FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu

FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu

USA balaa sana. Miezi imepita ubalozi wa US walitoa warning kuhusu matukio ya kigaidi out of nowhere tu na wabongo tukabaki tunashangaa, baadae ikasikika mkuu fln wa magaidi kakamatwa ukanda huu wa afrika. Ndo nikasanuka hawa jamaa walikua na intel mapema sana

Naomba link ya hiyo story ya aliekamatwa kama hutajali
 
Huyu Bwana yuko zake Kimara Bucha kwenye kasri au tuite hekalu lake mithili ya ikulu ndogo ya Singida, anakula bata huku akilea wajukuu,ameshazeeka sasa.

Yeye na kizazi chake walipigwa ban wasikanyage USA wala kusogelea ubalazi wao.

Wakati ubalozi wa Marekani unalipuliwa nchini pamoja na Nairobi Kenya, polisi na wapelelezi wetu wakaanza kukamatakamta watu ovyo eti ni washukiwa,watu wasiopungua 200 walikuwa shimoni kule Central Police, DSM.

FBI wakapata taharifa kuwa kuna suspects wamekamatwa wako central, wakaomba kuwaona. Kufika kule wakawaambia polisi wa bongo kuwa waachieni wote hakuna suspect hapa, hakuna gaidi anavaa yeboyebo amepauka kwa njaa.hawa ni vibaka tu,IGP akaambiwa u know anything about terrorism?

Jamaa wakaingia chimbo wakaomba akaunti za wafanyabiashara na vionhozi wote wa kisiasa na wanaharakati ambao wameingiziwa mpunga mrefu ndani ya miezi kadhaa (sikumbuki) Thomas Lyimo mfanyabiashara aliyekuwa na garage yake Kimara bucha na vibanda vya maziwa Dar nzima enzi hizo akajikuta matatani, ni baada ya kuonekana akaunti yake iliingiziwa pesa hazina maelezo, kipindi hicho sheria ya money laundering haijatungwa.

Kufustilia kwa kina ni kweli bomu lililolipua ubalozi liliunganishiwa kimara kwenye garage yake.

Hayo yakifanyika mastermind alikuwa kijana mdogo toka Zanzibar Ahmed Khalfan Ghailan ndie alimuingizia huo mpunga kabla ya kukimbilia Nairobi na uarabuni.alikuwa kijana mfogo tu wa miaka 24 au 25, kwa sasa bwana Ghailan ni mtu mzima sasa anakaribia miaka 50 yuko Guantanamo Bay Camp chini ya ilinzi mkali.

Huwapendi USA ila una vingi vya kujifunza kwao

OKW BOBAN SUNZU
Rekodi
 
USA balaa sana. Miezi imepita ubalozi wa US walitoa warning kuhusu matukio ya kigaidi out of nowhere tu na wabongo tukabaki tunashangaa, baadae ikasikika mkuu fln wa magaidi kakamatwa ukanda huu wa afrika. Ndo nikasanuka hawa jamaa walikua na intel mapema sana
Ni kazi ya ujasusi. Marekani wana majasusi kila sehemu. Na hapa nazungumzia majasusi wale ambao ni sehemu ya hivyo vikundi vya kigaidi. Kwa mfano wanaweza ''kumtongoza'' mjahidina wa Al Shabab, wakampa fedha ndefu, wakamwambia endelee kuishi kwenye hilo kundi huku akijifanya ni mwenzao ili achukuwe siri na mikakati yao. Siri wanazozipata mara kwa mara ndiyo zinasaidia kutoa maonyo kama hayo.
 
Hapo tutatofautiana mkuu. Mchaga yesu ni utamaduni tu mbele ya hela hela iko mwanzo.
Wachaga wengi wenye maduka (Kwa mangi) wana redio iko tuned Radio Maria muda wote unaweza sema utakatifu ndio huu sasa, cha ajabu ktk kila kilo moja ya unga, mchele, sukari na mafuta ya kupikia lazima anapiga kiasi fulani na hicho anachopiga ndio anakula yeye unakuta mara nyingi wanapikia humohumo dukani. Kingine ana uza tena kupata hela ya vitunguu, nyanya, ndizi na nyama.

