Mkuu Masuke, mimi sio mtabiri na sijawahi kuwa mtabiri, mimi ni mchambuzi wa soka na ndio maana ninapotoa pre-match analysis huwa natoa vigezo. Mtabiri ni mtu anasema yatakayotokea bila kuwa na kigezo chochote.
Kwa kifupi mimi si mshabiki wa timu yoyote ya nje ya Tanzania, ila ni muangaliaji mkubwa wa ligi za Europe na Amerika ya kusini. Kutokuwa mshabiki ndio kunanifanya ninapotoa vigezo vya mchezo ninakuwa siegemei upande wowote ila naongelea soka zaidi.
Ukisoma vizuri post niliyoituma (Sababu 5 kwanini Barcelona itaifunga Manchester United) utagundua ndio sababu zilizoiangamiza Man U, japo mashabiki wa man U wengi walibisha na kutoa arguments zao lakini baada ya game hakuna anayeweza kubisha tena.
Hapa nataka niongelee point ya tano ambayo nilizungumzia Trio. Kuna mdau aliargue JS Park ndiye angemdhibiti Messi, nilimshangaa sana sana na nikajiuliza uwezo wake wa kuchambua soka kama kweli upo sawa.
Naipaste hapa point ya Trio halafu nitasummarise Trio ilivyoidestroy Man U
Trio
Ofcoz, Trio ni sababu kubwa ya 5 ya Man U kufungwa tarehe 28. Hawa watu watatu wataigharimu sana Man U kuweza kuwadhibiti dakika zote 90 za mchezo. Nionavyo ni kwamba kwa sababu Pep anajua Man U ina ukuta mgumu sana katikati, atakachofanya ataanza kwa kushambulia tokea pembeni huku akiwa hana namba 9. Lionel Messi atacheza deep kama kiungo akiwa anatumika kama virtual centre forward hii itamfanya asiweze kukabwa na Vidic au Ferdinand. Wakati Messi atacheza kama kiungo, David Villa atakuwa anashambulia zaidi kwa kutokea kulia huku Pedro Rodriguez na Andres Iniesta watakuwa wanashambulia tokea kushoto. Hii itawalazimisha Nemanja Vidic na Rio Ferdinand kutanuka pembeni ili kuwasaidia mafullback Patrice Evra na kulia sina akika ataanza Fabio au Raphael, ila binafsi ninaamini akianza John Oshea itakuwa advantage kwa Man U maana yupo physic kuliko mapacha na pia anauwezo mkubwa wa kukaba na kuoverlap. Kutanuka kwa hawa centre defenders kutatoa mwanya kwa Xavi Hernandez na Andres Iniesta kusupply mipira kwa Lionel Messi. Mbinu pekee ambayo itawasaidia Man U kuweza kuwadhibiti hawa Trio ni kuanza kwa kutumia double holding midfielders, Darren Fletcher na Michael Carrick. Sina hakika sana na fitness ya Fletcher kwa ajili ya huo mpambano, maana japokuwa amecheza mechi ya mwishoni mwa msimu lakini bado fitness yake ina mashaka kidogo especially kwa sababu ya ugumu wa mechi yenyewe.
Hapo red ndio nilitegemea Sir AF afanye, kwa maana ya kuongeza idadi ya viungo ili kuwacondense Trio, kutokuwa na viungo wengi katikati kuliwagharimu sana Man U. Hakika ndio maana Sir AF hataki kupoteza muda wa kumsaini super play maker, to me huyu ndiye kiungo mchezesha timu bora zaidi kwa sasa katika ligi ya UK, Luca Modric.