Fatma Karume: Yaani leo nimethibitisha Adelardus (AG) hajui Katiba, anadai Serikali ina mihimili mitatu na yeye ndie anasimamia yote

Dola (state) ndiyo yenye mihimili mitatu ambayo ni serikali, mahakama na bunge, na kila mhimili una mkuu wake. Tanzania na nchi nyingine zenye mfumo kama wa Tanzania ndiko mkuu wa serikali pia ni mkuu wa dola (head of state), lakini katika nchi nyingine za mfumo wa kidemokrasia kuna head of state ambaye anaweza kuwa rais (kama vile India, Ujerumani) na mkuu wa serikali ambaye ni waziri mkuu. Kwingineko mkuu wa dola ni mfalme au malkia (kama UK, Uholanzi nk) na mkuu wa serikali ni waziri mkuu.
Hapa kwetu waziri mkuu ni kiongozi wa mawaziri lakini hana executive powers kwa sababu mfumo wetu ni wa executive presidency.
Wanafunzi wengi hawakuelewa somo la uraia ndiyo maana wengi wanachanganya vitu hivyo akiwemo Professor Killange.
 
Serikali ni mhimili mmoja kati ya 3,ana maanisha nini?
Serikali ina mihimili 3,Executive judiciary and Legislature, kosa liko wapi? Maana ni serikali moja iliyojigawa katika mihimili mitatu.
Chadema imejaa wavuta bangi na wanywa konyagi. Upuuzi kama huu sio wa kushabikia.
Wee mburula tofautisha kati ya dola na serikali!
 
Kwakua uzi huu ni wa kitaaluma naomba washabili wa siasa mtupishe kwanza kidogo mtachangia uzi ukifikisha koment 500+ labda huko mtakua na la kusema ila kwa sasa tafadhali nendeni SNAPCHAT kwanza.

Ok anachokisema Fatma Karume ni sahihi tatizo ni tafsiri ya neno executive na Serikali.

Alipaswa kusema Tanzania inafuata mfumo wa Nchi za Jumuia ya Madola ambapo Dola huundwa na mihimili mitatu nayo ni SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA.

Mwanasheria Mkuu sio msimamizi wa mihimili yote mitatu bali yeye ni mshauri wa masuala ya kisheria chini ya muhimili mmoja wa Serikali.

Ahsante
Kwa hiyo Bunge sio serikali? Mahakama sio serikali?
 
Mwenzenu kaweka Hadi reference, Nyie mnamshambulia yeye Kama yeye. Tatizo Ni Nini mataga?

Hizo reference ndo shida kuzitambua na ndio maana kila mara wanashinswa baada ya kupewa tafsiri halisi
Yeye anaweza kuzifahamu hizo reference kama wanavyojua wasabato, R catholic na walokole kwenye neno la mungu.
 
Ulikuwa wapi kwenda shule uje unisumbue humu Jf. Nenda kamtafute Prof Safari.
Tatizo ulifundishwa na Waalimu ambao pia Ni failure Mama wewe ikapelekea na wewe ukafeli na bahati mbaya zaidi HUJUI kama Hujui.
Tuna kitu kinaitwa DOLA na kwa waalimu na wakufunzi waliotufundisha sisi wengine, kwa Kiingereza tuna State. Dola ndiyo yenye Mihimili Mi 3. Mmoja ni Serikali, mwingine ni Bunge, na wa Mwisho ni Mahakama. Ukisoma Katiba ya JMT Ibara ya 4, utaelewa angalau kidogo. Kwa kiingereza ambacho ni cha elimu ya juu, tuna 3 Arms of State ambazo ni 1. Executive (Government) 2. Legislature (Parliament) na 3. Judiciary.

Huyo Mwalimu aliekufundisha 3 Branches of the Government, aidha yeye mwenyewe ndie tatizo, au Mtaala uliotumika kukufundisha (ambao naamini ulitungwa kutengeneza VILAZA wengi kama ulivyo lengo likiwa kuendelea kuwatawala)

Kama hadi hapa utakuwa mbishi, basi endelea kutetea 7000/ yako.
 
Kwa hiyo Bunge sio serikali? Mahakama sio serikali?
Naomba kukuuliza kwa wepesi KABISA?

1. Mbunge ni mtumishi wa Serikali?
Usinichanganyie na habari za UTUMISHI wa umma.

2. Hakimu au Jaji ni mtumishi wa Serikali?

NB
Unapozungumzia Serikali ziko mbili ni ile ya KUU NA TAMISEMI hawa ndio wanaoingia kwenye kundi la watumishi wa Serikali ukiondoa nafasi zote za kuchaguliwa na wananchi Mfano Rais na Mawaziri.

Hivyo unaposema Watumishi wa Serikali hasa ni TAMISEMI NA SERIKALI KUU pekee, wengine wanaingia kwenye kundi la Watumishi wa umma.
 
Kwakua uzi huu ni wa kitaaluma naomba washabili wa siasa mtupishe kwanza kidogo mtachangia uzi ukifikisha koment 500+ labda huko mtakua na la kusema ila kwa sasa tafadhali nendeni SNAPCHAT kwanza.

Ok anachokisema Fatma Karume ni sahihi tatizo ni tafsiri ya neno executive na Serikali.

Alipaswa kusema Tanzania inafuata mfumo wa Nchi za Jumuia ya Madola ambapo Dola huundwa na mihimili mitatu nayo ni SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA.

Mwanasheria Mkuu sio msimamizi wa mihimili yote mitatu bali yeye ni mshauri wa masuala ya kisheria chini ya muhimili mmoja wa Serikali.

Ahsante
Bado

Kwa sasa kutokana na sheria ya juzi pia na mwanya wa kikatiba yeye ni mshauri wa mihimili yote

AG ni mshauri wa serikali
AG ni mbunge na mshauri wa bunge kwenye masuala ya utungaji na kufuata sheria husika bungeni

AG ni mshauri wa mahakama kutokana na tume ya utumishi wa Umma ambaye yeye ni mjumbe

Ni mshauri wa mihimili mitatu katika mashauri ya wakuu wa vyombo hivyo

Fatuma anasema moja katika 3 yaani nguvu hizo haziko sawa kwa kuwa 1 ndiye anazaa tatu as if hakuna watu! Rais licha ya kuwa kiongozi wa nchi hapaswi kuingilia mifumo mingine kiutendaji isipokuwa kwenye checks and balance

Msingi wa mhimili na watu hivyo ndiyo maana uchaguliwa kwa kuwa mahakama ni ya kudumu na uhitaji wa watendaji inaundwa na principle za utendaji na si mawazo ya watu isipokuwa mkuu ambaye anachaguliwa na rais aliyechaguliwa na watu kisha anapaswa kuidhinishwa na bunge ambao ndiyo watu kwa mifumo ya marekani na kenya lkn ilipaswa CJ achaguliwe na bunge ambao ni wawakilishi wa watu tena kwa kura ya siri baada ya kuomba nafasi hiyo kwa utaratibu uliowekwa au watendaji wote wa mahakama ndiyo wapige kura kumchagua kiongozi wao mkuu kama lilivyo bunge hata kama si mwajiriwa isipokuwa awe na cheti cha sheria au leseni ya uanasheria

Tunaendelea
 
Dola (state) ndiyo yenye mihimili mitatu ambayo ni serikali, mahakama na bunge, na kila mhimili una mkuu wake. Tanzania na nchi nyingine zenye mfumo kama wa Tanzania ndiko mkuu wa serikali pia ni mkuu wa dola (head of state), lakini katika nchi nyingine za mfumo wa kidemokrasia kuna head of state ambaye anaweza kuwa rais (kama vile India, Ujerumani) na mkuu wa serikali ambaye ni waziri mkuu. Kwingineko mkuu wa dola ni mfalme au malkia (kama UK, Uholanzi nk) na mkuu wa serikali ni waziri mkuu.
Hapa kwetu waziri mkuu ni kiongozi wa mawaziri lakini hana executive powers kwa sababu mfumo wetu ni wa executive presidency.
Mamlaka ya nchi yanaendeshwa kwa kuwa na mimili mitatu ambayo ni Executivu,judiciary na legislature ambayo ndio serikali. Sasa Tatizo lipo wapi?
 
Dola (state) ndiyo yenye mihimili mitatu ambayo ni serikali, mahakama na bunge, na kila mhimili una mkuu wake. Tanzania na nchi nyingine zenye mfumo kama wa Tanzania ndiko mkuu wa serikali pia ni mkuu wa dola (head of state), lakini katika nchi nyingine za mfumo wa kidemokrasia kuna head of state ambaye anaweza kuwa rais (kama vile India, Ujerumani) na mkuu wa serikali ambaye ni waziri mkuu. Kwingineko mkuu wa dola ni mfalme au malkia (kama UK, Uholanzi nk) na mkuu wa serikali ni waziri mkuu.
Hapa kwetu waziri mkuu ni kiongozi wa mawaziri lakini hana executive powers kwa sababu mfumo wetu ni wa executive presidency.
Unazidi kunikoroga hebu serikali iwekee mabano kwa lugha ya kibeberu labda ntaweza kukuelewa mfano dola(state), serikali( ? )
 
Mkuu kwani uanasheria mkuu wa serikali niwa kusomea au kuteuliwa? Na Kama niwa kuteuliwa why unadhani kuwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ndo kujua Sheria?
MKuu, Raisi akiteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye hana uwezo wa kuzijua sheria basi huyo raisi hana akili sawasawa. Ndio maana Mwanasheria Mkuu anapaswa awe amekuwa wakili kwa miaka si chini ya 15, ikimaanisha kuwa na uzoefu mwingi wa kushughulika na kesi mbalimbali za kisheria nk. Sasa ukiangalia Fatima, ni mzoefu sana katika haya mambo, kuanzia shule alizosoma, kuwa mwajiriwa katika kampuni maarufu ya Sheria ya Mkono & Co, na hatimae partner katika kampuni maarufu ya uwakili. Huwezi kumlinganisha Fatima kiuwezo wa sheria na Mwanasheria Mkuu. Lakini hili jambo Fatima alilolitolea tamko, ni dogo sana kwa Mnwanasheria Mkuu kutolielewa. Na kama tuna Mwanasheria Mkuu haelewi jambo dogo kama hili basi ni kihiyo sana wa sheria! Atakuwa katika kundi la watu Magufuli anateua sio kwa kuangalia uwezo wao, bali kwa sababu zake binafsi
 