Achana na kina Mangi aisee....[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sheria na taratibu nyingi sana viwanja za ndege zimewekwa na kubadilishwa baada ya matukio ya kigaidi!
Jamaa awakurupuki. Kule Libya Ghadafi alipopanga kulipua ndege ya Wamarekani kwenye anga la UK. Mahesabu ilikuwa ndege idondokee baharini hivyo kufanya uchunguzi wa nini kimesababisha ajali uwe mgumu na isiwezekane. Bahati Mbaya Ndege ikaangukia kwenye makazi ya watu kule Lockerbie. Pale walipata mabaki ya electronic timer circuit iliyoundwa na Kampuni moja ya Uswis. FBI wakatia timu Uswis wakaomba wanunuzi wa zile timers boards. Kwenye list wakaona Libya walinunua circuit 12. Wakawabana waonyeshe walivyozitumia[emoji23]Ghadafi circuit 2 akakosa maelezo amezitumiaje , wakampa zile 2 zilizokutwa kwenye mabaki ya ajali ya Ndege na walipo connect the dots backward( always we connect the dots backward[emoji16]) wakaja gundua kuwa kuna majamaa wawili waliingiza mizigo yao (2-Briefcases (Samsonite- Brand) ambazo ndo mabomu yenyewe) ndani ya Ndege lakini awakupanda. (Now days ukishakaa kwenye kiti ndani ya ndege ndo mizigo yako inaingia nayo!) wale majamaa walikamatwa na wakakutwa ni majausi wabobezi wa Libya. Mmoja wamwemwachia miaka ya hivi karibuni toka jela kwa sababu za kibinadamu (ana kansa)
 
Huyu Bwana yuko zake Kimara Bucha kwenye kasri au tuite hekalu lake mithili ya ikulu ndogo ya Singida, anakula bata huku akilea wajukuu,ameshazeeka sasa.

Yeye na kizazi chake walipigwa ban wasikanyage USA wala kusogelea ubalazi wao.

Wakati ubalozi wa Marekani unalipuliwa nchini pamoja na Nairobi Kenya, polisi na wapelelezi wetu wakaanza kukamatakamta watu ovyo eti ni washukiwa,watu wasiopungua 200 walikuwa shimoni kule Central Police, DSM.

FBI wakapata taharifa kuwa kuna suspects wamekamatwa wako central, wakaomba kuwaona. Kufika kule wakawaambia polisi wa bongo kuwa waachieni wote hakuna suspect hapa, hakuna gaidi anavaa yeboyebo amepauka kwa njaa.hawa ni vibaka tu,IGP akaambiwa u know anything about terrorism?

Jamaa wakaingia chimbo wakaomba akaunti za wafanyabiashara na vionhozi wote wa kisiasa na wanaharakati ambao wameingiziwa mpunga mrefu ndani ya miezi kadhaa (sikumbuki) Thomas Lyimo mfanyabiashara aliyekuwa na garage yake Kimara bucha na vibanda vya maziwa Dar nzima enzi hizo akajikuta matatani, ni baada ya kuonekana akaunti yake iliingiziwa pesa hazina maelezo, kipindi hicho sheria ya money laundering haijatungwa.

Kufustilia kwa kina ni kweli bomu lililolipua ubalozi liliunganishiwa kimara kwenye garage yake.

Hayo yakifanyika mastermind alikuwa kijana mdogo toka Zanzibar Ahmed Khalfan Ghailan ndie alimuingizia huo mpunga kabla ya kukimbilia Nairobi na uarabuni.alikuwa kijana mfogo tu wa miaka 24 au 25, kwa sasa bwana Ghailan ni mtu mzima sasa anakaribia miaka 50 yuko Guantanamo Bay Camp chini ya ilinzi mkali.

Huwapendi USA ila una vingi vya kujifunza kwao

OKW BOBAN SUNZU
Nawakubali sana hawa jamaa
 
Karakana yake aliendelea nayo baada ya kuachiwa?
Upo sahihi FBI walianza kwa kunusa boza la maji lilobeba bomu. Wakagundua vitu viwili. Modification iliyofanywa kwenye Boza kuweza kubeba bomu la uzito ule, Aina ya vyuma vilivyotumika, aina ya kilipuzi (baruti) iliyotumika.
Kujulikana kwamambo hayakulisababisha usadisi juu ya Karakana gani yenye vyuma na uwezo wa kukata vyuma vikubwa na kutengeneza carriage ya lile bobu, Duka gani lenye uwezo wa kuuza Fertilizer ya ujazo ule na kwa sababu vyuma vilionyesha kukatwa kwa gesi ni wapi gesi hiyo inapatikana.
Hapo ndipo Karakana ya uncle Thomas (mtengenezaji wa trailers za malori) akawa mshukiwa kwa sababu hapakuwa na Karakana kubwa binafsi ya kuunga vyuma zaidi yake. Katika mahojiano alipatika fundi aliyefanya kazi ile kwa maelekezo ya mtuhumiwa wa ugaidi bila yeye kujua nini kazi ya kitu anacho tengezeza. Risiti za TOL na Fertilizer zikathibitisha Thomas na gaidi ndio wanunuzi wakubwa ktk kipindi hicho.
 
