Fatma Karume: Yaani leo nimethibitisha Adelardus (AG) hajui Katiba, anadai Serikali ina mihimili mitatu na yeye ndie anasimamia yote

Wanafunzi wengi hawakuelewa somo la uraia ndiyo maana wengi wanachanganya vitu hivyo akiwemo Professor Killange.
 
Wee mburula tofautisha kati ya dola na serikali!
 
Kwa hiyo Bunge sio serikali? Mahakama sio serikali?
 
Mwenzenu kaweka Hadi reference, Nyie mnamshambulia yeye Kama yeye. Tatizo Ni Nini mataga?

Hizo reference ndo shida kuzitambua na ndio maana kila mara wanashinswa baada ya kupewa tafsiri halisi
Yeye anaweza kuzifahamu hizo reference kama wanavyojua wasabato, R catholic na walokole kwenye neno la mungu.
 
Ulikuwa wapi kwenda shule uje unisumbue humu Jf. Nenda kamtafute Prof Safari.
Tatizo ulifundishwa na Waalimu ambao pia Ni failure Mama wewe ikapelekea na wewe ukafeli na bahati mbaya zaidi HUJUI kama Hujui.
Tuna kitu kinaitwa DOLA na kwa waalimu na wakufunzi waliotufundisha sisi wengine, kwa Kiingereza tuna State. Dola ndiyo yenye Mihimili Mi 3. Mmoja ni Serikali, mwingine ni Bunge, na wa Mwisho ni Mahakama. Ukisoma Katiba ya JMT Ibara ya 4, utaelewa angalau kidogo. Kwa kiingereza ambacho ni cha elimu ya juu, tuna 3 Arms of State ambazo ni 1. Executive (Government) 2. Legislature (Parliament) na 3. Judiciary.

Huyo Mwalimu aliekufundisha 3 Branches of the Government, aidha yeye mwenyewe ndie tatizo, au Mtaala uliotumika kukufundisha (ambao naamini ulitungwa kutengeneza VILAZA wengi kama ulivyo lengo likiwa kuendelea kuwatawala)

Kama hadi hapa utakuwa mbishi, basi endelea kutetea 7000/ yako.
 
Kwa hiyo Bunge sio serikali? Mahakama sio serikali?
Naomba kukuuliza kwa wepesi KABISA?

1. Mbunge ni mtumishi wa Serikali?
Usinichanganyie na habari za UTUMISHI wa umma.

2. Hakimu au Jaji ni mtumishi wa Serikali?

NB
Unapozungumzia Serikali ziko mbili ni ile ya KUU NA TAMISEMI hawa ndio wanaoingia kwenye kundi la watumishi wa Serikali ukiondoa nafasi zote za kuchaguliwa na wananchi Mfano Rais na Mawaziri.

Hivyo unaposema Watumishi wa Serikali hasa ni TAMISEMI NA SERIKALI KUU pekee, wengine wanaingia kwenye kundi la Watumishi wa umma.
 
Bado


Kwa sasa kutokana na sheria ya juzi pia na mwanya wa kikatiba yeye ni mshauri wa mihimili yote

AG ni mshauri wa serikali
AG ni mbunge na mshauri wa bunge kwenye masuala ya utungaji na kufuata sheria husika bungeni

AG ni mshauri wa mahakama kutokana na tume ya utumishi wa Umma ambaye yeye ni mjumbe

Ni mshauri wa mihimili mitatu katika mashauri ya wakuu wa vyombo hivyo


Fatuma anasema moja katika 3 yaani nguvu hizo haziko sawa kwa kuwa 1 ndiye anazaa tatu as if hakuna watu! Rais licha ya kuwa kiongozi wa nchi hapaswi kuingilia mifumo mingine kiutendaji isipokuwa kwenye checks and balance

Msingi wa mhimili na watu hivyo ndiyo maana uchaguliwa kwa kuwa mahakama ni ya kudumu na uhitaji wa watendaji inaundwa na principle za utendaji na si mawazo ya watu isipokuwa mkuu ambaye anachaguliwa na rais aliyechaguliwa na watu kisha anapaswa kuidhinishwa na bunge ambao ndiyo watu kwa mifumo ya marekani na kenya lkn ilipaswa CJ achaguliwe na bunge ambao ni wawakilishi wa watu tena kwa kura ya siri baada ya kuomba nafasi hiyo kwa utaratibu uliowekwa au watendaji wote wa mahakama ndiyo wapige kura kumchagua kiongozi wao mkuu kama lilivyo bunge hata kama si mwajiriwa isipokuwa awe na cheti cha sheria au leseni ya uanasheria

Tunaendelea
 
Mamlaka ya nchi yanaendeshwa kwa kuwa na mimili mitatu ambayo ni Executivu,judiciary na legislature ambayo ndio serikali. Sasa Tatizo lipo wapi?
 
Unazidi kunikoroga hebu serikali iwekee mabano kwa lugha ya kibeberu labda ntaweza kukuelewa mfano dola(state), serikali( ? )
 
Mkuu kwani uanasheria mkuu wa serikali niwa kusomea au kuteuliwa? Na Kama niwa kuteuliwa why unadhani kuwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ndo kujua Sheria?
MKuu, Raisi akiteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye hana uwezo wa kuzijua sheria basi huyo raisi hana akili sawasawa. Ndio maana Mwanasheria Mkuu anapaswa awe amekuwa wakili kwa miaka si chini ya 15, ikimaanisha kuwa na uzoefu mwingi wa kushughulika na kesi mbalimbali za kisheria nk. Sasa ukiangalia Fatima, ni mzoefu sana katika haya mambo, kuanzia shule alizosoma, kuwa mwajiriwa katika kampuni maarufu ya Sheria ya Mkono & Co, na hatimae partner katika kampuni maarufu ya uwakili. Huwezi kumlinganisha Fatima kiuwezo wa sheria na Mwanasheria Mkuu. Lakini hili jambo Fatima alilolitolea tamko, ni dogo sana kwa Mnwanasheria Mkuu kutolielewa. Na kama tuna Mwanasheria Mkuu haelewi jambo dogo kama hili basi ni kihiyo sana wa sheria! Atakuwa katika kundi la watu Magufuli anateua sio kwa kuangalia uwezo wao, bali kwa sababu zake binafsi
 
Waambie hao mapimbi
 
N
Nikujibu wewe hujanijibu? Kwani anaewalipa wabunge na watumishi wa mahakama si Executive ambae ni Rais. Jibu kwanza bunge ni serikali? Mahakama ni serikali?
 
Unajua chanzo cha alichokisema au umedandia treni kwa mbele. Fatma kaitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili. Mlalamikaji ni AG Prof Kilangi anaelalamika kukejeliwa na Fatma. Ameambiwa aseme kejeli ni zipi hapo, kashindwa, kaanza kusema Serikali ina Mihimili Mitatu, kabla ya kumalizia maelezo yake Fatma kaondoka zake maana hawezi endesha kesi na mtu anaekwaambia SERIKALI ina Mihimili Mitatu.
 
Hypothetically

Mwenyekiti wa Kijiji ni mjumbe wa kamati ya Usalama ya Wilaya, unataka kuniambia Mwenyekiti ni msimamizi wa kamati ya Usalama ya Wilaya?

Mwanasheria Mkuu sio msimamizi bali mshauri na hapo ndipo usahihi wa Fatma ulipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…