Unajua kwanini Luis Enrique anaondoka ?sababu flavour ya Barca imepotea pressing,kutawala mchezo nk
Luis Enrique timu yake inacheza pass nyuma sana possession ipo kwenye defence akitegemea kucheza counter akiwategemea MSN
Mechi ya juzi na ATM tumeona ATM wakifanya pressing na kiungo cha Barca kilielemewa na hata ule ushindi wa Barca ni wa bahati tu
Timu nyingi zilizofanya pressing zimeisumbua Barca Tizama mechi na Betis ,Celta Vigo,Villarreal ,sevilla ,PSG nk nk
Wakati Barca ilikuwa ndio timu inayofanya high pressing ila saizi haifanyi ndio maana kiungo cha Barca haswa msimu huu kipo hovyo
Barca imefanya vizuri chini ya Luis Enrique shukran kwa MSN sababu huwa counter zinazigharibu timu zifanyao press Lakini msimu huu Barca kapoteza points nyingi kwa timu za aina hiyo au mfano mzuri mechi ya marudiano dhidi ya man city Barca haikuendana na pressure ya city
Tuseme ukweli Luis kafanya kazi nzuri ila midfield imekuwa hovyo akicheza na timu zinazo press ,
Barca ya kufanya pressing mwisho wake ulikuwa kipindi cha Tito na Tata kidogo
Barca hii haina pressing kabisa