Farhan Jr kauliza kwanini elimu ya sasa imepungua mvuto? Majibu aliyo pewa, wanaosomesha English Mediums hawatayafurahia👇

Farhan Jr kauliza kwanini elimu ya sasa imepungua mvuto? Majibu aliyo pewa, wanaosomesha English Mediums hawatayafurahia👇

Mwingine huyu hapa 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20240110-135559.png
    Screenshot_20240110-135559.png
    57.7 KB · Views: 2
Elimu imepoteza mvuto lakini haijapoteza quality. Quality ya elimu imeongezeka.
Zamani mzee ana phd lakini movie ikiisha kwenye deck anapiga kelele Kobello!! kisa nikabadilishe VCR, yaani amekulia kijijini hata kujifunza kuplay VCR hataki hata kufikiria. Hayo ni matokeo uya elimu duni.

Sema watu wengi wana elimu siku hizi hata ukimuona mwanamke anaendesha gari hushangai, wakati ilikuwa ni nadra sana.
Kweli wewe ni kobello. Unajua kilichoulizwa hapa? Yaani kuendesha gari au kutumia chombo cha muziki kuna uhusiano na elimu ya darasani?
 
Haijapoteza mvuto ila supply imekuwa kubwa na demand ni ndogo haswa kweny ajira.

Binafsi enzi zile nilikuwa nakaa karibu na makanisa ,basi matokeo yakitoka siku tunaenda kuangalia ya darasa la saba kwa halmashauri ni kimbembe kwanza unakuta watu wamezimia ,wengine wana furaha .

Baada ya kama siku mbili tu mtaani panakuwa kama na sherehe ,tents zimefungwa kila kona watu wanafanya sherehe ...Hayo makanisa karibu ya nyumba yetu walikuwa wanafanya kama sherehe sasa usiombe uwe umfeli na kesi za watu kujinyonga zilikuwa kibao, unakuta shule mpo kama 90 ila wanafaulu watu hata nusu hawafiki hiyo ni kwenda form one pekee.....Ila sasa kawaida sana kwa vile demand ni kubwa.

Ukishafaulu habari zinazagaa kwa vile kuna majini ,basi ile ukipita mtaani unapewa hongera😅😅😅unajiona msomi.
 
Maoni yangu kama Likud.

Likud anapokuwa anawaambia hapa jukwaani nyinyi wazazi mnao jinyima ili watoto wenu wapate " elimu bora" kwenye shule za kiingereza muwe mnatambua kwamba lengo langu ni kuwasaidieni ninyi na vizazi vyenu. Hakuna elimu bora yoyote inayo tolewa kwenye hizo mnazo ziita shule za English Mediums.

KWA SABABU 👇
Elimu bora ina sifa kuu tatu kama ifuatavyo👇

1. It helps you to acquire power.

2. It helps you to maintain power.

3. It helps you to protect power.

Elimu yoyote ambayo haikusaidii ku acquire power haina hadhi ya kuitwa elimu bora na wala hutakiwi kulipa mamilioni kuipata.

Kwa bahati mbaya sana hakuna shule yoyote ya English Medium Afrika yenye uwezo wa kutoa elimu yenye vigezo tajwa hapo juu. In fact hata duniani kwa ujumla zipo shule chache sana zenye uwezo huo.

English Medium ni Kayumba zilizo changamka. Mtoto anaenda kukua tu na kujifunza kusoma kuandika na kuhesabu.


Kuliko kujistress kupoteza mamilioni yako kumpeleka English Medium kwanini usimpeleke Kayumba halafu umsimamie kwa ukaribu? Okoa hizo pesa kwa ku invest kwenye mambo mengine na vitabu plus programmes za kumfanya mtoto wako aanze kupata maarifa mapana from his tender age.

Don't stress urself mkuu life is not that hard bro.
 
Mfumo wa maisha ya zamani elimu ndio ilikuwa mkombozi wa maisha tofauti na sasa elimu imekuwa ina asilimia chache kwenye maisha ya mtaani .
Zamani wazazi waliuza mifugo na viwanja ili watoto wasome, sasa hivi mzazi bora mtoto asisome ila kiwanja kibaki, yaani mzazi anampa mtoto mifugo na kiwanja sio elimu kwakuwa imekuwa haina msaada sana mtaani
 
Kweli wewe ni kobello. Unajua kilichoulizwa hapa? Yaani kuendesha gari au kutumia chombo cha muziki kuna uhusiano na elimu ya darasani?
Kuna uhusiano mkubwa sana, tena sana kaa ujiulize usikurupuke.
Binadamu aliyeelimika vizuri yupo more exposed kuliko binadamu asiyeelimika.
Mwenye elimu ni rahisi sana kucheck in airport kwa kutumia kiosk, bila hata kufundishwa lakini mtu asiyeelimika ni kazi sana kutumia vitu kama hivyo.
Hata kujumlisha tu chenji kamili ni kazi mpaka azoee.
kuna vitu vinapima elimu ya jamii, kimojawapo ni exposure.
 
Back
Top Bottom