FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Man UTD wanahitaji Modric wa Spurs na Sneider wa Inter kama kweli wanataka kuitungua Barca......................wachezaji wa kati hawana vipaji vya kumiliki mpira hata kukaba.......................

Nahisi wewe umecheza mpira............ni kweli kabisa..............hata kijana Anderson jana angekuwa much better than Carrick..........design ya uchezaji wa Barca inataka viungo wakabaji kama Anderson/Owen Hergreaves...........there was too much space for Viungo wa Barca............
 
Yaani barca ni noma hakuna alionyesha kucheza saaana they played as a team na hiki ndicho kilichowachanganya man u,hawakujua nani wa kumdhibiti.

Nampenda sana 'la maquena' the machine.
 


...Kwasasa sidhani kuna master tactician mzuri wa defence kama Mourinho, ambaye pamoja na kuwatumia Lassana Diarra, Alonso et al...bado Barcelona waliweza penetrate.

Jamaa wako kwenye different level,....tusubirie kina Xavi na Iniesta waondoke ndipo tutaona udhaifu wao...Mind you, hao jamaa pia wanaiweka juu Spain National team.
 
Kuna tofauti kati ya mpira wa mdomoni na uwanjani. Wapenzi wa EPL ni kuwatia adabu uwanjani tu
 
fulu jezi next next UEFA final
huu ndio mpira,sio vitete man u na alex
ivi mikono yake ilikumbwa na kifafa gani???:biggrin1:
 


MKuu Jumamosi ishapita, vp una UJASIRI wa kuyarudia haya maneno ?
 
True and real barca fans hii ni thread yenu jisikieni huru . Tuko pamoja kwenye shida na raha . To be number one is easy kama tulivyo fanya na tunaelewa how tough to remain namba one . Kubali kataa hizi ni nyakati za barcelona na si vinginevyo muda wenu utafika mtadominate viva barcelona . One love
 
huuu nikimuona uyu mwanaume nahama kabisa
safi sana guardiola,love every bit of barca

wananipa raha sana,mpira safi
 
Observer badala ya kuanza na neno nikiwa kama mchambuzi uanze na neno nikiwa kama mtabiri, uchukue jukumu la pweza paul, unaonaje hapo mkuu observer.

Mkuu Masuke, mimi sio mtabiri na sijawahi kuwa mtabiri, mimi ni mchambuzi wa soka na ndio maana ninapotoa pre-match analysis huwa natoa vigezo. Mtabiri ni mtu anasema yatakayotokea bila kuwa na kigezo chochote.

Kwa kifupi mimi si mshabiki wa timu yoyote ya nje ya Tanzania, ila ni muangaliaji mkubwa wa ligi za Europe na Amerika ya kusini. Kutokuwa mshabiki ndio kunanifanya ninapotoa vigezo vya mchezo ninakuwa siegemei upande wowote ila naongelea soka zaidi.

Ukisoma vizuri post niliyoituma (Sababu 5 kwanini Barcelona itaifunga Manchester United) utagundua ndio sababu zilizoiangamiza Man U, japo mashabiki wa man U wengi walibisha na kutoa arguments zao lakini baada ya game hakuna anayeweza kubisha tena.

Hapa nataka niongelee point ya tano ambayo nilizungumzia Trio. Kuna mdau aliargue JS Park ndiye angemdhibiti Messi, nilimshangaa sana sana na nikajiuliza uwezo wake wa kuchambua soka kama kweli upo sawa.

Naipaste hapa point ya Trio halafu nitasummarise Trio ilivyoidestroy Man U

Trio
Ofcoz, Trio ni sababu kubwa ya 5 ya Man U kufungwa tarehe 28. Hawa watu watatu wataigharimu sana Man U kuweza kuwadhibiti dakika zote 90 za mchezo. Nionavyo ni kwamba kwa sababu Pep anajua Man U ina ukuta mgumu sana katikati, atakachofanya ataanza kwa kushambulia tokea pembeni huku akiwa hana namba 9. Lionel Messi atacheza deep kama kiungo akiwa anatumika kama virtual centre forward hii itamfanya asiweze kukabwa na Vidic au Ferdinand. Wakati Messi atacheza kama kiungo, David Villa atakuwa anashambulia zaidi kwa kutokea kulia huku Pedro Rodriguez na Andres Iniesta watakuwa wanashambulia tokea kushoto. Hii itawalazimisha Nemanja Vidic na Rio Ferdinand kutanuka pembeni ili kuwasaidia mafullback Patrice Evra na kulia sina akika ataanza Fabio au Raphael, ila binafsi ninaamini akianza John Oshea itakuwa advantage kwa Man U maana yupo physic kuliko mapacha na pia anauwezo mkubwa wa kukaba na kuoverlap. Kutanuka kwa hawa centre defenders kutatoa mwanya kwa Xavi Hernandez na Andres Iniesta kusupply mipira kwa Lionel Messi. Mbinu pekee ambayo itawasaidia Man U kuweza kuwadhibiti hawa Trio ni kuanza kwa kutumia double holding midfielders, Darren Fletcher na Michael Carrick. Sina hakika sana na fitness ya Fletcher kwa ajili ya huo mpambano, maana japokuwa amecheza mechi ya mwishoni mwa msimu lakini bado fitness yake ina mashaka kidogo especially kwa sababu ya ugumu wa mechi yenyewe.

Hapo red ndio nilitegemea Sir AF afanye, kwa maana ya kuongeza idadi ya viungo ili kuwacondense Trio, kutokuwa na viungo wengi katikati kuliwagharimu sana Man U. Hakika ndio maana Sir AF hataki kupoteza muda wa kumsaini super play maker, to me huyu ndiye kiungo mchezesha timu bora zaidi kwa sasa katika ligi ya UK, Luca Modric.
 
Goli la kwanza.

Busquet alimpa Iniesta, Iniesta akampa Xavi, Xavi akapiga killer pass to Pedro, ukiangalia vizuri goli lilivyotokea, wakati Xavi anakokota mpira, Messi akawa anakimbia kuingia katikati, ile kimbia ya Messi ikahamisha concentration ya mabeki wa man U kuelekea kwa Messi na kumuacha Pedro akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga. Xavi akamuona na kutoa pasi kwa Pedro. Goli la kwanza.

Goli la pili.

Iniesta alimpa Xavi akamrudishia Iniesta, Iniesta akampa Messi, Messi alivyochukua akakokota kidogo, mabeki wa Man U wakaduwaa wakidhani Messi atatoa pasi tena kwa maana kabla ya hapo alikuwa hajajaribu long shot hata moja, Messi akaona hiyo opportunity akapiga shuti la mbali, goli la pili.

Goli la tatu

Messi akaingia kwa spidi ndani ya 18 akiwaacha wachezaji wa Man U, wakati anampa Sergio Busquet mpira ukababatiza mabeki wa Man U na kumkuta Busquet, Busquet akampa David Villa, Villa akachip kwenye nyuzi 90, goli la tatu.

Ukiangalia kwa umakini hayo magoli matatu, wachezaji wa Barcelona kuanzia namba 6 mpaka 11 wote wamehusika kwenye hayo magoli matatu. Kama sio kufunga (Pedro, Messi na Villa) basi wamepiga pasi za mwisho (Xavi, Iniesta, Busquet). Hii inadhihirisha hawa jamaa walivyo bora zaidi. It is a complete best team in the world.
 
Ulikuwa ni uchambuzi mzuri, mkuu kama utaendelea hivi hivi napenda nikushauri utafute kituo cha tv au redio ili ujiongezee kipato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…