Farewell RO....

Status
Not open for further replies.
wanatokea kanda gani hao mkuu??????? Mana kaskazini tayari imezinduliwa.

NAKEMEAUDINI Nilichomanisha ni kuwa Baregu au Rwaitama si waislam, kama alivyo Rashid Othman. Hivyo correlation ya RO na mamlaka ya uteuzi (JK) ni kubwa kuliko ilivyo ya Baregu na Rwaitama! Basis ya arguement yangu ni kutokana na complaints ambazo zimewahi kujitokeza mara nyingi hapa kuwa mamlaka ya uteuzi inatoa "upendeleo" kwa religious affiliates wake!!
 
Last edited by a moderator:
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anatakiwa awe anastaafu leo kwa mujibu wa sheria. Ametumikia chini ya Kikwete tangu miezi michache tu baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani.
Tusubiri uteuzi wa 'mwenzetu' mwingine!
 
kinachotakiwa si kijana bali ni uwezo wa mtu katika kuongoza na kufanya maamuzi yasiyo na shaka na ambayo hayatawaumiza walio wengi. kama mnajidanganya kuwa atateuliwa huyo mnayemuita kijana ili mumyumbishe hapo mmedanganyika


Sheria za kazi kweli zinasema pale mwajiri anapoona inafaa anaweza kumpa mkataba wa kazi yule aliyefikisha muda wa kustaafu. Sawa, lakini serikali ya baba MwanaAsha sio consistent katika hili kwani mikataba huwa wanapewa watu wa majina na itikadi anayohusiana nayo na hapo ndipo malalamikao yanapoanzia kuwa jamaa bado anakoleza itikadi ya vipedo!! He is not consistent in his decision making.
 
Japhet Mosi, naona na wewe ni miongoni mwa wale wanaoona kuwa othman ni kikwazo. kumbe hata hili la kushinikiza astaafu nimebaini ni kutokana na jitihada zenu za kumshinikiza ajiuzulu kwa sababu zenu za kisiasa kushjindikana. na mara zote huwa nasema ukitaka kuwa mtu mzuri jaribu pia kusikiliza maoni ya wale usiowapenda. kwa kushinikiza mimi nifungiwe ni wazi kuwa una huo ugonjwa. na kama mnataka muongoze nchi kwa staili ya kusikia maneno yanayowafurahisha tu ni wazi kuwa mtalipeleka taifa pabaya. ndiyo maana watanzania wamebainio hivyo na huyo Dr Slaa wenu mnayempenda anaendelea kuporomoka kiwango chake cha kupendwa na mpaka 2015 ndo atakuwa amepotea kabisa kwenye ulimwenu wa siasa tanzania. halafu unaafikiri wale jamaa wa mlimani watamruhusu agombee tena? wapi. jamaa wamejipanga kweli.
 

ndio kigezo kilichotumika hadi baregu akateuliwa na padre slaa na aikaeli mbowe kuwa mshauri wao???? mana huko ndio kuna hivyo vigezo............

katika serikali na vyombo vya dola kabla mtu hajateuliwa kuwa mkuu wa idara au kitengo flani, huwa wanakaa wakuu wa idara mbalimbali zilizo chini ya taasisi hiyo mfano, katika idara ya polisi wanaangalia ma RPC, Wakuu wa idara makao makuu, makamishna na majenerali. wanajadiliwa na idara husika yanabaki majina matatu ndio yanapelekwa kwa mamlaka ya uteuzi ambayo ni rais wa nchi. so siamini kwamba hivyo vigezo vya LAANA VILITUMIKA NA KWA HAKIKA NAKEMEA UDINI KWA NGUVU ZANGU NA AKILI ZANGU NA UWEZO WANGU WOTE NASEMA UDINI NA MDINI MSHINDWE NA MLEGEE..............
 

CAG ie mkaguzi na mthibiti wa hesabu za serikali ni mkristo anaitwa LUDOVICK UTOUH!!!!!!!!!!!!!! ALIONGEZEWA MUDA WA MKATABA...HAPO UNASEMAJE??????????? ACHENI UJUHA KWA KUCHOCHEA CHUKI ZA KIDINI..MNALIANGAMIZA TAIFA
 

ahaaa, kumbe kwa kadri mnavyochangia mnazidi kufunguka na kutoa yenu ya moyoni. kumbe sababu si umri wa kustaafu. kumbe ni kwa sababu ni muislamu? haya kama ni kwa kesi hiyo naomba nitajie orodha ya wakurugenzi wa Idara toka inaanzishwa hadi leo. Halafu utaniambia waislamu walikuwa wangapi na wakristo wangapi. au kama unajifanya wewe unaijua sana idara nitajie orodha ya waislamu walioongezewa mikataba na wakristo walionyimwa mikataba. siku zote tunasema watu wakiongozwa na fikra za kidini wataipeleka nchi pabaya maana watakuwa na mawazo mpindo kuegemea dini waitakayo.

kinachoendelea sasa katika nchi hii ni mazoea yaliyojengeka miongoni mwa watanzania wapumbavu kuwa wakristo tu ndiyo wenye mamlaka ya kutawala na pale anapotawala mtu wa dini nyingine wanajaribu kila hali kumchafua. huo ni ujinga kwani tanzania ni ya kila mtu na baba wa taifa mwalimu Julius nyerere aliweka misingi imara ndo maana hadi leo hii tunaishi kwa amani na utulivu. na hicho chama chenu cha kidini, chadema mtatupeleka pabaya
 
Hawa watoto wetu ukiwakuta jioni baada ya masomo wanavyoponda maisha as if kila kitu tayari kumbe ndo kwanza wanarudi nyumbani kutoka shule. Wapo ambao hata makwao wanajulikana kua usiku wanatorokaga na wanarudi asubui lakini wakifeli tunakimbilia kusema kua fulani ajiuzuru. Tatizo kubwa tulilobalo tunaangalia solution za kisiasa(tulipoangukia kuliko tulikojikwaa).
 
Kwa jicho la kawaida siyo rahisi kuuona utendaji hasa wa hii idara.Unahitaji 'jicho la tatu' kuona nini kinaendelea. Kwa utendaji wa kawaida kama taasisi uko sawa kwani wakusanya taarifa,wachambuzi,n.k wanafanya kazi zao kama kawaida. Lakini pia ieleweke si kila pendekezo lenye 'mantiki' lazima litekelezwe 'to the dot'..
Tatizo kubwa sasa hivi ni siasa (hasa ya vyama) kupewa kipaumbele zaidi ya nyanja nyingine zote kama usalama wa raia, uchumi wa nchi,uhamiaji,ulinzi ajira za Watanzania n.k
RO kama 'spymaster' anaweza asiwe na tatizo lakini matakwa ya 'system' yanaweza kumfanya kisionekane afanyacho.
 
NAKEMEAUDINI umesahau kutaja kwa jina la....maana kwa nguvu zako wewe kama mwana wa Adam sidhani kama utaweza kutokomeza udini. Mimi nasema, kwa Jina lililo kuu kuliko yote la Yesu Kristo na kwa nguvu za yeye aniwezeshaye katika kila jambo, washindwe wote wanaotangaza udini. Amina.
 
Last edited by a moderator:

mkuu, unavyojadili suala la usalama wa taifa ni vyema ukajikita huko. ulipaswa kufahamu kwenye idara ya usalama uteuzi unafanyika vipi. kumbuka hivi ni vyombo viwili tofauti na havifanani katika muundo wake na utendani wake
 

