FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu

Nenda Moshi, Dar es Salaam street ukajionee machangudoa. Wachaga kwenye hela hawajui Yesu. Kinachowasaidia huwa wako smart sana
 
Yeye alifuatwa na wateja na kumpa design ya Tank(lilowekwa chemicals za bomu na kilipuzi (bom detonetor ) wakamlipa na kuchukuwa tank lao. akuusika kama muunda bomu
Kibongo bongo nae angeonja joto ya jiwe.

Wenzetu wanafanya kazi kwa weledi na haki mtu usiyehusika hupewi case kizembe bongo ukihisiwa tu kwa lolote hata kama ulikatiza eneo la tukio muda linatokea unaweza ukaoga mvua.
 
Tuwaheshimu kwakuwadharau polisi wetu!? Kwani ugaidi na Tanzania wapi na wapi!?
Kila nchi ina uzoefu wa kukabiliana na uhalifu uliokithiri kwenye nchi zao

Kwa Polisi hawa wa Wambura, unawezakuta 50% ya wanaodaiwa ni wahalifu, sio wahalifu kwa sababu inatumika akili ndogo sanaaaa kuwatambua wahalifu
 

Ulianza vizuri ukamalizia na pumba. Marekani hawazi kumnasa Putin na ikitokea wakafanya hivyo either marekani au Urusi inaweza futika kwenye ramani ya duniani
 
Ilikuaje,hebu tupe faida na sisi

Kilikua ni kipindi kigumu cha vurugu za kidini katika miaka ya 90's mwanzoni nchini India.
Dutt baba yake ni mhindu mama yake alikua ni muislamu, kwahiyo hilo halikumuacha salama akawa anapokea barua za vitusho nyingi kutoka watu wasiojulikana akishutumiwa kama kuwa ana damu ya kiislamu na wao wahindu hawamtaki kuwa pamoja nao na wanaweza kumfanyia baya lolote. Jamaa alivyooona vitisho ni vizito sana, akaona isiwe tabu akatafuta connection ya kupata silaha ya kujihami.
Kwahiyo akapata connection kwa arm dealers wakamuahidi watamuekea mambo sawa.
Bomb Blast ya Bombay ilifanywa na Gangsters' amabao ndio walikua waki rule ma gang ya kihuni Mumbai ambao majority yao walikua ni waislamu. SO ulipofanyika ule mchongo wa miripuko mzigo ulipitia Bahari ya Gujrati ukasafairishwa kwa malori mpaka mumbai. Wengi walioshiriki hili jambo hawakuwa waki juwa lolote kama ilivyo matukio mengi ya Kigaidi. Wanaokua wanafahamu ni wachache sana.
Mzigo uliingia Gujrat ukionekanwo kama mizo wa Pombe ukisimamiwa na Wavuvi na maofisa Neavy. Kipindi hicho Gujrat Pombe ilipigwa marufuku kwahiyo Pombe ilikua ndio dili kubwa ya kimagendo ukanda ule. Na baada ya hapo ukasafirishwa kwa malori mpaka Mumbai. Ulipofika Mumbai mzigo ukaelekea moja kwa moja kwenye Nyumba ya Dutt. akapewa Bunduki yake. Na jamaa wakamuomba awahifadhie gari ilikua na mzigo kwa muda wa siku mbili tatu watakuja kuuchukua waende nao sehemu zao husika. Yeye akaona isiwe noma akawahifadhia gari lao ndani ya kompound yake huku yeye akijua kua lile gari limebaba silaha na risasi za biashara ambazo walikua wakiuuza kwa magendo. Kumbe ndani yake hamkua na silaha tu bali mulikua na Mabomu yaliyotumika kuripulia.
Baada siku mbili tatu wakachukua mzigo wao maisha yakaendelea.
Mara tu baada mabomu kuripuka katika msako wa ufuatiliaji ndio ikagundulikana kuwa mzigo uliwahi lala kwenye nyumba ya Dutt kwa siku mbili tatu, nayeye akaingizwa kundini ya watuhumiwa. ALikaa ndani kwa muda wa miaka miwili, na alipotoka kesi iliendelea kwa zaidi ya miaka 10. Na mwisho alshinda kesi kuwa hakuhusika na ugaidi, Ila alihukumiwa kufungwa miaka 6 kwa kosa la umilikaji wa sialha kinyume na Sheria.

Wengi waliohusika kwenye lile tukio hawakuelewa kabisa kinachoendelea. Wengine walielewa ni Ishu za Pombe haramu, wengine walijua ni Madawa ya kulevya, wengine walijua silahi za biashara. So walishirikishwa bila kufahamu nini wanafanya. Wengi waliteswa, wengine walijiua kwa fadhaa, wengine walifia majela. Wako waliokuja kutoka siku za mbele ila mpaka leo wanashindwa kuishi kwa amani.

Magaidi wa kimataifa ni watu wanaofanya mambo yao kwa kutumia akili kubwa mno.
 
Kenya siku mbili baada ya kushambuliwa alitumwa Fbi mmoja ambaye kwa maelezo yake alikuwa hajawahi kukanyaga ardhi ya Afrika , let alone Kenya ,
Jamaa ndani ya saa 24 toka kuingia kenya alifanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa anauguzwa hospitalini kwa kutumia jina bandia ..
 
Dah wwnzetu wako mbali kwenye mambo ya intelligence
 
Dah wwnzetu wako mbali kwenye mambo ya intelligence
Ni hadi upate nafasi ya kujua wanayoyafanya , otherwise utaona marekani na intelligence yao ni ya kawaida .
Shambulio la Nairobi lilikuwa na changamoto ya taarifa ,mashuhuda walikuwa wanasema gari lililokuwa limebeba bomu lilikuwa canter, uhalisia ninkuwa gari lililobema bomu lilikuwa ni Isuzu, ambayo kwa wakati huo nalo lilikuwa maarufu kwa jina la canter , pamoja na misleading info , Fbi walikamata wahusika
 
Hatari
 
Asnt mkuu kwa simulizi nzr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…