FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

J.S Park hawezi kumzuia Messi kabisa, Messi anataka mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kukaba na kuzunguka uwanja mzima. Kumbuka ishu nyingine inatakiwa supply ya mipira kuelekea kwa Messi ipunguzwe sana au iwe blocked kabisa. Shida ya Messi akishaweka mpira mguuni kuuchukua ni either umfanyie faulo au otherwise anakuacha. Faulo kadhaa kwa Messi lazima zitaelekea kutolewa kwa kadi. Hivyo basi Messi anahitaji timu iliyojipanga vema sana kwenye diffence. Na kwa tactics ya mpira kama ushacheza, sio rahisi kwa mtu anayetumia mguu wa kushoto kukabwa na mtu anayetumia mguu wa kushoto.

Utakuwa mdau wa chelsick bila shaka wewe, Kama mara hii tu umejitahidi kusahau aliyepeleka kiama nyumbani kwenu basi subiri aibu jmosi.

SAF ameshasema ameandaa timu yake kukabiliana na tiu ya barcelona, hii habari ya messi inawapa pressure sana wanazi wa chelsick na asenali.

Safari hii barcelona hatoki, hakuna cha messi, david villa wala pedro wote watashikwa vizuri tu na man u anatoka na ushindi wa 2-0!!
 
Natamani Barca ifungwe siku hiyo. Uchambuzi wa muanzisha thread ni wa kitaalamu pia (Na actually kimsingi ndiyo ukweli wenyewe).
 
Observer analysis yako imekaa kitanzania Tanzania sana... Hivi katika Man Utd kuna mchezaji anayezunguka uwanja mzima kuanzia dakika ya mwanzo hadi mwisho zaidi ya Park?

Lazima uwe wa Kitanzania ndugu yangu cause I am typical Tanzanian. Sitegemei uchambuzi wangu kama Mtanzania uwe wakinaijeria au wa kifaransa etc etc !!!

Kuhusu Park, hakuna ubishi ni kiungo mzuri sana kwenye kukaba na kushambulia na ndio maana Sir AF huwa katika mechi yoyote ngumu lazima ampange J. S Park, ila unavyosema atamkaba Messi (kwa maana kuwa ndio litakuwa jukumu lake la msingi) ndio hapo kama itatokea kweli (though nauhakika Sir AF hawezi fanya huo utani) basi kutatokea msiba mzito OT. Nimegusia somewhere kuwa kitaalam, mtu anayetumia mguu wa kushoto ni kazi sana kukabwa na mtu anayetumia mguu wa kushoto and vice versa. Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mbinu za soka utagundua siku hizi makocha wengi wanapenda kumpanga mtu anayetumia kushoto namba 7 (ili akabwe na beki namba 3 ambao majority wanatumia mguu wa kushoto) na pia mtu anayetumia mguu wa kulia anapangwa namba 11 ili akabwe na namba 2 anayetumia mguu wa kulia. Kwa mifano michache tu, mwangalie Aarjen Robben na Frank Ribbery wa Bayern Munich. Kumbuka Thiery Henry wa Arsenal, alikuwa always anashambulia tokea kushoto. Leonel Messi mara nyingi huwa anashambulia tokea kulia, Andres Iniesta mara nyingi anatokea kushoto etc, mifano ni mingi sana ya kuonyesha hiki ninachokuambia.

Anyway, hizi ni pre match analysis. Ngoja tusubiri hiyo kesho.

Cheers !
 
Lazima uwe wa Kitanzania ndugu yangu cause I am typical Tanzanian. Sitegemei uchambuzi wangu kama Mtanzania uwe wakinaijeria au wa kifaransa etc etc !!!

Kuhusu Park, hakuna ubishi ni kiungo mzuri sana kwenye kukaba na kushambulia na ndio maana Sir AF huwa katika mechi yoyote ngumu lazima ampange J. S Park, ila unavyosema atamkaba Messi (kwa maana kuwa ndio litakuwa jukumu lake la msingi) ndio hapo kama itatokea kweli (though nauhakika Sir AF hawezi fanya huo utani) basi kutatokea msiba mzito OT. Nimegusia somewhere kuwa kitaalam, mtu anayetumia mguu wa kushoto ni kazi sana kukabwa na mtu anayetumia mguu wa kushoto and vice versa. Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mbinu za soka utagundua siku hizi makocha wengi wanapenda kumpanga mtu anayetumia kushoto namba 7 (ili akabwe na beki namba 3 ambao majority wanatumia mguu wa kushoto) na pia mtu anayetumia mguu wa kulia anapangwa namba 11 ili akabwe na namba 2 anayetumia mguu wa kulia. Kwa mifano michache tu, mwangalie Aarjen Robben na Frank Ribbery wa Bayern Munich. Kumbuka Thiery Henry wa Arsenal, alikuwa always anashambulia tokea kushoto. Leonel Messi mara nyingi huwa anashambulia tokea kulia, Andres Iniesta mara nyingi anatokea kushoto etc, mifano ni mingi sana ya kuonyesha hiki ninachokuambia.

Anyway, hizi ni pre match analysis. Ngoja tusubiri hiyo kesho.

Cheers !

Haya bwana observer nimeziona sababu zako tano, sijui ni observer wewe au observer mwingine.
 
Nikiwa kama mchambuzi wa soka nisiye shabiki wa timu yoyote duniani (ukiondoa Tanzania), hizi hapa nazitoa ni sababu 5 kati ya nyingine kadhaa zitakazoifanya FC Barcelona kuifunga Man U tarehe 28/05/2011. Ukiweza soma taratibu mstari kwa mstari, nimejaribu kufupisha sana angalau nisiweze kukuchosha.
  1. Ubora wa Kikosi
Hakuna ubishi kuwa hii ni fainali inayokutanisha timu mbili bora zaidi duniani kwa sasa. Wachambuzi wa soka tunaamini Barcelona ndio timu bora kuliko zote duniani kwa sasa na Man U ni timu ya pili kwa ubora kwa sasa. Ukiangalia kwa udani, utagundua kikosi cha Man U kimekosa ubora wa kiwango cha juu katika msimu huu ukilinganisha na misimu ambayo Man U ilitwaa ubingwa wa UCL (2008,1999). Ukiangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa FC Barcelona na Man U utaona fika kwamba kikosi cha Barca ni bora zaidi. Man U ina wachezaji wenye ubora, lakini wachezaji wenye ubora wa juu kabisa binafsi nawaona ni Edwin Van Der Sar, na beki nguli, kisiki cha mpingo Nemanja Vidic. Ili Man U iweze kuwa bingwa basi hawa wachezaji wawili ndio watakuwa nyota wa mchezo. Kuna makosa mengi ambayo Sir AF huwa anakubali kuwa aliyafanya na yaliicost Man U, kati ya yote ukimuuliza ni kosa lipi kubwa sana alilifanya atakuambia, pamoja na kumuuza beki nguli Jaap Stam bila kuwa na replacement, kosa kubwa zaidi alilolifanya ni kutomnunua Edwin Van Der Sar baada ya Peter Schmeichel kustaafu mwaka 1999.
Kwa tathmini ya one to one, FC Barcelona ni bora zaidi ya Man U.

  1. Kutokuwa na Consistence
Kikosi cha Man U msimu huu kimekosa consistence, ukiangalia tathmini ya msimu huu utagundua wachezaji wa Man U wamekuwa na ups na downs nyingi. Kuna mechi wanaweza cheza vizuri mno, lakini kuna mechi wanacheza hovyo kabisa, hii sasa inawaweka njia panda, kama siku ya fainali watakuwa down basi dhahama itawakumba. FC Barcelona wamekuwa katika kiwango cha juu msimu mzima. Hata game wanayofungwa unaona kabisa timu pinzani lazima ifanye kazi ya ziada sana sana sana. Japokuwa wachambuzi wa soka tunaamini FC Barca bado haijaweza kuwa katika kiwango chao walichofikia mwezi wa December, 2010 ila bado wanacheza katika consistence ya hali ya juu mno.

  1. Ukosefu wa Mchezaji Kiongozi
Baada ya Man U kupata tabu sana katika mechi ya kwanza iliyochezwa Old Trafford kwenye nusu fainali ya UCL 1999 na Juventus, goli la Ryan Giggs la dakika ya 90 likiwa la kusawazisha baada ya Antonio Conte kuwapa goli la kuongoza Juventus, kila mmoja alijua mechi ya marudiano jijini Turin, Man U angeangamizwa vibaya. Kumbuka Juventus ilikuwa inaongozwa na viungo bora kabisa Zinedine Zidane na Edgar Davids. Kweli, kwenye mechi ya marudiano baada ya magoli mawili ndani ya dk 11 za kwanza ya Fillipo Inzaghi kila mtu alijua Man U washatolewa. Inapofika sasa katika hali kama hii ndio hapo timu inahitaji mchezaji kiongozi. Kwa sasa Man U haina mchezaji wa kuinyanyua timu inapokuwa imelowa. Enzi zile walikuwa na kiungo, mwongoza timu Roy Keane. Yaliyotokea baada ya Roy Keane kufunga goli la kwanza la kurudisha matumaini dk ya 34 ya mchezo naamini wote mnayakumbuka.

