FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu

Upo sahihi FBI walianza kwa kunusa boza la maji lilobeba bomu. Wakagundua vitu viwili. Modification iliyofanywa kwenye Boza kuweza kubeba bomu la uzito ule, Aina ya vyuma vilivyotumika, aina ya kilipuzi (baruti) iliyotumika.
Kujulikana kwamambo hayakulisababisha usadisi juu ya Karakana gani yenye vyuma na uwezo wa kukata vyuma vikubwa na kutengeneza carriage ya lile bobu, Duka gani lenye uwezo wa kuuza Fertilizer ya ujazo ule na kwa sababu vyuma vilionyesha kukatwa kwa gesi ni wapi gesi hiyo inapatikana.
Hapo ndipo Karakana ya uncle Thomas (mtengenezaji wa trailers za malori) akawa mshukiwa kwa sababu hapakuwa na Karakana kubwa binafsi ya kuunga vyuma zaidi yake. Katika mahojiano alipatika fundi aliyefanya kazi ile kwa maelekezo ya mtuhumiwa wa ugaidi bila yeye kujua nini kazi ya kitu anacho tengezeza. Risiti za TOL na Fertilizer zikathibitisha karakana ya Thomas na gaidi ndio wanunuzi wakubwa ktk kipindi hicho.
 
Kino miaka hiyo balaa
 
Baada ya matukio ya Dar na Nairobi, baadae ikalipuliwa USS Cole na Ahmed Shah Masoud kuwa assasinated, mwamba Putin akaunganisha dots akaona kuna jambo zito linaenda kuwatokea wamarekani. Akampigia simu Bush akamtahadhalisha kuhusu tukio kubwa na kweli baada ya siku kadhaa Sep 11 hii hapa.
 
Hatuwezi kuwafikia si
Leo wala kesho
USA ni ngumu sana kusingiziwa kesi ukiwa na mwanasheria mzuri,maana wanaamini katika evidence kabla ya judgement
Huku bongo sasa...
Bongo unapewa judgement kabla ya trial na trial kabla ya evidence.
Yaani wakikuhisi tu utachezea kipigo wakuvunje vunje Taya na mbavu! Trial ikifanyika na judgement inatoka huna kesi ya kujibu!!
 
Yaani kwa bongo hadi manyoka ya hiyo gereji na jamaa zake wa Moshi waliokuwa wakimpigia simu au kula nae kitimoto muda huu bado wangekuwa wanasota segerea na Kisongo!
Elimu ni ufunguo wa maisha!
Dah nimecheka sana
 
USA balaa sana. Miezi imepita ubalozi wa US walitoa warning kuhusu matukio ya kigaidi out of nowhere tu na wabongo tukabaki tunashangaa, baadae ikasikika mkuu fln wa magaidi kakamatwa ukanda huu wa afrika. Ndo nikasanuka hawa jamaa walikua na intel mapema sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…