Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Fatma Karume amezungumza na Wakili TV na kufafanua mambo kadhaa ikiwemo kuhusu hali ya demokrasia nchini, siasa ya Tanzania na kurejea kwa Tundu Lissu. Huyu hapa anafafanua:
Nikiwa kama Rais mstaafu wa TLS nimefurahi sana kusikia Tundu Lissu anarudi Nchini Tanzania kwa sababu mazingira aliyoondokea hayakuwa ya kuridhisha, yalikuwa mabaya sana.
Hatuwezi kukubali mtu apigwe risasi kama vile kwa sababu ya siasa, haikubaliki kwenye Nchi yoyote inayopenda amani na demokrasia.
Nawaomba Serikali watazame hili suala, kwani waliofanya hicho kitendo cha kihalifu hawajakamatwa, ilikuwa ni kosa la jinai la kujaribu kufanya mauaji.
Serikali imekaa kimya, ni muhimu sana wale watu wakamatwe, kama inashindikana kukamatwa basi Tundu Lissu apewe ulinzi, yeye mwenyewe, familia yake wasipitie yale aliyopitia Septemba 7, 2017.
Baada ya Lissu kupigwa risasi, Watanzania tulipata mshtuko mkubwa sana, tulipitia katika kipindi cha traumatic period.
Niwaambie Watanzania wenzangu, kuwa hakuna jambo baya kukaa kimya ukiona uovu, ni jambo baya sana, tumia chochote ilichokuwa nacho kuonesha haujafurahishwa, tumia hata uso wako au sauti yako kuonesha hivyo.
Kukaa kimya na kupiga makofi huku mambo maovu yakitendeka ni kuungana na huo uovu, tusifanye hiyo tabia na tuiache.
Kuhusu ukimbizi wa kisiasa inasikitisha kuna watu walikimbia Tanzania kutokana na mambo ya kisiasa, siasa si ugomvi, siasa ni haki ya kutazama namna nyingine ya kuendesha Nchi, ni haki ya kila mwananchi kufanya siasa.
Kuwa na Wakimbizi wa kisiasa Tanzania ni aibu sana, niwakumbushe hasa CCM hawa wakimbizi wa kisiasa wametokea wakati wa CCM, tumepata wakimbizi wengi tu zaidi ya Lissu na watu kama kina Lema.
Pemba kuna watu walikimbia kwa sababu ya kisiasa, tuache huu ugomvi, tuishi kama binadamu, Tanzania ni kubwa sana, tupo watu Milioni 62, kuna nafasi sote kuishu humu ndani kwa amani.
Japokuwa hatuwezi kubaliana kwa mawazo lakini sote ni Watanzania, tupendane.
Kuhusu Demokrasia Nchini kwetu, tunakwenda hatua mbili mbele tunarudi tatu nyuma, tunakwenda tano tunarudi nne, tupo kwenye transitional democracy.
Tunatakiwa kutoka huko tuingie kwenye Demokrasia, kwa sabababu bado tupo kwenye transitional democracy, hatuwezi kuingia huko bila kubadilisha Katiba.
Lazima tutazama mfumo wetu wa kisheria na Katiba ili tuingie kwenye demokrasia inayoweza stahili na siyo mtu kuingia kwenye madaraka mkukimkuki.