Dola (state) ndiyo yenye mihimili mitatu ambayo ni serikali, mahakama na bunge, na kila mhimili una mkuu wake. Tanzania na nchi nyingine zenye mfumo kama wa Tanzania ndiko mkuu wa serikali pia ni mkuu wa dola (head of state), lakini katika nchi nyingine za mfumo wa kidemokrasia kuna head of state ambaye anaweza kuwa rais (kama vile India, Ujerumani) na mkuu wa serikali ambaye ni waziri mkuu. Kwingineko mkuu wa dola ni mfalme au malkia (kama UK, Uholanzi nk) na mkuu wa serikali ni waziri mkuu.
Hapa kwetu waziri mkuu ni kiongozi wa mawaziri lakini hana executive powers kwa sababu mfumo wetu ni wa executive presidency.