'Farouk Tech' inawafaa wengi hapa nchini kukomesha wizi: Mwizi akutwa amelala ndani ya gari

'Farouk Tech' inawafaa wengi hapa nchini kukomesha wizi: Mwizi akutwa amelala ndani ya gari

Kenya yalifanyika Sana hayo maigizo ya kufiniana lakini hakukuwa na video ya kuwaonyesha live watu walibebwa wakiwa wamefunikwa na mashuka kwa kile kinachoitwa kuwastiri watu wasione walivyogandamana uchi kumbe ikaja gundulika Ni uongo na michezo ya kuigiza ya kitapeli ya kumtafutia soko mganga!!!

Hao wa njombe tuwekekee picha Yao ya uchi walivyogandamana Kama unayo au na wewe ulisikia stories tu au uliwaona ?
Wewe ni Mkenya
 
Mi nilipewa ile mwizi akiiba mzigo unaganda hautoki akirudi alipo chukua unakubali kushuka
 
Mi nilipewa ile mwizi akiiba mzigo unaganda hautoki akirudi alipo chukua unakubali kushuka
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Inakuwaje hii?
 
huyu mzee ni balaa kweli huu usingizi sijapata kuuona kabisa 🔥 maajabu zaidi mwizi kaamswa na zaidi ya vibao vitatu na kumwagiwa maji juu kulala gani huku 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 angetutajia tu huyu fundi na sisi tumtafute tumechoka kuibiwa bhana.
 
Akiwa anaelewa hilo Promo atapiga pesa, hata kama si kweli akimpanga mganga fulani wabongo watamiminika
 
Mchezo wa kuigiza. Movie ya kupanga hadi Polisi yumo. Mwizi feki.
 
NA MWANDISHI WETU

Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim, amesema kuwa siri kubwa ambayo mtu yeyote anaweza kuifanya ili wezi watakapofika nyumbani kwake waibe lakini wapitiwe na usingizi hapo hapo ni kumuamini na kumuomba Mungu ili awalinde wote ndani ya familia.

[https://www]

Mwizi aliyekutwa ndani ya gari la Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim.

Farouk ameyabainisha hayo leo Juni 2, 2020, wakati wa mazungumzo mubashara kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na ndipo aliposimulia mkasa wake baada ya mwizi kuruka geti la nyumba yake huko Fuoni visiwani Zanzibar na kuiba nguo na viatu lakini baadaye aliingia ndani ya gari na kupitiwa usingizi.

"Huyu mwizi kaingia usiku wa manane karuka geti, na hatuna mlinzi pale nyumbani, kakusanya zile nguo zilizokuwa zimeanikwa kaziwekwa kwenye mfuko, katika magari yaliyokuwepo pale gari moja lilikuwa wazi akaingia, akapitia mlango wa abiria akachukua power window, akaenda upande wa dereva kuchukua power window ikamshinda ndiyo akalala hapo hapo" amesema Farouk Karim.

Akielezea siri ya mwizi kumuibia na kisha kupitiwa na usingizi Farouk amesema,"Tumempeleka Polisi kama ambavyo huwa tuna msindikiza Bi harusi, na ile kulala huenda kaiba sana hivyo karidhika, na dawa kubwa ya kumfanya mwizi alale ni moja tu kumuomba Mungu akulinde wewe na nyumba yako, na watu kama sisi ambao hatuna madhambi, Dua zinakubalika, kama unataka hiyo Dua nitafute inbox".
 
Back
Top Bottom