FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Guardiola asherekea ushindi wa Barcelona


Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameipongeza klabu yake ya zamani Barcelona kwa ushindi wao wa jumla ya magoli 6-5 PSG kwenye michuano ya Champions League usiku wa Jumatano March 8, 2017.

Neymar akiwa kwenye kiwango cha juu aliisaidia Barcelona kufanya kisichowezekana kuwa kinawezekana, Mbrazil huyo alifunga mara mbili katika harakati za kupindua matokeo ya kipigo cha magoli 4-0 kwenye mechi ya kwanza kwa style ya aina yake baada ya goli la ushindi la Sergi Roberto dakika za mwisho.

Guardiola alishinda taji la Champions League mara mbili akiwa na kikosi cha Barca msimu wa 2008-9 na 2010-11 lakini hakuweza kuushuhudia mchezo huo uliomalizka kwa Barca kushinda 6-1 kwa sababu alikuwa anaisimamia timu yake ya Man City kwenye mchezo wa Premier League dhidi ya Stoke City.

“Napenda kuwapongeza Barcelona ni matokeo yanayoshangaza sana,” alisema Guardiola baada ya timu yake kulazimishwa suluhu kwenye uwanja wao wa nyumbani ili kupunguza gape la pointi dhidi ya Chelsea.

“Inashangaza na ninasherekea matokeo haya hususan kwa ajili ya Luis Enrique. Lakini pia na kizazi hiki cha wachezaji, ambao wanafanya vitu vingi vizuri. Natamani kuona mechi hiyo kwenye marudio kwa utulivu nikipata muda.”
 
Rekodi 3 zilizovunjwa na Barcelona baada ya kuishangaza Dunia ya soka


Kilichotokea pale Nou Camp usiku wa Jumatano March 8, 2017 ilikuwa ni historia kwenye mchezo wa marudiano katika michuano ya Champions League ambayo imevunja rekodi ya muda wote iliyokuwa inashikiliwa na Deportivo dhidi ya mabingwa wa zamani wa michuano hiyo AC Milan mwaka 2004.

Mchezo wa kwanza Deportivo ililala kwa bao 4-1 ikiwa ni hatua ya robo fainali lakini wakafanikiwa kuongoza kwa goli 3-0, zikiwa zimesalia dakika 14 huku aggregate ikisoma 5-4, Fran akafunga goli la nne kwa Deportivo usiku huo.

Mechi za raundi ya kwanza ambazo zilimalizika kwa magoli timu kuongoza kwa magoli manne kwenye michuano ya UEFA lakini matokeo yakabageuka kwenye mechi ya marudiano:

Borussia Monchengladbach v Real Madrid (1985-86 Uefa Cup)
Real waliikaribisha Borussia Monchengladbach kwenye mchezo wa marudiano katika raundi tatu ya Uefa Cup baada ya miamba hiyo ya Ujerumani kushinda 5-1 kwenye mchezo wao wa nyumbani lakini Madrid wakaweza kutengua matokeo kwa kupata ushindi wa magoli 4-0 na kufuzu hatua ya nane bora.

Leixoes v La Chaux-de-Fonds (1961-61 Cup Winners’ Cup)
Leixoes walikuwa wamechapwa 6-2 huko La Chaux-de-Fonds, lakini mabingwa hao wa zamani wa Uswis walishinda 5-0 kwenye uwanja wao wa Estádio do Mar na kusonga mbele kwenye mashindano.

Partizan v QPR (1984-85 Uefa Cup)
QPR ilishinda 6-2 kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Highbury kwa sababu uwanja wao wa Loftus Road ulikuwa wa nyasi za plastic, lakini wakapoteza game ya pili kwa kipigo cha magoli 4-0 kwenye uwanja wa Belgrade na kutupwa nje ya mashindano kwa sheria ya goli la ugenini.
 
5 bora ya comeback zilizowahi kutokea kwenye Champions League.


Mechi kati ya Barcelona na PSG imeingia kwenye rekodi za Champions League.Barcelona inakuwa timu ya kwanza kufungwa bao 4 kwa 0 katika mchezo wa kwanza lakini baadae kupindua matoke.Ifuatayo ni orodha ya mechi 5 katika Chapions League ambazo timu zilipindua matokeo yasiyotarajiwa.

BARCELONA VS PSG – 2017.
Hii ni mechi ya karibu na ndiyo ambayo kwa sasa kila mtu anaizungumzia.Ni jambo ambalo lilionekana haliwezekani kabisa, katika mchezo wa kwanza pale Ufaransa PSG waliwafunga Barcelona goli 4 kwa sifuri na hii ilionesha wazi mchezo ungeishia hapo.

Tofauti na wengi walivyofikiria, Barcelona waliwasubiri PSG uwanjani kwao huku kocha wao akisema wanaweza kuwafunga 6 Barcelona,wengi waliona Enrique anaota. PSG walifika Nou Camp na matumaini kibao lakini ikawakuta fedheha na maneno ya Enrique yakatimia Barca wanamfunga PSG 6 na kuaonga katika hatua inayofuata ya Champions League.