New York

JINSI MTUHUMIWA ALIVYONASWA

Makabrasha ya ushahidi uliowakilishwa mbele ya korti na waendesha mashataka wa U.S. Attorney for the Southern District of New York kesi ya Ahmed Khalfan Ghailani

Gari ya kijapani ya mvuvi wa pweza iliyokuwa na mfumo wa barafu kutunza mazao ya uvuvi yasiharibike ilinunuliwa kwa noti za Marekani cash zilizochoka kisha ilipelekwa gereji Kimara kufanyiwa modification bila mwenye gereji kujua njama hizo.

Mtuhumiwa Ahmed Khalfan Ghailani alikuwa akitumia usafiri wa baiskeli kusafiri toka kwenye nyumba kitongoji cha Magomeni kwenda mjini na kurudi kwa ajili ya mipango yake miovu.

Mtuhumiwa alikuwa anajivika hali ya unyonge kila akiwasili na baiskeli yake ktk hoteli moja alipokuwa akikutana na aliowaita wageni zake waliokula njama naye. Picha ya unyonge aliyojivika Ahmed Khalfan Ghailani ni kila mara kusisitiza kuwaambia mlinzi na watu waliokaa kijiweni nje ya hoteli kumtizamia baiskeli yake iliyochoka aliyoacha nje isiibiwe na vibaka wa Mnazi Mmoja DSM

FBI walifika baadaye baada ya tukio na kuipata nyumba iliyokuwa inatumika kutengeneza vilipuzi. FBI waliondoka na mazulia pamoja na rangi iliyokwangulia toka vyumba vya nyumba ya Magomeni. Vitu hivyo viliyokuwa na mabaki ya kemikali hivyo vyote vikuwa ni sehemu ya vithibiti vya uhusika njama hiyo mbaya ovu.

WaTanzania kadhaa wasio na hatia lakini walikumbana na wapanga njama bila kujua walichukuliwa mpaka Marekani kutoa ushahidi upande wa mwendesha mashtaka wa Marekani kuhusu tukio hilo baya la ugaidi.

Kesi hii imehifadhiwa mtandaoni na waweza kuisoma yenye mamia ya kurasa ili kuweza kuona umahiri wa uchunguzi uliofanyika na hatimaye Ghailani kukamatwa Afrika ya Kusini akiwa na kazi ya mkanda mikate katika bekari moja ya kuoka mikate Afrika ya kusini baada ya kukimbilia huko.....

Maafisa wa FBI walifika mjini Cape Town South Africa ofisi ya uhamiaji baada ya fununu kutoka wasiri wao kuwa wafike kuomba kupatiwa majina ya watu waliowasili kuomba ukaazi au ukimbizi kabla kidogo na baada ya August 1998 ndipo waliona alama za dole gumba zinazoshabiana na zilizochukuliwa ktk nyumba ya Magomeni DSM, hoteli ya Mnazi Mmoja pia sehemu zingine na picha ya mtuhumiwa akiwa amejiandikisha ukimbizi kwa jina la bandia kwa ajili ya kupatiwa hadhi ya ukimbizi wa kisiasa ....

FBI wakaambiwa wamsubiri atafika kuripoti ofisi ya uhamiaji ya Afrika ya Kusini kama yalivyo masharti ya wanaoomba hifadhi kuwa lazima kila mwezi wawe wanaripoti ili waendelee kutafutiwa hifadhi ya kudumu waliyoomba ya ukimbizi.

Siku ya miadi ya kuripoti Ghailani alifika ofisi za uhamiaji Cape Town na kuzuiliwa na vyombo vya usalama vya Afrika ya Kusini na kuanza kuhojiwa kwanini ametumia jina bandia huku pia vyombo vya usalama vya Marekani maofisa wao wakisikiliza utetezi za Ghailani

Alipobaini kuwa maji yapo shingoni South Afrika, Ghailani alijaribu kutumia mfumo wa haki jamii wa Afrika ya Kusini asisombwe kwa deportation kwenda Marekani kusomewa mashtaka yake , hata hivyo ilishindikana na hivyo akapakiwa ktk ndege baada ya kurupushani za wanasheria ktk korti za Afrika ya Kusini ... soma hapa :
Justia Law
https://law.justia.com › district-courts
United States v. Bin Laden, 156 F. Supp. 2d 359 (S.D.N.Y. 2001)

Even the extradition treaty in force at the time of the arrest and deportation of Khalfan Mohamed did not allow the South African.....