Hahaaaa hujui kuwa kwenye chama chenu ndo kuna vilaza? Ndo maana huwez kuta bungeni Mbunge wa upinzani aliyeishia standard seven all are educated ,,,, Tumeshuhudia kila aliyetoka chadema ameingia ccm na kupewa either uwaziri or ukuu wa wilaya directly huku nyie sisiem mkikaa benchi kisa ELIMU yenu
Waambie hao mapimbi
 
N
Naomba kukuuliza kwa wepesi KABISA?

1. Mbunge ni mtumishi wa Serikali?
Usinichanganyie na habari za UTUMISHI wa umma.

2. Hakimu au Jaji ni mtumishi wa Serikali?

NB
Unapozungumzia Serikali ziko mbili ni ile ya KUU NA TAMISEMI hawa ndio wanaoingia kwenye kundi la watumishi wa Serikali ukiondoa nafasi zote za kuchaguliwa na wananchi Mfano Rais na Mawaziri.

Hivyo unaposema Watumishi wa Serikali hasa ni TAMISEMI NA SERIKALI KUU pekee, wengine wanaingia kwenye kundi la Watumishi wa umma.
Nikujibu wewe hujanijibu? Kwani anaewalipa wabunge na watumishi wa mahakama si Executive ambae ni Rais. Jibu kwanza bunge ni serikali? Mahakama ni serikali?
 
Hako Ka Shangazi huwenda ni kaongo vibaya Sana, eidha kametumia Ile nafasi ya Ulimi hauna mifupa ndipo kakaandika huu ujinga hapa,

Kwanza CV ya AG na CV ya Shangazi ni Sawa na Mbingu na Aridhi, kameamua kuwa kadakia vijimakosa vya Ulimi ndipo kanapata genda za kisiasa, Ujinga tu
Unajua chanzo cha alichokisema au umedandia treni kwa mbele. Fatma kaitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili. Mlalamikaji ni AG Prof Kilangi anaelalamika kukejeliwa na Fatma. Ameambiwa aseme kejeli ni zipi hapo, kashindwa, kaanza kusema Serikali ina Mihimili Mitatu, kabla ya kumalizia maelezo yake Fatma kaondoka zake maana hawezi endesha kesi na mtu anaekwaambia SERIKALI ina Mihimili Mitatu.
 
Bado

Kwa sasa kutokana na sheria ya juzi pia na mwanya wa kikatiba yeye ni mshauri wa mihimili yote

AG ni mshauri wa serikali
AG ni mbunge na mshauri wa bunge kwenye masuala ya utungaji na kufuata sheria husika bungeni

AG ni mshauri wa mahakama kutokana na tume ya utumishi wa Umma ambaye yeye ni mjumbe

Ni mshauri wa mihimili mitatu katika mashauri ya wakuu wa vyombo hivyo

Fatuma anasema moja katika 3 yaani nguvu hizo haziko sawa kwa kuwa 1 ndiye anazaa tatu as if hakuna watu! Rais licha ya kuwa kiongozi wa nchi hapaswi kuingilia mifumo mingine kiutendaji isipokuwa kwenye checks and balance

Msingi wa mhimili na watu hivyo ndiyo maana uchaguliwa kwa kuwa mahakama ni ya kudumu na uhitaji wa watendaji inaundwa na principle za utendaji na si mawazo ya watu isipokuwa mkuu ambaye anachaguliwa na rais aliyechaguliwa na watu kisha anapaswa kuidhinishwa na bunge ambao ndiyo watu kwa mifumo ya marekani na kenya lkn ilipaswa CJ achaguliwe na bunge ambao ni wawakilishi wa watu tena kwa kura ya siri baada ya kuomba nafasi hiyo kwa utaratibu uliowekwa au watendaji wote wa mahakama ndiyo wapige kura kumchagua kiongozi wao mkuu kama lilivyo bunge hata kama si mwajiriwa isipokuwa awe na cheti cha sheria au leseni ya uanasheria

Tunaendelea
Hypothetically

Mwenyekiti wa Kijiji ni mjumbe wa kamati ya Usalama ya Wilaya, unataka kuniambia Mwenyekiti ni msimamizi wa kamati ya Usalama ya Wilaya?

Mwanasheria Mkuu sio msimamizi bali mshauri na hapo ndipo usahihi wa Fatma ulipo.
 
Back
Top Bottom