Fatma Karume: Wamasai waheshimu Sheria zetu Wazanzibar

Fatma Karume: Wamasai waheshimu Sheria zetu Wazanzibar

Huyu mwanasheria na mtu aliyejitambulisha kama mwanaharakati wa haki za binadamu amewashukia Wamasai akitaka wasitembee na panga au rungu kama ilivyo jadi ya utamaduni wao.

Hata hivyo sijawahi kumsikia akikemea wanaume ambao hufunga ndoa au wanaenda katika sherehe za harusi wakiwa wamebeba majambia mfano Ali Kiba au Diamond,
 
Mwanasheria maarufu na mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Fatma Karume, ameunga mkono suala la Wamasai kukatazwa kutembea na Silaha huko Zanzibar.

Kupitia ukurasa wake wa "X" Fatma amesema,

"Ukibeba silaha Zanzibar unavunja Sheria za Jinai, Utamaduni si sababu ya kuvunja sheria.

Wazenji tuna utamaduni wa kubeba HANJAR, hatuzibebi kwasababu ni uvunjifu wa Sheria.

Wamasai waheshimu sheria, Wasibebe silaha hakuna SIMBA ZNZ.

Hakuna haja ya kujilinda na panga ukitoka."- Fatma Karume

View attachment 2890893

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1 ✍️
Wazanzibar wameshiba maharage ya Mbeya sasa wanataka kuharibu shughuli za kitalii wafe njaa. Shibe imewalemea.
 
Hana MAKOSA!
Kwa mjibu wa Katiba ya Zanzibar, Zanzibar ni NCHI ina Serikali yake, Bunge lake (Baraza la Wawakilishi) na Mahakama Kuu yake! Hivyo ina sheria zake! Wanatulazimisha tuwavue koti la Muungano lakini hatutaki!
 
Masai waachiwe sime zao hazina madhara mbona nimewapiga masai wengi sana wakiwa hivyohivyo na sime na rungu zao nyie mnaogopa nini?
Yeah kwa kipindi cha Nyerere angalau umuhimu wa muungano ulionekana sio sasa upo kimkakati wa kisiasa zaidi.
 
Mwanasheria maarufu na mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Fatma Karume, ameunga mkono suala la Wamasai kukatazwa kutembea na Silaha huko Zanzibar.

Kupitia ukurasa wake wa "X" Fatma amesema,

"Ukibeba silaha Zanzibar unavunja Sheria za Jinai, Utamaduni si sababu ya kuvunja sheria.

Wazenji tuna utamaduni wa kubeba HANJAR, hatuzibebi kwasababu ni uvunjifu wa Sheria.

Wamasai waheshimu sheria, Wasibebe silaha hakuna SIMBA ZNZ.

Hakuna haja ya kujilinda na panga ukitoka."- Fatma Karume

View attachment 2890893

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1 ✍️
Uongozi ni hekma na busara. Hakuwa na uweledi katika kuliendea jambo hili hasa kwa kuwataja wamasai pekee. Ingesemwa tu ni marufuku kubeba silala Zanzibar au mjini ikiwa ni kwa watu wote bila kuwataja wamasai au wamwera au wasukuma. Yes, mimi sikubaliani na kubeba silaha kwa hao wamasai au jamii nyingine yoyote lakini pia sikubaliani na utoaji wa maagizo ya utekelezaji wa sheria wenye kuwahusisha jamii au kabila moja tu. Hapo ndipo mlipolikuza jambo. Sime ni silaha lakini ni sehemu ya mavazi kwa mmasai. Yaani haoni kama amekamilika pasipo kuwa na mkanda wenye sime. Je tukienda kwenye jamii ya wamaasai na wao wakisema ni marufuku kuvaa kofia tutawachukuliaje?

Kwa upande mwingine, majambia ni maarufu sana Zanzibar toka enzi ya Sultan. Je kwa kipindi hicho kulikuwa na Simba au Nyati wa kuwawinda na hayo majambia?
 
Msiwapangie,kwani kule ni kwenu ama.
Masai kwenda kule ni sawa na mtalii.
Kwani kule Kuna makazi ya Masai🙄.
Mtakalia hayohayo,ile ni Nchi na Ina uhuru wake,na Sheria na taratibu zake.
Kama nyie ni hamjielewi nyie ni Nani,basi wao wanajitambua.

Kuna Mtanganyika mwenye nyumba kule🤣.ila wazenji wana makazi ya kudumu huku.
Mnajikombw komba vya nn
 
Back
Top Bottom