New York

Ahmed Khalfan Ghailani Found Guilty in Manhattan Federal Court of Conspiring in the 1998 Destruction of United States Embassies in East Africa Resulting in Death​

Al Qaeda Terrorist and First Guantanamo Detainee to be Tried in Civilian Court Faces Possible Life Sentence in January​

U.S. Attorney’s OfficeNovember 17, 2010
  • Southern District of New York(212) 637-2600

U.S. Attorney for the Southern District of New York Preet Bharara announced that Ahmed Khalfan Ghailani was found guilty today for his role in the 1998 bombings of the U.S. Embassies in Kenya and Tanzania that took the lives of 224 people, including 12 Americans. Ghailani, 36, a Tanzanian national, and the first detainee held at the Guantanamo Bay Naval Base in Cuba to be tried in a civilian court, was found guilty of conspiring to destroy property and buildings of the United States, following a five-week trial before U.S. District Judge Lewis A. Kaplan. Ghailani faces a mandatory minimum sentence of 20 years in prison and a maximum sentence of life on this count. Ghailani was acquitted of the remaining counts against him.
“Ahmed Ghailani was today convicted of conspiring in the 1998 destruction of the United States Embassies in Kenya and Tanzania, causing death as a result,” said U.S. Attorney Preet Bharara. “He will face, and we will seek, the maximum sentence of life without parole when he is sentenced in January. I want to express my deep appreciation for the unflagging commitment, dedication and talent of the agents who so thoroughly investigated this case and the prosecutors who so ably tried it.”
According to the evidence presented at trial, previous court proceedings in this case, and documents filed in Manhattan federal court:
Ghailani was first indicted on Dec.16, 1998, by a federal grand jury in the Southern District of New York. In that indictment and subsequent superseding indictments, Ghailani was charged with conspiring with Usama Bin Laden and other members of al Qaeda to kill American nationals and with several related crimes in connection with the twin bombings of Aug. 7, 1998, that destroyed the American Embassies in Nairobi, Kenya and Dar es Salaam, Tanzania. Ghailani was also charged with 224 individual murder counts for each of the victims of the two embassy bombings.
The evidence at trial showed, among other things, that each of the embassies was attacked by suicide bombers driving large truck bombs packed with approximately 1,000 pounds of TNT. Ghailani purchased the truck as well as tanks of oxygen and acetylene gas that were used in the bombing of the U.S. Embassy in Tanzania. He also stored explosive detonators that were used in the bomb at his residence.
The evidence also showed that the day before the bombings, using a fake passport in an assumed name, Ghailani flew from Nairobi, Kenya to Pakistan in a coordinated escape from Africa. Two other al Qaeda operatives, a senior operations leader and an explosives expert who had traveled between Kenya and Tanzania in the weeks before the bombings departed Africa for Pakistan on the same flight as Ghailani. Those operatives were also involved with the bombings.
Ghailani is scheduled to be sentenced on Jan. 25, 2011, at 11:00 a.m. EST.
Mr. Bharara praised the FBI and the National Security Division of the U.S. Department of Justice for their extraordinary work in the investigation of this case. He also thanked the Tanzanian Police for their assistance in the case.
This case is being handled by the Office's Terrorism and International Narcotics Unit with assistance from the Justice Department’s National Security Division. Assistant U.S. Attorneys Michael Farbiarz, Harry A. Chernoff, Nicholas Lewin and Sean S. Buckley are in charge of the prosecution

This content has been reproduced from its original source.
Mkuu
Sikuwahi, kusoma hii stori na hii ni mara yangu ya kwanza, na sikujua kuwa kuna watanzania walikamatwa kwenye hii kesi.
Ikabidi niingie google kutafuta story yote, sio mchezo, nikapata mpaka hata mipango ya kigaidi ilyofanyika upande wa Kenya, na pia Tanzania, yaani ni maelezo yote mpaka siku ya tukio,na pia jinsi gani mission zote zilitibuliwa kwenye siku ya tukio, ambapo kwa Tanzani walitaka lile lori liingie,ndani kabisa,lakini kitete chao, mmoja alitakiwa kushuka na bastola aende kwneye geti kumuamrisha mlinzi afungue,lakini alivyoshuka akasahau bastola kwenye jacket ndani ya lori, ikabidi atoe stun grenade, alivyotupa, akasanua mpaka mission yote, ikabidi mwenzake aliyebaki ndani ya lori kuamua kulipua,
Na pia yule mmoja wao kwa upande wa Kenya, ambaye alitakiwa pia ajitoe mhanga, lakini alivyoshuka kuelekea kwenye ubalozi mwenzake kitete chake akalipua, lakini yeye alijeruhiwa na sasa hapo ndio akawa kila anakoenda anaacha traces ilimfanya kukamatwa. sababu alianzakuwapigia simu wenzake Pakistani, kuomba atumiwe passport na hela ya nauli, wanamshangaa wakati walitegemea na yeye ajitoe mhanga mbona yupo hai.

Sasa kwa hawa watanzania, kulikuwa na Khalfan Khamis Mohamed na Ahmed Khalfan Ghailan
Khalfan Khamis Mohamed ndio aliye kamatwa South Africa na huyu mwingine Ahmed Khalfan Ghailan,yeye alikamatwa Pakistani mnamo 2004



 
Back
Top Bottom