu kabla hujatetea hicho chama chako hapa.
 
mkuu nadhani umeenda chaka hapo. mie nasema kuwa suala la ufanisi wa mtu halitokani na rika lake. kama mtu ana uwezo haijalishi ni mzee au kijana. tunachotaka ni kuzuia makosa katika kufanya maamuzi. halafu kumbuka uwepo wa hao watu unaowaita wazee haimaanishi kazi haziendi mkuu. hao unaowaita wazee wanafanya kazi kwa ushauri wa vijana ambao wamewazunguka kila kona. kumbuka penye wazee hapahalibiki neno. hata kule kijijini maamuzi mazito na jukumu la kuangalia jamii wamepewa wazee kwa kuamini kuwa kuishi kwao miaka mingi, wamevumilia mengi na wana busara ya kutosha. cha muhimu ni namna gani ninyi vijana mtatumia busara za wazee kufanya maamuzi sahihi

kuhusu hilo la kuvunjwa kwa sheria hapo dnugu umepotea. pitia sheria namba 2 ya 2002 ya utumishi wa umma pamoja na miongozo yake. utajua kuwa kumbe kuna ajira za kudumu na ajira za mkataba. kama mtumishi amestaafu na mwajiri bado anamhitaji, kinachofanyika ni kuwa anastaafu kwa mujibu wa sheria na mwajiri anampa mkataba kwa kadri inavyofaa. kumbuka anayetoa mkataba ni mwajiri. hivyo huwezi kuanza kulialia eti Othman na Zoka wanazuia nafasi za wengine. hayo ni majembe. hata kule kijijini, mara nyingi jembe zuri halitupwi labda unabadilishwa mpini tu. lakini jembe baya hata kama umelinunua leo unaweza kulitupa darini kwa vile halikusaidii.

Nadhani watu kama ninyi mnahitajika ili muwe mnatufafanulia masuala ya msingi kama haya hasa pale ambapo tunataka kupotoshwa kwa sababu tu hatujui na hivyo tunabakia kuona serikali yetu haifai kumbe sivyo. Ila pamoja na kutojua bado mleta mada alini-bore pale alipo tajamajina ya watu wanaotakiwa kustaafu na kuongeza kuwa na wengine wengi, sasa nikajiuliza huyu jamaa interest yake katika hili ni nini? nikaanza kujiuliza naye anafanyakazi huko idara ya usalama wa taifa na anaona amezibiwa riziki au basi tu.
 
Unaongea nini wewe?wezi wa EPA,Kagoda,Richmond,Twiga,Pembe za Ndovu,Mwakyembe,Dr nani sijui na uozo mwingine mwingi uko wapi,unakuja kutuletea eti wanakamata majambazi wakati wanakamata vibaka tu.
Think twice mkuu kabla hujatetea hicho chama chako hapa.

taratibu mkuu, hasira haijengi, hata ruzuku ya chama pia imeliwa na inazidi kuliwa, wakihoji wanatimuliwa
 
UDINI udini utatumaliza sana tu watanzania, kumbe tatizo hapa ni jina na siyo umri tena? kazi ipo! Basi RASHID aondoke aingie PETER SLAA au vipi. Nimesha kuwa bored, hivi tutafika wapi na udini udini huu.

Mbona CAG alionezewa mda lakini watu hawasemi.
 
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anatakiwa awe anastaafu leo kwa mujibu wa sheria. Ametumikia chini ya Kikwete tangu miezi michache tu baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Chini ya uongozi wake wa idara hii nyeti kabisa nchini ambayo haiko chini ya Katibu Mkuu Kiongozi mengi yametokea na kwa kiasi kikubwa mengi ya kufanya watu wakumbuke idara wakiwa na maswali mengi kichwani.

Tunaweza kuanza kuorodhesa mambo ambayo yameonesa ulegevu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika ulinzi wa taifa chini ya uongozi wa Rashid Othman na Zoka (ambaye naye legally amestaafu lakini "bado yupo"). Kuna viongozi kadhaa wa Idara wanaotakiwa kustaafu hivi sasa lakini wote bado "wapo" na kuna dalili kuwa RO anataka Rais amuongezee muda ili wamalize wote 2015.

hiki chombo hakitabomoka kirahisi kama mnavodhani mkuu mwanakjj.........na wala hakitayumba, due to its proffessionalism........ajenda zenu za kisiasa hazitafanikiwa...........jaribu tena baadae.
 
kuwepo kwa hao watu uliowataja haimaanishi hakuna mfumo kristo. hebu ngoja nikuulize na naomba ujibu inavyotakiwa. kama wewe ni mpenzi au mchezaji wa mpira wa miguu, bila shaka unajua kuwa timu yenye wachezaji 11 hucheza kwa mujibu wa formation inayoandaliwa na kocha ambaye ni mmoja tu. je kwa wachezaji wanapokuwa uwanjani wanafuata matakwa yao au maelekezo ya kocha. hata kama watafuata matakwa yao kuna mtu yuko pembeni (kocha) anawaangalia na wakienda kinyume anawarekebisha. ndo maana ya mfumo (formation) kristo. ingawa mmeshikilia nyinyi hizo nafasi lakini mnaongozwa na mamlaka nyingine. fanya utafiti kwa kila idara ya serikali ili kujua idadi ya waislamu na wakristo. matokeo utakayoyafanya ndiyo yatakayokubainisha kuwa kweli kuna kitu kiitwacho MK

Umewahi kusikia msemo wa kiswahili kuwa WINGI SI HOJA? Mnaweza kuwa wengi kwenye taasisi; if you do not have the power, you are castrated!! It is he who has the power that will influence the direction to be followed na ndio maana Kikwete cannot hide from his involvement in tearing this nation asunder on religious lines; kwenye huo mfano wako Kikwete ndio Kocha na wote wanacheza kufuatana na formation yake kwani yeye ndiye anayepanga timu kufuatana na itikadi ya vipedo.
 
umesema kweli mkuu, maandamano yaanzie ofisi za chadema makao makuu tumtoe slaa kwani amezeeka sana lakini bado wamo tu, kisha tumtoe na mbowe maana amekaakwenye uenyekiti yapata miongo kadhaa sasa......tukimaliza hapo tunaingia mawizarani sasa, mbona patamu apoooooooooooooo

Jicho langu la tatu linaona mbali sana. Sasa tuendako siko, Sidhani kuna sababu yoyote ya kujibu post kama hii ya KAJUNGU. Mikataba hiyo inayosemwa kwenye ajira ipo kisheria na imepitishwa bungeni, lakini kwa sababu Wabunge wetu hao hao ndiyo wanaotunga sheria na ndo hao hao wanaokuja kunadamana kuwa sheria zimevunjwa wanaweza kufanya hivyo.
 
wanaolalamika ni wale ambao watoto wao, ndugu zao na jamaa zao wamefanya vibaya katika matokeo hayo[/COLOR], wale ambao watoto wao wamefanya vizuri wamefurahi sana na kuipongeza serikali tena tunao mitaani wanasema wazi kuwa watoto wa jirani zao walikuwa wavuta bangi, watumia simu za mikononi hovyo na vitu kama hivyo. Hivi mtaala hata ukiwa mzuri vipi utamzuia mtoto kuvuta bangi?

Kwanza to put the records straight sina ndugu aliyefanya mtihani wa form 4 mwaka ulopita, na je mkuu wa Green Acres aliyelalamikia wanafunzi wa shule yake walowekewa maksi kwenye masomo ambayo hawakufanya na walofaulu bila kufanya mtihani unawaongeleaje? kinachoniuma ni number of failures tunaongeza mtaani kila uchao, niliposema mfumo ndo umewafelisha watoto hao nilikuwa na maana yangu, km una kumbukumbu nzuri serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mh. Lowassa ndo walioanzisha shule za kata na walikuwa na kusudi zuri, lakini shule hizi zilisahaulika baada ya kuingia Mh. Pinda aliyekuja na sera ya kilimo kwanza, so to say shule za kata zingekuwa well furnished kwenye walimu ambao wapo well paid, maabara, maktaba, vitabu vya kiada na ziada hzo zero zingepungua na watoto hao waloelimika wangeendesha kilimo cha kisomi zaidi, vilevile imefika kipindi shule zetu zote wafundishe vocational skills ambazo zingewasaidia hata hao walopata zero kupata kitu cha kujikimu, kuliko sasa ambapo hawajielewi maana hawana mbinu mbadala wa kujikimu, hence kwa hali hii tutazalisha vibaka na machangudoa wengi coz hata wakiingia umachinga na mama ntilie mgambo hawatawaacha salama.
 
kuna baadhi ya waandishi, wachangiaji hapa JF wenye majina makubwa wanazidi kuporomoka umaarufu wao kutokana na kuleta mada za chuki, fitna, majungu na zinaoonyesha hasira ama kukosa kitu flani hivi kama madaraka au mali... hii haitatufikisha mbali kama taifa.
 
tujenge hoja zinazojenga sio kwa sababu mtu una komputa chumbani kwako basi unaandika tu kile kinachokujia kichwani. nchi inakabiliwa na mambo mengi makubwa yanayopaswa kujadiliwa kwa kina, leo tunaletewa mjadala wa kujadili maisha ya mtu na familia yake....huku ni kutumia vibaya akili na maarifa uliyopewa bure na mungu

Mbona unaonekana sana kuguswa na hii hoja ya MM,Please whats so apecial abt this thread kamanda
 
Hongera kwasababu unaonyesha your ignorance, ina maana umri wa kustafu uliwekwa ili uwe trampled upon? mtu akisema ukweli siyo lazima awe wa kijiweni mkuu, so take care not to judge a book by its cover, tusifanye vitu kwa kubebana na usiwadharau walopata zero maana mfumo unaoutetea ndo umewapa matokeo hayo tumekengeuka maadili ya kitaifa na tumebaki kushabikia trivial party politics, udhaifu mfumo wa elimu aliuzungumzia Mh. Mbatia wabunge wa magamba walichomfanyia unakielewa, Mungu si Athuman matokeo yamewaumbua sasa wanaleta tume, shame.

Mbatia hapo alipo amefika kwa sababu ya huruma ya magamba, vinginevyo angekua anagmbania ruzuku na viongozi wenzake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom