Kwanza to put the records straight sina ndugu ayelifanya mtihani wa form 4 mwaka ulopita, na je mkuu wa Green Acres aliyelalamikia wanafunzi wa shule yake walowekewa maksi kwenye masomo ambayo hawakufanya na walofaulu bila kufanya mtihani unawaongeleaje? kinachoniuma ni number of failures tunaongeza mtaani kila uchao, niliposema mfumo ndo umewafelisha watoto hao nilikuwa na maana yangu, km una kumbukumbu nzuri serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mh. Lowassa ndo walioanzisha shule za kata na walikuwa na kusudi zuri, lakini shule hizi zilisahaulika baada ya kuingia Mh. Pinda aliyekuja na sera ya kilimo kwanza, so to say shule za kata zingekuwa well furnished kwenye walimu ambao wapo well paid, maabara, maktaba, vitabu vya kiada na ziada hzo zero zingepungua na watoto hao waloelimika wangeendesha kilimo cha kisomi zaidi, vilevile imefika kipindi shule zetu zote wafundishe vocational skills ambazo zingewasaidia hata hao walopata zero kupata kitu cha kujikimu, kuliko sasa ambapo hawajielewi maana hawana mbinu mbadala wa kujikimu, hence kwa hali hii tutazalisha vibaka na machangudoa wengi coz hata wakiingia umachinga na mama ntilie mgambo hawatawaacha salama.