MKuu, Raisi akiteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye hana uwezo wa kuzijua sheria basi huyo raisi hana akili sawasawa. Ndio maana Mwanasheria Mkuu anapaswa awe amekuwa wakili kwa miaka si chini ya 15, ikimaanisha kuwa na uzoefu mwingi wa kushughulika na kesi mbalimbali za kisheria nk. Sasa ukiangalia Fatima, ni mzoefu sana katika haya mambo, kuanzia shule alizosoma, kuwa mwajiriwa katika kampuni maarufu ya Sheria ya Mkono & Co, na hatimae partner katika kampuni maarufu ya uwakili. Huwezi kumlinganisha Fatima kiuwezo wa sheria na Mwanasheria Mkuu. Lakini hili jambo Fatima alilolitolea tamko, ni dogo sana kwa Mnwanasheria Mkuu kutolielewa. Na kama tuna Mwanasheria Mkuu haelewi jambo dogo kama hili basi ni kihiyo sana wa sheria!