FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu


Naomba link ya hiyo story ya aliekamatwa kama hutajali
 
Rekodi
 
Ni kazi ya ujasusi. Marekani wana majasusi kila sehemu. Na hapa nazungumzia majasusi wale ambao ni sehemu ya hivyo vikundi vya kigaidi. Kwa mfano wanaweza ''kumtongoza'' mjahidina wa Al Shabab, wakampa fedha ndefu, wakamwambia endelee kuishi kwenye hilo kundi huku akijifanya ni mwenzao ili achukuwe siri na mikakati yao. Siri wanazozipata mara kwa mara ndiyo zinasaidia kutoa maonyo kama hayo.
 
Hapo tutatofautiana mkuu. Mchaga yesu ni utamaduni tu mbele ya hela hela iko mwanzo.
Wachaga wengi wenye maduka (Kwa mangi) wana redio iko tuned Radio Maria muda wote unaweza sema utakatifu ndio huu sasa, cha ajabu ktk kila kilo moja ya unga, mchele, sukari na mafuta ya kupikia lazima anapiga kiasi fulani na hicho anachopiga ndio anakula yeye unakuta mara nyingi wanapikia humohumo dukani. Kingine ana uza tena kupata hela ya vitunguu, nyanya, ndizi na nyama.

Achana na kina Mangi aisee....[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sheria na taratibu nyingi sana viwanja za ndege zimewekwa na kubadilishwa baada ya matukio ya kigaidi!
 
Nawakubali sana hawa jamaa
 
Karakana yake aliendelea nayo baada ya kuachiwa?
 
Mkuu
Sikuwahi, kusoma hii stori na hii ni mara yangu ya kwanza, na sikujua kuwa kuna watanzania walikamatwa kwenye hii kesi.
Ikabidi niingie google kutafuta story yote, sio mchezo, nikapata mpaka hata mipango ya kigaidi ilyofanyika upande wa Kenya, na pia Tanzania, yaani ni maelezo yote mpaka siku ya tukio,na pia jinsi gani mission zote zilitibuliwa kwenye siku ya tukio, ambapo kwa Tanzani walitaka lile lori liingie,ndani kabisa,lakini kitete chao, mmoja alitakiwa kushuka na bastola aende kwneye geti kumuamrisha mlinzi afungue,lakini alivyoshuka akasahau bastola kwenye jacket ndani ya lori, ikabidi atoe stun grenade, alivyotupa, akasanua mpaka mission yote, ikabidi mwenzake aliyebaki ndani ya lori kuamua kulipua,
Na pia yule mmoja wao kwa upande wa Kenya, ambaye alitakiwa pia ajitoe mhanga, lakini alivyoshuka kuelekea kwenye ubalozi mwenzake kitete chake akalipua, lakini yeye alijeruhiwa na sasa hapo ndio akawa kila anakoenda anaacha traces ilimfanya kukamatwa. sababu alianzakuwapigia simu wenzake Pakistani, kuomba atumiwe passport na hela ya nauli, wanamshangaa wakati walitegemea na yeye ajitoe mhanga mbona yupo hai.

Sasa kwa hawa watanzania, kulikuwa na Khalfan Khamis Mohamed na Ahmed Khalfan Ghailan
Khalfan Khamis Mohamed ndio aliye kamatwa South Africa na huyu mwingine Ahmed Khalfan Ghailan,yeye alikamatwa Pakistani mnamo 2004



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…