2. MONACO VS REAL MADRID – 2004

Wakiwa uwanjani kwao Santiago Bernabeu,Real Madrid waliwapiga Monaco katika mchezo wa kwanza kwa jumla ya magoli 4 kwa 2.

Walipoenda Ufaransa,Raul Gonzalez aliwapatia Madrid goli la ugenini ni ikawa aggeregate ya 5 kwa 2. Dakika 10 baada ya goli la Raul, Monaco walipata goli kabla ya Fernando Morientes aliyekuwa Monaco kufunga lingine na baadae Guilly nae aliwafungia Monaco na hadi mwisho wa mchezo Monaco waliibuka kidedea na ushindi wa magoli 3 kwa 1 na wakafuzu kwa faida ya goli la ugenini.

3. DERPOTIVO VS AC MILLAN – 2004Mch

ezo wa kwanza katika uwanja wa nyumbani wa Ac Millan almanusra itokee kilichomtokea Barcelona lakini Deportivo walipata goli moja na mechi yao ya kwanza kuisha kwa kipigo cha goli 4 kwa 1.

Baadae Ac Millan waliwafuata Deportivo hapo ndipo balaa liliwakuta. Magoli ya Walter Pandiani, Carlos Verlon na Albert Leaque yaliipeleka Deportivo mapumziko wakiongoza goli 3 kwa 0. Kipindi cha pili Gonzalez Fran aliipatia Deportivo goli la 4 na mechi kuisha kwa aggregate ya 5 kwa 4.

4. CHELSEA VS NAPOLI – 2012

Wakiwa chini ya kocha wao Andre Villas Boas Chelsea walikubali kipigo cha bao 3 kwa 1 kutoka Napoli katika mchezo wa kwanza Italia lakini Chelsea hao hao mechi iliyofuata ya ligi walifungwa na West Bromich ndipo Boas alipotimuliwa na nafasi yake ikichukuliwa na Di Matteo wakati wakiisubiri mechi ya pili na Napoli.

Wakiwa na kocha mpya Di Matteo Chelsea waliikaribisha Napoli Stamford Bridge.

Magoli ya dakika 90 za mwanzo kutoka John Terry,Frank Lampard na Didier Drogba yaliufanya mchezo uende “xtra time”.

Katika dakika hizo za nyongeza Ivanovic alifunga goli dakika ya 104 na mechi na kuifanya Chelsea kufudhu kwa kushinda 4-3.

5. AC MILAN VS LIVERPOOL – 2005

Hii ni mechi ambayo hakuna shabiki wa Liverpool aneisahau. Lakini tofauti na hizo mechi nyingine hii ilikuwa ni fainali kwa hiyo ilikuwa mechi moja tu. Kipindi cha kwanza kilishuhudia Ac Millan wakiifunga Liverpool magoli matatu na ni wazi wakawa na nafasi kubwa ya kutwaa kombe la UEFA.

Kipindi cha pili magoli ya Xabi Alonso,Vladmir Smicer na kapteni Steven Gerrad yaliifanya iwe 3-3.Baada ya kumalizika kwa sare ilibidi fainali iamuliwe kwa mikwaju ya penati ambapo Liverpool waliibuka kidedea kwa penati 3 kwa 2.
 
Screenshot_2017-03-10-09-00-49-1.png
 
bebweni na nyie[emoji3] [emoji3]
Mbeleko, mbeleko. Barca imepigwa mbeleko.

Ipo haja ya Mwamuzi na yule msaidizi wake kuchunguzwa kwa kuwapa Barca penalti 2 za bure. Wanaharibu kandanda.
 
Number of teams who lost 4-0 in the first leg of a UCL game: 145

Number of teams who qualified the next game: 1

This is Barça.
 
Neymar na Rafinha hawatacheza mechi ya leo .

BARCELONA

The big news coming out of Catalunya today is that Rafinha and Neymar both missed training through illness and injury respectively; the Brazilian pair are both absent from Luis Enrique’s squad for tomorrow’s match and that is sure to be a big blow for the Blaugrana. Neymar is of course a sensational player and any team would be weaker without him, while Rafinha has been influential in Barcelona’s switch to a 3-3-1-3.


The question therefore is whether Enrique will persevere with that system without two key players, or whether he will revert to a 4-3-3 and if that will be enough to defeat Deportivo.

I suspect that Enrique will revert to a 4-3-3, if only because of the personnel at his disposal. Sergi Roberto and Jordi Alba will start on either flank, with Gerard Pique and Samuel Umtiti together in the centre of defense. Sergio Busquets, Ivan Rakitic and Andres Iniesta are likely to start in midfield, with Andre Gomes and Denis Suarez both likely to push for staring berths, then Arda Turan will replace Neymar in attack.
 
Back
Top Bottom