Kuna haja ya kuwa na Mashaka na uwezo wa huyu mkuu wa shule ya sekondari GREEN ACRES na kuichunguza hii shule, inawezakana kabisa kuna fojari zinafanyika ambazo aidha mkuu wa shule hazijui hasa wakati wa ujazaji wa fomu za CA(continous assessement) au mkuu wa shule huwa hana kumbukumbu sahihi ya idadi ya wanafunzi wake, Lakini pia itambulike kuwa waraka mpya wa wizara ya elimu unamkataza mkuu wa shule kumfukuza mwanafunzi hasa anapokuwa amekwishajisajili kufanya mtihani wa taifa,sasa kama aliwafukuza wanafunzi wake tayari wakiwa wamekiwishajisajili kufanya mtihani wa kidato cha nne basi hao walikuwa ni watahiniwa halali na anapaswa kutueleza watanzania ni katika mazningira gani walifanya mtihani. Kuhusu shule kufundisha vocation skills, sijui unachukua wapi reference, inawezekana kabisa hujui nini maana ya skills. Elewa kuwa hata yule mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza, bado hana skills za kufanyakazi na ndiyo maana wanakwenda kidato cha tanona vyuo na huu unakuwa ni mchakato wa kuelekea kupata skills ambazo unaziongelea hapa bila hata kujua maana yake. Labda utahoji kwa nini wanafunzi wa zamani walikuwa wakimaliza kidato cha nne na kupata kazi huku ukifikiri elimu waliokuwa wakiipata ni tofauti na hii ya sasa, la hasha.
Kutoakana na uhaba wa wataalamu kipindi hicho ndiyo sababu kidato cha nne walichukuliwa maeneo ya kazi siyo kwamba walikuwa na ujuzi(skills) bali walipewa mafunzo wakiwa huko huko makazini, na kwa taariafa yako ndiyo maana kuna kipengele cha uzoefu kazini hivi sasa wakati nafasi mbalimbali zinatangazwa, jambo ambalo si sahihi kwa vile hivi sasa wanahitimu wanahitimu vyuo tayari wakiwa na ujuzi(skills)

Kwa kifupi ni kwamba hakuna kipindi ambacho mwanafunzi alihitimu kidato cha nne akiwa tayari amepata ujuzi, uliza hata babu yako kama alipata nafasi ya kupiga umande.
 
CAG ie mkaguzi na mthibiti wa hesabu za serikali ni mkristo anaitwa LUDOVICK UTOUH!!!!!!!!!!!!!! ALIONGEZEWA MUDA WA MKATABA...HAPO UNASEMAJE??????????? ACHENI UJUHA KWA KUCHOCHEA CHUKI ZA KIDINI..MNALIANGAMIZA TAIFA


Asingechakachua ile ripoti ya ufisadi wa Jairo, CAG asingeongezewa muda!! Alimlinda mshirika wa baba MwanaAsha at the expense of his professional integrity hivyo akazawadiwa contract; which is corruption from the highest levels!!
 

mkuu, inavyoonekana hata majukumu ya idara ya usalama huyajui. hayo uliyoeleza ni matukio na ni jukumu la jeshi kutolea ufafanuzi. jukumu la ulinzi wa raia na mali zao lipo chini ya jeshi la polisi. jukumu la kulinda mipaka ni la jeshi la wananchi. hivyo kama kuna mtu kamwagiwa tindikali, kung'olewa meno kwa koleo au mapadri kuuawa zanzibar ni jukumu la jeshi la polisi kufanya upelelezi na kutolea taarifa. wao wameajiriwa kwa kazi hiyo, na wanamepata mafunzo ya kutosha juu ya masuala hayo na wana kitengo maalum cha upelelezi. kama hujui majukumu ya Idara ya UsaLAMA wa taifa ni bora kukaa kimya kuliko kuropoka
 

Rashid Othman anatakiwa kustaafu lini kwa mujibu wa sheria?
 
wataje hao. na wewe mwenyewe umo nini? naona umejishtukia. usisahau katika hiyo orodha na huyo mwanakijiji
unaona....nilisema ni rahisi kuwatambua! wa kwanza wewe umejileta...nasubiri next person!
 
Asingechakachua ile ripoti ya ufisadi wa Jairo, CAG asingeongezewa muda!! Alimlinda mshirika wa baba MwanaAsha at the expense of his professional integrity hivyo akazawadiwa contract; which is corruption from the highest levels!!

comment zako zinaku difine uwezo wako wa kiakili kwa maana unaongea usiyoyajua wala kuyafanyia utafiti...kumbuka hapa jf wanapita watu wenye akili na uwezo wa kupambanua mambo than u can imagine
 
Msitake nicheke bure hapa! Kwani hapa Tz kuna usalama wa Taifa au usalama wa Viongozi?

Maneno yote haya ni kwa sababu, nchi yetu ni salama, tungekuwa kama huko CONGO, SOMALIA sidhani kama tungekuwa tunavikebehi vyombo vyetu vya ulinzi kiasi hiki.
 
Hivi, unafikiri kweli kuwa hilo dege liliingia nchini bila kibali cha wizara ya ulinzi au Kikwete? They knew about it.
vijana walipokagua wakaonyeshwa pasi za kusafiria za kidiplomasia za Qatar
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…