  1. Nje ya Uwanja
Nje ya uwanja Man U ipo katika wakati mgumu sana. Ni ukweli usiopingika kuwa Man U wanaingia katika hili game la tarehe 28 wakiwa hawana uhakika mkubwa wa ushindi kama FC Barcelona. Kuingia kwenye game kama underdogs kawaida huwa kunakuwa na madhara sana especially pale mambo yanapoenda kinyume na matarajio dakika za mapema. Endapo Man U itaanza kufungwa uwezekano mkubwa mpira ukaisha mapema hata kabla ya dk 90, kwa wanaojua soka nadhani mmenielewa ninaposema mpira utaisha mapema. Kiujumla nje ya uwanja Barcelona wapo katika saikolojia nzuri zaidi kuliko Man U.

  1. Trio
Ofcoz, Trio ni sababu kubwa ya 5 ya Man U kufungwa tarehe 28. Hawa watu watatu wataigharimu sana Man U kuweza kuwadhibiti dakika zote 90 za mchezo. Nionavyo ni kwamba kwa sababu Pep anajua Man U ina ukuta mgumu sana katikati, atakachofanya ataanza kwa kushambulia tokea pembeni huku akiwa hana namba 9. Lionel Messi atacheza deep kama kiungo akiwa anatumika kama virtual centre forward hii itamfanya asiweze kukabwa na Vidic au Ferdinand. Wakati Messi atacheza kama kiungo, David Villa atakuwa anashambulia zaidi kwa kutokea kulia huku Pedro Rodriguez na Andres Iniesta watakuwa wanashambulia tokea kushoto. Hii itawalazimisha Nemanja Vidic na Rio Ferdinand kutanuka pembeni ili kuwasaidia mafullback Patrice Evra na kulia sina akika ataanza Fabio au Raphael, ila binafsi ninaamini akianza John Oshea itakuwa advantage kwa Man U maana yupo physic kuliko mapacha na pia anauwezo mkubwa wa kukaba na kuoverlap. Kutanuka kwa hawa centre defenders kutatoa mwanya kwa Xavi Hernandez na Andres Iniesta kusupply mipira kwa Lionel Messi. Mbinu pekee ambayo itawasaidia Man U kuweza kuwadhibiti hawa Trio ni kuanza kwa kutumia double holding midfielders, Darren Fletcher na Michael Carrick. Sina hakika sana na fitness ya Fletcher kwa ajili ya huo mpambano, maana japokuwa amecheza mechi ya mwishoni mwa msimu lakini bado fitness yake ina mashaka kidogo especially kwa sababu ya ugumu wa mechi yenyewe.
Ni jinsi gani Sir AF ataweza kuwadhibiti hawa vijana wa Barca, lets wait and see.

Cheers.

Good analysis: but as Manchester United Fans we can't give up, we know exactly that ''Nothing is Impossible Under Much Struggle''.
 
....walete, walete, waleteeeee!!! and the countdown finally starts....he he he
Wacha1, Ab-tichaz, ...mwageni picha mpaka kieleweke hapa leo...

Kuna watu weshaanza kutafuta visingizio humu, ooh....TANESCO, oooh, Server Down,...leo hakuna cha mgao wala
maintenance...wote mje hapa...Manda, Mfarisayo, sijui Kiduku....
Eqlypz hujalala ee...posts zako zipo hewani 24hrs ha ha ha... presha presha preshaaaaa!

BelindaJacob, mbona leo umevaa jezi ya Barcelona, kulikoni? ...ha ha ha!
 
Mbu, mambo ya timezone babu -8 GMT Ndio napanda kitandani sasa...! Ebanae niko nervous kama 99 na 08...!
Ila tutabanana hapa hapa.
 
Guardiola_2600425.jpg


Josep Guardiola looks cool and calm answering questions
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Iniesta_2600426.jpg


Andres Iniesta takes on water. The Spanish ace is sure to be a key performer at Wembley


IniestaValdes_2600427.jpg



MascheranoPique_2600429.jpg


Former Liverpool man Javier Mascherano puts Gerard Pique under pressure
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Messi2_2600430.jpg


Lionel Messi, who many regard at the best in the world, will be the one United will be watching the most.


Messi_2600431.jpg



PuyolMessi_2600433.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom