Maoni ya Mbu;
...kuna wachezaji wana Gundu!...
Ashley Cole na Thierry Henry! Kamwe hawataweza kuvaa medali za Champions League, wala World Cup wanazozitafuta kwa udi na uvumba.
Hawa wawili waliondoka Arsenal wakiwa miongoni mwa ile invincibles team, waliotwaa FA cup, na Premier league title. Wachezaji hawa wawili (kutokana na majeraha) hawakufikiriwa wangecheza Champions league final 2006 baina ya Arsenal vs Barcelona, ingawa dakika za mwisho Arsene Wenger aliwapanga. Hata katika team zao za taifa, matokeo yamekuwa mabaya pamoja nakwamba wachezaji hawa wana vipaji pekee!
Kwa "gundu" hilo, mwaka jana Chelsea ilifungwa fainali na Man U, Ashley Cole akiwa mchezaji siku hiyo. Mwaka huu wametolewa na Barca kwenye nusu final.
May 27, Thierry Henry atakuwemo kwenye team, lakini Man United ndio wataoibuka kidedea. Binafsi nipo neutral, kwani naamini itakuwa mwisho mzuri kwa Man United Great players, Ryan Giggs na Paul Scholes...
Wakati huo huo kelele za kina Icadon zitani bore hapa, hivyo nitajisikia raha Josep "Pep" Guardiola, akitwaa rasmi taji la "the special one!"
Signed; ....Bzzzzzzzzz!