FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Jmos naanza kampeni yakuitoa PSG nitakuja na historia fupi ya strenth ambazo tunazo na potentials camp Nou [HASHTAG]#ibelieveinbarca[/HASHTAG] and we believe in treble [HASHTAG]#forcabarca[/HASHTAG] tutawajua tu washabiki wa kweli mwaka huu
 
kuna pressing inatisha duniani kama ya Barca?ni stle tu ya uchezaji tukiamua kwani AT last week amekufa vipi?halafu hamna timu iko flexible kama Barca ,hizo pressing ndio zilimpa ujik Louis Enrique Barca na kumbuka wachezaji ni wale wale

Unajua kwanini Luis Enrique anaondoka ?sababu flavour ya Barca imepotea pressing,kutawala mchezo nk

Luis Enrique timu yake inacheza pass nyuma sana possession ipo kwenye defence akitegemea kucheza counter akiwategemea MSN

Mechi ya juzi na ATM tumeona ATM wakifanya pressing na kiungo cha Barca kilielemewa na hata ule ushindi wa Barca ni wa bahati tu

Timu nyingi zilizofanya pressing zimeisumbua Barca Tizama mechi na Betis ,Celta Vigo,Villarreal ,sevilla ,PSG nk nk

Wakati Barca ilikuwa ndio timu inayofanya high pressing ila saizi haifanyi ndio maana kiungo cha Barca haswa msimu huu kipo hovyo

Barca imefanya vizuri chini ya Luis Enrique shukran kwa MSN sababu huwa counter zinazigharibu timu zifanyao press Lakini msimu huu Barca kapoteza points nyingi kwa timu za aina hiyo au mfano mzuri mechi ya marudiano dhidi ya man city Barca haikuendana na pressure ya city

Tuseme ukweli Luis kafanya kazi nzuri ila midfield imekuwa hovyo akicheza na timu zinazo press ,

Barca ya kufanya pressing mwisho wake ulikuwa kipindi cha Tito na Tata kidogo

Barca hii haina pressing kabisa
 
Sijakusoma kabisa hasa ulivyomalizia ,Enrique ndio kaipa Barca Treble na ushindi wa laliga kila mwaka tangu ameichukua team kwa tick tack na ku press ,ninachokifahamu msimu huu alisema atakua unpredictable which means atakua na mchanganyiko wa flavor nyingi iys not the case may be enzi zake zimeisha
 
Tatizo siyo kikosi kikubwa tatizo mtaiweza pressing ya celta

Maana Barca ya sasa ikicheza na timu inayofanya high pressing wanapata tabu sana mpaka unawaonea huruma ,na celta inaisumbua Barca Mara nyingi sababu ya pressing yao
Tupo nyumbani Mkuu, huyo bwana hawezi chomoka Camp Nou.
 
Jmos naanza kampeni yakuitoa PSG nitakuja na historia fupi ya strenth ambazo tunazo na potentials camp Nou [HASHTAG]#ibelieveinbarca[/HASHTAG] and we believe in treble [HASHTAG]#forcabarca[/HASHTAG] tutawajua tu washabiki wa kweli mwaka huu
Kikosi kilichocheza jana ndicho nachopendekeza kicheze dhidi ya PsG, tena tutumie hiyohiyo 3-4-3 ila Rafinha asianze.
 
Nimeshakupa LIKE yako!

Ni dhahiri kabisa timu haina radha kama miaka iliyopita. Viungo ni kama havipo uwanjani. Nilisikitika saana kuondoka kwa yule mtoto Thiago Alcantara, alikuwa ni mbadala mzuri wa Xavi Hernandez.

Timu inahitaji viungo ambao tunajua wanaweza wakachezesha timu, mimi kuanzia hata msimu ujao sitapenda kumuona Andrea Iniesta anaanza kikosi cha kwanza. Watafutwe vijana wapya ili kuinua hii sehemu ya viungo.

Game ya Atletico hatukufanya vyema, na hii weakness ya viungo ilionekana tangu last year. Inabidi tulipatie ufumbuzi jambo hili.
 
Tatizo siyo kikosi kikubwa tatizo mtaiweza pressing ya celta

Maana Barca ya sasa ikicheza na timu inayofanya high pressing wanapata tabu sana mpaka unawaonea huruma ,na celta inaisumbua Barca Mara nyingi sababu ya pressing yao
Wakiwa kwao sio camp nou
 
Kitu pekee Enrique alichofanya ni kutupa washambuliaji wazuri ila Enrique sio mwalimu mzuri kama akina Pep, Anceloti, Zidane n.k

Kama ulikuwa unaifatilia Barca vyema utagundua kwamba zama za Enrique viungo wamekuwa hawana msaada mkubwa sana kwa timu tukicheza na timu kubwa. Ile radha ya timu haipo kabisa.
 
Zidane? Mkuu uko serious na hilo jina?
 
Mkuu tuombe iwe hvyo lkn watu wenyewe tunawatoa wapi sasa? Hiyo ndio shida kubwa
 
Ukubali au ukatae ila jamaa ni mwalimu.
Mzee wa ''comeback'' kikosi tu kinambeba. hana tofauti na Enrique. Anamng'ang'ania Benzema kama Enrique na Gomes. Hana ualimu wowote.
 
kuna pressing inatisha duniani kama ya Barca?ni stle tu ya uchezaji tukiamua kwani AT last week amekufa vipi?halafu hamna timu iko flexible kama Barca ,hizo pressing ndio zilimpa ujik Louis Enrique Barca na kumbuka wachezaji ni wale wale
Lini Barca ya Enrique inacheza pressing ?

Kitu alichofanikiwa Lucho ni kutengeneza mfumo uliweza kuwa-accomodate MSN na wote wakacheza vizuri na hao ndio walikuwa key kwenye mafanikio ya timu tofauti na kina Pep ambao walitengeneza timu kwenye kiungo (Busquets,Iniesta na Xavi) huwezi linganisha na hawa kina Gomes,(Busquets na Iniesta now wameshachoka).Rosell/Batromeu walifanya kosa kubwa kumuuza Thiago na kumuacha Fabregas na wakazembea kumsajili Kroos ambaye angefit kwenye mfumo wao
 
Iniesta kabla ya kuumia alikuwa fresh tatizo Enrique mfumo wake wa kuiweka timu chini na kutegemea MSN

343 ya juzi kumbuka sporting alikuwa anapaki basi na viungo kama Rakitic,Gomes footwork yao sio nzuri ,mistake ambayo bodi ya Barca ilifanya ni kumuuza Thiago
Ndio alipaswa achukue mikoba ya xavi

Kingine Barca ya pep na Tito ikipoteza mpira ndani ya sekunde kadhaa wanarudisha kwenye himaya yao sababu wana press kwa nguvu ,kitu ambacho kwasasa hakuna


Ndio maana sampaoli anatajwa sababu ya aina yake ya uchezaji


Game ijayo ajitoe mhanga 343 na messi,iniesta waperform kwa hali ya juu

Busi,iniesta,raki ,denis/Alba
 

Kipigo cha mabao 4 kwa 0 toka kwa PSG kiliamsha hisia tofauti kwa mashabiki wa Barcelona.Wengi walifedheheshwa sana na kipigo hicho cha aibu.Swalu kubwa limekuja kuhusu uwezo wa kocha wa Barcelona Luis Enrique,je ana uwezo sahihi kuwa kocha wa Barcelona.Wengi wameonekana kutokukubaliana na uwezo wake.Ushindi wa dakika za lala salama dhidi ya Athletico Madrid ulitilia shaka kuhusu uwezo wa Enrique na japo mpira unadunda lakini kuna asilimia kubwa kwamba Barcelona wameshachungulia mlango wa kutoke UEFA.


Jorge Sampaoli kocha wa Sevilla amekuwa gumzo sana katika ligi ya Hispania.Uwezo wa Sampaoli umewashtua wengi kwani hadi sasa Sampaoli yuko katika mbio moja na Real Madrid na Barcelona wote wanataka ubingwa.Uwezo wake mkubwa umemfanya ahusishwe sana na kujiunga na klabu ya Barcelona.Miaka kadhaa iliyopita alitajwa miongoni mwa makocha watatu bora duniani.Sampaoli ni kama anaudai mpira kwa kuwa akiwa na miaka 19 tu alilizimika kuacha kucheza soka baada ya kuvunjwa miguu yote miwili.Kwanini Sampaoli na sii mwingine?

AINA YA MPIRA.Sampaoli anapenda kushambulia,ni aina ya kocha ambaye mara zote na timu zote anazofundisha huwa anashambulia tu.Toka enzi za “Dream Team” ambapo ni jina la timu ya Barcelona ililopewa kipindi inafundishwa na Johan Cryuf hadi hivi leo zama za Enrique,Barcelona hawakai nyuma wamekuwa timu ya kushambulia mwanzo mwisho.Mchezo wa kwanza wa Sampaoli La Liga ilikuwa dhidi ya Espanyol na waliwafunga bao 6 kwa 4,mechi hii ilikuwa ushahidi tosha wa aina ya mbinu za Sampaoli.Alipokuwa Chile alionekana kuwaunganisha Artulo Vidal,Edurdo Vargas na Alexis Sanchez kutengeneza kikosi ambacho kilionekana na safu ya ushambuliaji hatari sana kombe la dunia.Mfumo wake wa 3-4-3 ni kati ya mbinu inayowapa tabu sana wapinzani wake.Ni mtu sahihi kabisa kuwa kocha wa MSN.

UNYUMBULIKO WA MBINU.Moja kati ya matatizo makubwa ya Luis Enrique ni kukosa Plan B.Mara nyingi ambazo mbinu zake zinashikwa na wapinzani huwa anabaki kama mtu asiyejua ni nin afanye.Sampaoli amwonekana na mbinu mpya kila siku,kama umebahatika kuwaona Sevilla unaweza kushudia anavyomtumia Samir Nasri na Steven N’zonzi.Nasri amekuwa bora sana chini ya Sampaoli huku akicheza nafasi tofauti kutokana na Sampoli anavyotaka.Hatumii tu 3-4-3 bali michezo mikubwa mingi formation hii inaonekanaga kubadilika akicheza 4-3-3 na 4-4-2 pale inapohitajika.

IDEA MPYA ZA SOKA.Unaweza kumuona Lioneil Messi,amekuwa Messi yule yule wa mwaka 2014 akicheza vile vile habadiliki.Barcelona imekwama kimbinu na inahitaji mtu mpyaa kuwapa kitu kipya.Wanachofanya Barcelona leo ndio kilichofanywa miaka kadhaa iliyopita,sitaki kuamini kwamba kipindi chote hicho wapinzani wameshindwa kuona wanachofanya Barcelona.Ni jambo jema kwa timu kuamini katika philosophy yao ya soka,lakini kama philosophy yenu inashindwa kuwapa mutakacho kwanini ing’ang’aniwe?.Barcelona wanataka kuwa tishio tena duniani kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.Sii kwamba Barcelona wanashuka kiwango laa hasha bali wapinzani wanapanda kiwango.Mtu mpya anatakiwa kuja kuwarudisha walipokuwa na ni Jorge Sampaoli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…